Jamani naombeni msaada wenu, mke wangu katapelewi Magufuli stand

Ukiwa unafanya kitu chochote fanya utafiti kwanza ameshindwa hata kuulizia magari ya songea ni yapi na baadhi ya details
 
Mjukuu sisi wazee wa zamani wakati wa ujana wetu hatukuwa kama nyinyi,mnaopotezewa mda wenu na serikali,na hatukuwa tunan'ga'ngania kuishi kwa wazazi na elimu kwetu haikuwa kipaumbele lakina tulikuwa na uwezo mkubwa wa kujua mambo,nikiwa na miaka 20 nilikuwa namiliki paspoti kubwa tena ya inchi ambayo hata Lugha yake siijui kiufasaha sijui hapo ulipo mwenzangu uko wapi?
Niliondoka Nyumbani kwa kutoraka siyo kwa kuaga,maana tuliamini kuaga ni mkosi nililudi nyumbani nikiwa na miaka 22, na kuondoka na madogo zangu wawili
Changamoto yetu huku tuliko huwezi kuowa wanawake wa huku,ukijiloga wanakuuwa,wanachojali wao ni pesa yako na watoto uliowazalisha na siyo mzee kivile ninacheza na 49,nime

Yaani hunijui tu,kwanza niseme hakuna mjinga ambaye anaweza kujiunga na jamii forum,pili mimi nacheza na rate za Dola,Rand,Miticals,Kwacha,,mpaka shilingi,
Sijui unanipata lakini? Hizo ni hera ambazo unaposafiri kila unapofika border moja kwenda nyingine lazima uzibadilishe,na inabidi uujue mkato wake ili wajanja wasikuibie,na huyo aliyetapeliwa basi maana yake akifika border ya Tanzania na Mozambique kwa jina la mkenda na kwa upande wa Mozambique Congreso itabidi azibadilishe ili apate miticals,na akifika maputo inabidi abadilishe Miticals ili apate Rand,sijui unanielewa,
Sasa sijui wewe na mkeo wenye akili mnaliweza hilo?
Mimi nimeomba msaada sababu siko Tanzania,ningekuwepo Tanzania mbona nawamudu vizuri tu,najua humu wako watu tofauti wenye uzoefu tofauti na ueleo tofauti ambao wangenisaidia kimawazo
Haya maelezo yote hayana maana kabisa, wewe umepata wa kufanana nae,
Unacheza na dola na rand usingempandisha mkeo basi mkweche mpaka anatapeliwa kijinga namna hiyo, wala usingelia lia na hiyo elf 70
 
Jamani naombeni msada wenu,mke wangu alikuwa anaenda Songea kufika Mbezi wakamtapeli wakamkatia tiketi ya basi la kwenda kyela lenye jina la Kyela Express
Alipoomba msaada hakuna aliyemsikiliza mpaka gari za Songea zikaondoka, jibu walilompa ni kwamba watampeleka Songea,
Namba ya Hilo gari ni G 987 AWY na hayuko yeye peke yake kuna abilia mwingine na nauli waliyomkatia ni ya mpaka Kyela badala ya Songea
Hajui kusoma ?
 
Nimeuliza ukiwa ndani ya basi?
Kama basi alijatoka stendi shuka nenda kituo cha polisi humo Magufuli Bus Terminal.
Kama limetoka mpo njiani mkifika walipo Traffic police apige kelele kuomba msaada.
Au piga simu LATRA mamlaka ya usafiri hotline 0800110020.
Hizi smartphone mnafanyia kazi gani?
 
Poleni, nadhani zipo mamlaka kama LATRA zinaweza saidia ila isije ikawa mkeo ana mpango wa kulala Kyela kidogo.
 
Jamani naombeni msada wenu,mke wangu alikuwa anaenda Songea kufika Mbezi wakamtapeli wakamkatia tiketi ya basi la kwenda kyela lenye jina la Kyela Express
Alipoomba msaada hakuna aliyemsikiliza mpaka gari za Songea zikaondoka, jibu walilompa ni kwamba watampeleka Songea,
Namba ya Hilo gari ni G 987 AWY na hayuko yeye peke yake kuna abilia mwingine na nauli waliyomkatia ni ya mpaka Kyela badala ya Songea
Pole sana mkuu hapo Mbezi pana kituo cha polisi na dawati la wasafirishwaji kupeleka malalamiko jaribuni kwenda hapo watawapatia msaada, Mbarikiwe sana.
 
Inashangaza kukosa umakini nao ni janga
Hapo hakuna umakini zaidi ya kutapeliwa abiria kwa kupotoshwa na mawakala.

Wanakuwa na ushindani wa 'kujaza', kwa hiyo wanahadaa na kupokea abiria yeyote mwenye kuelekea njia hiyo na kuwafaulisha kwenye magari mengine njiani.

Hizo ndizo adha za booking 'manually'.

