James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

Usingekuwa na hoja za kitoto hivyo. Kila nikikutana na comment zako juu ya mnada yoyote, nyingi huwa ni mashudu matupu. Kama umekuwa kimwili jaribu kukua kiakili pia.
Acha kuwashwa washwa dogo. Kuna mnada gani tulifanya wewe na mimi?
 
Mama Samia S.H huyo Majaliwa baki nae atakufaa mbeleni, hao waliobaki ni uamuzi wako ila wafikirie kidogo hawa japo wana mapungufu ila wana Unafuu.

1.Jumaa Aweso - Waziri wa Maji

2.Suleiman Jafo - Tamisemi



The rest kula vichwa kadri utakavyoweza
Aisee!

Unataka kumuingiza chaka Mhe. Rais
 
Ajiuzulu fasta kumuachia nafasi Rais wetu mpendwa kuunda serikali aitakayo
 
Mwenyekiti wa NCCR mageuzi Mh James Mbatia amemtaka waziri mkuu ajiuzulu ili Rais aweze kuunda upya baraza lake la mawaziri badala ya kusubiri baraza kuvunjwa.
 
Mheshimiwa Rais wetu Samia suluhu Hassan nakushauri uunde baraza lako jipya la mawaziri kwa maslahi ya watanzania na taifa kwa ujumla wake.

Baraza la sasa limejaa mawaziri mizigo ambao hawawezi kukusaidia wewe binafsi na taifa kwa ujumla.

Wengi wa mawaziri waliopo katika baraza la sasa ni wanafiki ambao kazi yao kubwa ni kusifia na kujipendekeza ili kutetea nafasi zao.

Hata utendaji wao wa kazi hawafanyi kwa maslahi ya taifa na watanzania bali wanafanya kumfurahisha mteuzi maana ndivyo walivyozoezwa na aliyekuwa amewateua.

Mawaziri hawa wenye tabia na silika ya kujipendekeza usitegemee kwamba watakusaidia. Watakachofanya wataanza kusoma na kuratibu mwenendo wako kujua nini unataka, wakishajua wataanza kujipendekeza tena kulinda vyeo vyao kama walivyokuwa wanafanya kwa aliyekuwa mtangulizi wako, hayati magufuli.

Madame President siku zote kuanza upya sio ujinga bali ni mkakati wa kuboresha na kuongeza ufanisi utakaoleta matunda mazuri zaidi.

Nakushauri uvunjilie mbali hilo baraza la mawaziri upange safu yako mpya itakayofanya kazi kwa maslahi ya taifa na sio kulinda vyeo na matumbo yao.
 
Vipi akigoma kulivunja/kulisuka upya?
Asipovunja ategemee kukwamishwa au hata kuchukiwa kama alivyochukiwa mtangulizi wake maana baraza limejaa waganga njaa watupu wanaofikiria zaidi maslahi yao binafsi na sio maslahi ya kulisaidia taifa na watanzania wanao waongoza
 
Hakika mkuu.. ningekuwa mimi ningetoa hadi waziri mkuu ili niwe huru kuunda timu yangu ya ushindi!
Majaliwa kassim atakubali kung'atuka kweli? Maana kwa ile speech yake aliyotoa chato!mmmmh!!
 
Hakika mkuu.. ningekuwa mimi ningetoa hadi waziri mkuu ili niwe huru kuunda timu yangu ya ushindi!
Mnampotosha huyu mama, mnatafutia vita huyu mama CCM ni hile hile na watu ni wale wale au mnataka akalete mawaziri Zanzibar kwao?

yeye ni Vp Hilo balaza la mawaziri wakati linaundwa si alikuepo kwenye huo utawala
 
Wadau wengi wameshauri hili, asipolivunja ataonekana kama hajakamata sawa sawa mamlaka (consolidate power) na anaweza kujikuta anakwama huko mbeleni...
 
Kabisa ili mama aongoze nchi bila kufunikwa na kivuli cha Magufuli, inabidi avunje hilo baraza haraka. Ma hata hao mawaziri hilo wanalijua, lakini wanalazimisha kuwepo ili kumtisha huyo mama asiwaguse. Na kwenye kuunda baraza lake ahakishe Majaliwa, Kabudi, Mwigulu na Jafo wasiwepo. Wale wate waliokuwa wanajipendekeza wazi wazi kwa Magufuli awapige chini haraka maana ndio watamkwamisha. Hao waliokuwa mawaziri wa wizara nyingine, awageuze kuwa manaibu mawaziri.
 
Kumbukeni Mzee majaliwa alihakikisha kuwa anapita bila kupingwa kwenye jimbo lake na hakuna wapinzani waliothubutu kwenda kupiga kampeni jimboni kwake Luwangwa. Huyu anaweza kuwa mbaya sana kwa demokrasia kuliko hata JPM.
naskia skia kuwa jamaa ni mafioso sana😁😁😁
 
Back
Top Bottom