Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza; Mvuvi Nigeria atafuna samaki mwenye thamani ya mabilioni ya shilingi bila kujua

Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza; Mvuvi Nigeria atafuna samaki mwenye thamani ya mabilioni ya shilingi bila kujua

hii habari ilinichekesha sana, nlimuwazia sana mwamba alivopata mawazo lukuki baada ya kupata hizo taarifa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
" Blue Marlin ni moja ya samaki adimu sana duniani na wenye thamani kubwa sana baada ya Bluefin Tuna na White Marlin. Wanapatikana bahari ya Pacific tu, na kabla ya huyu aliyepatikana Nigeria, mwingine alipatikana nchini Nicaragua mwaka 2014.!"

Pacific Ocean inafika Nigeria??????? JF members tuwe tuna heshimiana please.
kwani baharini kuna ukuta mkuu?
 
Mvuvi mmoja katika kijiji cha Warri, jimbo la Niger Delta nchini Nigeria amevua samaki aina ya Blue Marlin mwenye uzito wa 87 kgs na kumchinja kisha kugawana nyama na wanakijiji wenzie.

Baadae kampuni ya Pacific seafood ya nchini Marekani iliposikia habari za kuvuliwa kwa samaki huyo adimu duniani ilitangaza offer ya 30,000$ kwa kila kilo sawa na TZS 69M kwa kilo, ambapo ingelipa jumla ya 2.6 US$ million sawa na Tshs bilioni 6 kwa kilo zote 87. Lakini wakati kampuni hiyo inatangaza offer hiyo tayari samaki huyo alikua ameshaliwa na kuisha.

Frank Dulcich Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Pacific Seafood amesema kitu ambacho mvuvi huyo hakujua ni kwamba wakati anafurahia kutafuna minofu ya samaki huyo, alitafuna pia urithi wa familia yake vizazi na vizazi.

"As he was eating together with his villagers, he didn't know that he has eaten the wealth for his generations to come" amesema Dulcich.!

Blue Marlin ni moja ya samaki adimu sana duniani na wenye thamani kubwa sana baada ya Bluefin Tuna na White Marlin. Wanapatikana bahari ya Pacific tu, na kabla ya huyu aliyepatikana Nigeria, mwingine alipatikana nchini Nicaragua mwaka 2014.!

Umasikini na njaa kama chupi na tako tu
 
kwani baharini kuna ukuta mkuu?
soma kilichoandikwa. wanapatikana bahari ya pacific TU. unadhani samaki nao wanazurura zurura kama wewe?ndo maana kuna samaki huwezi wapata huku TZ ila unawapata sehemu nyingine mbali huko. na hizi ni bahari zenye maji yenye sifa tofauti
 
Unaambiwa usilolijua ni sawa na usiku wa giza na hilo limemtokea mvuvi mmoja huko nchini Nigeria aliyefahamika kwa jina la Zion Godwin ambaye amemvua samaki aina ya 'Blue Marlin Fish' mwenye thamani ya Tsh Bilioni 6 lakini amemla yeye na marafiki zake kijijini.

Taarifa hiyo imesambaa zaidi kwenye mitandao ya kijamii baada ya jamaa huyo kushea picha ambazo zilionesha akiwa ametoka baharini kumvua samaki huyo lakini kwa sababu ya kutojua thamani yake wakaamua kumfanya kitoweo.

Blue Marlin Fish ni moja ya aina kubwa za samaki duniani ambao wanapatikana katika bahari ya kitropiki kama Atlantic na Pacific tu, na kwa bara la Afrika wanapatikana zaidi kwenye nchi za Africa Magharibi.

Aidha upatikanaji wao ni wa msimu hasa katika maeneo yenye joto na inasemekana ndani ya miili yao kuna aina ya madini ya Ruby na metali ya Zebaki ambayo matumizi yake ni kwenye mitambo na madawa.

Note: Ng'ombe wa maskini hazai akizaa anazaa dume, na shughuli ya dume tunaielewa.


FB_IMG_1616595513759.jpg
 
Back
Top Bottom