Njia sahihi ni online booking, ama kukatia ticket asubuhi ndani ya bus husika wakati safari inaanza.
 
Unajua wapiga debe kawaambia anaenda Songea wakamkatie tiketi ya kwenda Kyela na hayuko peke yake yuko na abilia mwenye tatizo kama lake,na kumbuka Songea nauli 64,000 wakati Kyele 76,000
Nauli ya Kyela 76000?
Kweli mmetapeliwa
 
Watamfaulisha! Hata mimi wakati naenda tanga mabasi yote yalikuwa yamejaa nikakata tiketi la basi linaloenda gonja wakanishusha handeni vijijini pale stend karibu na round about kulikuwa na coastal zinazoenda tanga wakanilipia nauli makonda wa basi la ngoja nikafika tanga kwa 20000
 
Haya maelezo yote hayana maana kabisa, wewe umepata wa kufanana nae,
Unacheza na dola na rand usingempandisha mkeo basi mkweche mpaka anatapeliwa kijinga namna hiyo, wala usingelia lia na hiyo elf 70
Mkuu unasagia kunguni, mpumzishe anastress za mke kufaulishwa [emoji23]
 
Jamani naombeni msada wenu,mke wangu alikuwa anaenda Songea kufika Mbezi wakamtapeli wakamkatia tiketi ya basi la kwenda kyela lenye jina la Kyela Express
Alipoomba msaada hakuna aliyemsikiliza mpaka gari za Songea zikaondoka, jibu walilompa ni kwamba watampeleka Songea,
Namba ya Hilo gari ni G 987 AWY na hayuko yeye peke yake kuna abilia mwingine na nauli waliyomkatia ni ya mpaka Kyela badala ya Songea
Songea mbona kuna kampuni kubwa tu na zina ofisi zinaeleweka? Yaani hadi leo bado kuna watu wanakata tiketi kwa watu au kampuni zisizoeleweka? Waendelee kutupiga hadi tunyooke. Hiyo namba ya gari ipeleke olisi kitengo cha usalama barabarani.
 
Jamani naombeni msada wenu,mke wangu alikuwa anaenda Songea kufika Mbezi wakamtapeli wakamkatia tiketi ya basi la kwenda kyela lenye jina la Kyela Express
Alipoomba msaada hakuna aliyemsikiliza mpaka gari za Songea zikaondoka, jibu walilompa ni kwamba watampeleka Songea,
Namba ya Hilo gari ni G 987 AWY na hayuko yeye peke yake kuna abilia mwingine na nauli waliyomkatia ni ya mpaka Kyela badala ya Songea
Nitumie namba yake nimsaidie kwa haraka. Kama hatojali nimpe lift mi naenda Songea na private asubuhi hii
 
Duuh pole sana mkuu, bahati mbaya mida naona hii post msaada kwa sasa tumeshachelewa.

Magari ya jioni kwa muda aliotoka yale ya kuja songea ndio muida hii yanafika songea, hapo kama wamemshusha makambako basi wangempakia kwenye super feo au new force, lakini pia jitahidi kumuelekeza mkeo kwa ufasaha na awe Shap kwa sasa unatarajia aingie boda ya Mozambique je ataelewana na wale jamaa wanaotumia kireno muda mwingi?

Pole sana kama ikiwezekana tumpokee shemeji hapa songea tumpe maelekezo mazuri ya kufika boda ya msumbiji nipo lilambo hapa kwa sasa.

Ilitakiwa atoe taarifa stand yoyote walioingia watu wa latra wapo na polisi wapo alitakiwa aende kwa hizo mamlaka awepe tarifa, Latra huwa wanakuwa mikese na mikumi wakati mwingine kwa ajili ya ukaguzi wa tiketi na kuulizia changamoto kama hizi.

Kingine jitahidi sana mtu anapokuwa safarini awe na simu yenye kukaa na chaji muda mrefu, wanawake kiukweli wanamadhaifu ila ninwajibu wetu kuwasimamia ipasavyo.

Huduma za wasafirishaji kwa Tanzania ninza hovyo sana wiki moja iliyopita nilipata mkasa kidogo nilikatia mtu toketi online bus la shabiby kutoka dar kwenda dodoma, bahati mbaya muhusika alipata emergency alfajiri nikajaribu kuwapa taarifa wahusika, kwanza simu naambiwa ile namba ni ya dodoma hivyo niwasiliane na watu wa dar

Nikawaambia nyie ni wababaishaji, kama umeweka namba hapa kwa tatizo lolote niwasiliane na hii namba mliweka mkiwa mnakusudia mpigiwe kwa matatizo yapi?

Mbona mnatoa huduma kihuni namna hii??
Nikapigia hiyo ya dar haikupokelewa kabisa na mara nyingine unaambiwa inatumika, sasa unona jinsi haya makmpuni ya usafirishaji yanavyoendeshwa na wahuni na watu wasiojali huduma kwa wateja, kurudi tena kwenye namba ya dodoma wakawa hawapokei simu kabisa baada ya kujua ninaewapigia nina shida gani.

