Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 32,639
- 42,908
Laana hii....Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Marwa Menganyi mkazi wa Kijiji cha Keroti wilaya ya Tarime mkoani Mara anadaiwa kumuua mtoto wake, Celine Marwa, mwenye umri wa miezi minne kwa kumbana pumzi kisha kumtumbukiza kwenye jaba.
Imeelezwa kuwa alifanya hivyo ili achangiwe pesa na kikundi aweze kulipa madeni yake.
Hata kama ndio hivyo ila kuua mtoto wa miezi minne ni zaidi ya unyama.Huyo atakuwa alihisi hata huyo mtoto sio wake.
Huenda huyo jamaa ana matatizo ya akili, wasisahau kumpima hili.