Jamani, tuwe wakweli: Hali ni mbaya siyo kwenye Ndoa pekee bali hata Mahusiano mengine

Jamani, tuwe wakweli: Hali ni mbaya siyo kwenye Ndoa pekee bali hata Mahusiano mengine

Tumeikanyaga mifumo ya asili, tumeacha kuishikwa zile kanuni za mwanzo. Usitegemee tubaki salama...
 
Ndoa ni tatizo kubwa sio dogo na tatizo kubwa ni Mwanaume kurudisha mpira kwa kipa hasa akiteteleka kipato Wanawake wengi wa mjini sio wavumilivu wanataka kila siku uwe na pesa na ndio maana unaona sehemu wanazouza vilevi zinajaa sana mtu anaona bora arudi nyumbani mwenza wake akiwa amelala kupunguza zogo.
Kabisa mkuu.ndomaana wanandoa wengi wanadanga sana.
 
Sababu ni zile zile!
  • Lack of support
  • Lack of employment opportunities
  • Lack of funds
 
Kila kitu katika maisha kinaanzia na mtazamo wa mtu binafsi. Suala la changamoto za ndoa au mahusiano hayawezi kumalizwa na dini,,wazazi au yeyote yule bali ni mtazamo binafsi wa mtu. Wengi wameumizwa kwenye mahusiano waliyokuwa nayo before matokeo yake anapokutana na mtu mwingine utasikia siwezi kumuonyesha upendo kama wa mwanzo kwa sababu wote ni wale wale. Lkn mtu anasahau binadamu wametofautiana ktk malezi na makuzi yao.

Mwingine anawekeza kwenye mapenzi ili apende au apendeke. Lkn anasahu kuwa unapoamua kufanya jambo fulani fanya kwa sababu moyo wako ni mzuri sio kwa sababu ya kumfurahisha mtu.

Wengine wanaanza mahusiano mapya moyoni wakiwa wamewabeba watu waliowajeruhi.

Tukibadili mtazamo kila kitu kitakuwa sawa. Niliwekeza kwa mtu kaniacha basi sawa hakuwa fungu langu. Kikubwa unapopenda usisahau akili nyuma nenda na akili zako.
 
Kumetokea nini kwenye jamii ya Sasa mbona kila sehemu NDOA zimekuwa shubili Yani amani hakuna furaha ya MAHUSIANO hakuna tabu tupu shida ni nini?
Si ndoa na mahusiano tu. Jamii nzima imekosa trust.

Hivyo mambo yameharibika kuanzia kwenye familia mpaka siasa za nchi.
 
Back
Top Bottom