Hivyo huduma za huko Sudi Africa ulipo huku kwetu ata robo yake hauwezi kuipata.

Mwisho wa siku niliacha nauli ile ipotee ingawa si kubwa sana ilikuwa 35 elfu tuu lengo ilikuwa kuwajulisha tunabdili muda wa safari.
 
Mjukuu sisi wazee wa zamani wakati wa ujana wetu hatukuwa kama nyinyi,mnaopotezewa mda wenu na serikali,na hatukuwa tunan'ga'ngania kuishi kwa wazazi na elimu kwetu haikuwa kipaumbele lakina tulikuwa na uwezo mkubwa wa kujua mambo,nikiwa na miaka 20 nilikuwa namiliki paspoti kubwa tena ya inchi ambayo hata Lugha yake siijui kiufasaha sijui hapo ulipo mwenzangu uko wapi?
Niliondoka Nyumbani kwa kutoraka siyo kwa kuaga,maana tuliamini kuaga ni mkosi nililudi nyumbani nikiwa na miaka 22, na kuondoka na madogo zangu wawili
Changamoto yetu huku tuliko huwezi kuowa wanawake wa huku,ukijiloga wanakuuwa,wanachojali wao ni pesa yako na watoto uliowazalisha na siyo mzee kivile ninacheza na 49,nime

Yaani hunijui tu,kwanza niseme hakuna mjinga ambaye anaweza kujiunga na jamii forum,pili mimi nacheza na rate za Dola,Rand,Miticals,Kwacha,,mpaka shilingi,
Sijui unanipata lakini? Hizo ni hera ambazo unaposafiri kila unapofika border moja kwenda nyingine lazima uzibadilishe,na inabidi uujue mkato wake ili wajanja wasikuibie,na huyo aliyetapeliwa basi maana yake akifika border ya Tanzania na Mozambique kwa jina la mkenda na kwa upande wa Mozambique Congreso itabidi azibadilishe ili apate miticals,na akifika maputo inabidi abadilishe Miticals ili apate Rand,sijui unanielewa,
Sasa sijui wewe na mkeo wenye akili mnaliweza hilo?
Mimi nimeomba msaada sababu siko Tanzania,ningekuwepo Tanzania mbona nawamudu vizuri tu,najua humu wako watu tofauti wenye uzoefu tofauti na ueleo tofauti ambao wangenisaidia kimawazo
yaani anauzoefu na safari zote hzo na bado katapelewa kwa magufuli.. basi tatizo ni kubwa zaidi poleni sana.
 
Haya maelezo yote hayana maana kabisa, wewe umepata wa kufanana nae,
Unacheza na dola na rand usingempandisha mkeo basi mkweche mpaka anatapeliwa kijinga namna hiyo, wala usingelia lia na hiyo elf 70
Unajua wewe siyo kila kitu cha kujibu humu ndani wewe mimi siyo boy naludia tena,siwezi kuandika kila kitu kilivyo sijaja kukuomba msada wa hela wala chakula,na nimesaidia watu wengi hasa wanawake wanaopatwa na matatizo njiani kama kuishiwa na hera na kila kitu
Inchi yenye watu matapeli na roho mbaya ni Tanzania tuliyozaliwa kwa bahati mbaya chini ya mkoloni mweusi CCM, unashanga stend kuna wapiga debe,
tunashindwa na kainch kadogo kama Malawi
inaonekana una stress zako za maisha pole sana ndugu yangu,
Nilipita njia ya Mozambique to Malawi kupitia border ya Dedza,kufika Lilongwe nikaambiwa sasa hivi kuna stand mpya zinakopaki basi, Safari yangu ilikuwa ya Lilogwe Mzuzu to border kalonga nilipofika nikakuta stende ya kistarabu safi kubwa kama ya Magufuri hakuna hata mpiga debe,wala muuza mandazi tabiya mbaya za Watanzania zinaanzia unapovuka border kuingia Tanzania ,kwa border zote yaani utasikia braza tukusaidie,ni usumbufu sana mpaka kwa wageni
 
Ukiwa unafanya kitu chochote fanya utafiti kwanza ameshindwa hata kuulizia magari ya songea ni yapi na baadhi ya details
Siyo kuulizia tu nina mpaka namba zao wahusika na mwezi uliopota nilikuwa Tanzania,nilipitia njia ya lindi kwenda Dar na nikaambiwa kutakuwa na route mpya ya Maning nice
Nitumie namba yake nimsaidie kwa haraka. Kama hatojali nimpe lift mi naenda Songea na private asubuhi hii

Hajui kusoma ?
Kusoma kunasaidia nini? Au kuajiliwa na ambao hawakusoma,mbona sasa hivi hata bodaboda wasomi,naongea lugha zaidi ya sita nitajilinganisha na wewe uliyesoma?
 
Back
Top Bottom