Kila kitu katika maisha kinaanzia na mtazamo wa mtu binafsi. Suala la changamoto za ndoa au mahusiano hayawezi kumalizwa na dini,,wazazi au yeyote yule bali ni mtazamo binafsi wa mtu. Wengi wameumizwa kwenye mahusiano waliyokuwa nayo before matokeo yake anapokutana na mtu mwingine utasikia siwezi kumuonyesha upendo kama wa mwanzo kwa sababu wote ni wale wale. Lkn mtu anasahau binadamu wametofautiana ktk malezi na makuzi yao.
Mwingine anawekeza kwenye mapenzi ili apende au apendeke. Lkn anasahu kuwa unapoamua kufanya jambo fulani fanya kwa sababu moyo wako ni mzuri sio kwa sababu ya kumfurahisha mtu.
Wengine wanaanza mahusiano mapya moyoni wakiwa wamewabeba watu waliowajeruhi.
Tukibadili mtazamo kila kitu kitakuwa sawa. Niliwekeza kwa mtu kaniacha basi sawa hakuwa fungu langu. Kikubwa unapopenda usisahau akili nyuma nenda na akili zako.