Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza; Mvuvi Nigeria atafuna samaki mwenye thamani ya mabilioni ya shilingi bila kujua

hii habari ilinichekesha sana, nlimuwazia sana mwamba alivopata mawazo lukuki baada ya kupata hizo taarifa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
kwani baharini kuna ukuta mkuu?
 
Umasikini na njaa kama chupi na tako tu
 
Bahari ya Hindi tumewavua Sana deep sea wanafika Hadi kilo Mia Tatu huku wanaitwa Samusuli Wana msumeno mbele
Huko mlipowavua mnaruhusiwa kufika ilo eneo
 
kwani baharini kuna ukuta mkuu?
soma kilichoandikwa. wanapatikana bahari ya pacific TU. unadhani samaki nao wanazurura zurura kama wewe?ndo maana kuna samaki huwezi wapata huku TZ ila unawapata sehemu nyingine mbali huko. na hizi ni bahari zenye maji yenye sifa tofauti
 
Unaambiwa usilolijua ni sawa na usiku wa giza na hilo limemtokea mvuvi mmoja huko nchini Nigeria aliyefahamika kwa jina la Zion Godwin ambaye amemvua samaki aina ya 'Blue Marlin Fish' mwenye thamani ya Tsh Bilioni 6 lakini amemla yeye na marafiki zake kijijini.

Taarifa hiyo imesambaa zaidi kwenye mitandao ya kijamii baada ya jamaa huyo kushea picha ambazo zilionesha akiwa ametoka baharini kumvua samaki huyo lakini kwa sababu ya kutojua thamani yake wakaamua kumfanya kitoweo.

Blue Marlin Fish ni moja ya aina kubwa za samaki duniani ambao wanapatikana katika bahari ya kitropiki kama Atlantic na Pacific tu, na kwa bara la Afrika wanapatikana zaidi kwenye nchi za Africa Magharibi.

Aidha upatikanaji wao ni wa msimu hasa katika maeneo yenye joto na inasemekana ndani ya miili yao kuna aina ya madini ya Ruby na metali ya Zebaki ambayo matumizi yake ni kwenye mitambo na madawa.

Note: Ng'ombe wa maskini hazai akizaa anazaa dume, na shughuli ya dume tunaielewa.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…