1)MAADILI KUSHUKA KATIKA JAMII
Hofu ya Mungu kushuka
Uzinzi michepuko fasheni
Dhambi imekuwa kitu cha kujisifia
2)NAFASI YA MWANAMKE IMEPANDA
Wanawake wamepanda ki ELIMU kujua haki zao na wanazitetea wanatetewa,nafasi za usawa katika sekta zote uongozi pia ,pia wapambanaji wanatafuta pesa,wanafanya baadhi ya shughuli/kazi zinavyofanywa na wanaume .
3)NDOA HAIHESHIMIWI
Kuachana imekuwa ni rahisi tu,kuwa single mother single father ni kitu cha kawaida,uvumilivu umepungua au haupo.
4)KUTOJITAMBUA KUKOSA AKILI/BUSARA/ULIMBUKENI
Kuna wanaotema bigi ji kwa karanga za kuonjeshwa.
Kuna wanaopata bahati au neema ya kuwapata wenza sahihi ila wanawaacha na kuamua kwenda kwa wanaume masharobaro au wanawake wenye muonekano mzuri au makali makubwa lakini wasio na akili.Mpumbavu huibomoa ndoa yake kwa mikono yake mwwnyewe badala ya kuijenga.
Mwisho wa siku wakitendwa huko walikokimbilia ndio hukumbuka shuka na kutaka kuyarudia matapishi.
5)KUKOSA UNYENYEKEVU
EGO kuwa juu kuna wakati inabidi kwenye baadhi ya vitu ujishushe uwe mjinga na yeye kuna baadhi ya vitu awe mjinga ili mfike kati kati mwende sawa.Yani kuna vitu kila mmoja havipendi kitoka kwa mwwnzake kila mmoja awe tayari ku compromise ili mfike kati.KUSIKILIZANA ,KUVUMILIANA ,KUHESHIMIANA.
6)UPENDO ndio cha mwanzo unatakiwa ujue kwanini mwenza wako ameamua kuwa na wewe na wewe kwa nini umeamua kuwa na yeye.Kupata muda wa kuchunguzana na kujua kuna upendo .Kama ni mwenzako anakuhitaji kama wewe unavyomuhitaji yeye.Yani mapenzi ya upande mmoja.
Mi naamini kama una akili timamu inteligence ndogo ya kumsoma au kumchunguza mtu,ni rahisi kujua huyu mwenza niliyenaye ana sifa za kuingia naye kwwnye agano la ndoa au hapana.Kusoma dalili ya mvua ni mawingu.Mana anayejipiga mwwnyewe halii.Yani kuna sehemu unajichomeka unaona kabisa hapa ni kwenye hamna unategemea atakuja kubadilika ndani ya ndoa sio rahisi.
Kama kulikuwa na uzi kuna mtu alikuwa anasema anataka aoe baa medi sasa ina maana huyu anataka kubadilisha daladala iwe gari binafsi,au sumu kwa kuionja
Ipo njia ionekanayo njema machoni pa mwanadamu ila mwisho wake ni mauti
NI VIZURI TUONGOZWE NA AKILI SIO HISIA ZA MAPENZI
Pia tuongozwe na Mungu katika kupata mwenza sahihi.
NI BORA KUZIBA UFA KULIKO KUJENGA UKUTA.
Ni bora kuachana katika hatua ya uchumba kabla ya ndoa kama utapata muda wa kutosha wa kuchunguzana katika hatua ya uchumba kabla ya ndoa.,kuvunja uchumba ni bora kuliko kuvunja ndoa.