Uchaguzi 2020 James Mbatia: Chama chetu cha NCCR Mageuzi kinakwenda kuwa chama kikuu cha upinzani nchini

Uchaguzi 2020 James Mbatia: Chama chetu cha NCCR Mageuzi kinakwenda kuwa chama kikuu cha upinzani nchini

Ningependa aseme ni njia gani itakayotumika kukifanya NCCR kuwa tena chama kikuu cha upinzani nchini.

Kwasababu kama ni mtaji wa watu naamini hana, na yeye mwenyewe analijua hilo, sasa ningependa awe na ujasiri wa kutuambia hiyo sababu nyingine ni ipi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mtaji wake wengi wameuona....CCM
 
Nina wasiwasi mleta mada umemnukuu vibaya Mwenyekiti. Siamini kama malengo na matamanio ya Mwenyekiti ni kuona chama chake kinakuwa chama kikuu cha upinzani.

Malengo ya chama ni kushinda uchaguzi na kuunda serikali, hii kuwa chama kikuu cha upinzani ni nafasi inayotokea tu baada ya kushindwa uchaguzi kwa kushika nafasi ya pili lakini hilo halijawahi kuwa lengo la chama.

Hivyo nina wasiwasi Mwenyekiti amenukuliwa vibaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UKAWA sasa = na UKIWA

Sasa Kwa mwaka huu kuna watu watajajuta Kwa kuwa washabiki wa Vyama kulikopindukia, kama wengine hatujawabeba machela Kwa vipigo vya wananchi wenye hasira Kali kwa kuwanyima Kura!!!

Yetu macho
 
Kwa hiyo ndoto yake ni kuwa tu chama kikuu cha upinzani......
 
Shida ni kuwa chama kikuu au kuwa kweli chama cha upinzani?? Hata mkipata wabunge 6 tu si tiyari mtakuwa chama kikuu cha upinzani?? Je, na kule visiwani mna mvuto au mtafanya kolabo??

Mbona hii Matrix ni rahisi mno, Kura za upinzani Unguja watagawana CUF & ACT then CCM watashinda, Pemba ACT watashinda, Bara Chadema hawezi kupata majimbo zaidi ya 2 kwa sababu wagombea wazuri wote wameshasepa kwenda CCM & NCCR Mageuzi so finally mwenye uwezo wa kupata kura nyingi Bara za upinzani atakuwa NCCR Mageuzi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ningependa aseme ni njia gani itakayotumika kukifanya NCCR kuwa tena chama kikuu cha upinzani nchini.

Kwasababu kama ni mtaji wa watu naamini hana, na yeye mwenyewe analijua hilo, sasa ningependa awe na ujasiri wa kutuambia hiyo sababu nyingine ni ipi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hilo swali lako jibu ni jepesi sana, wabunge siku hizi hawachaguliwi na wananchi bali Magufuli. Kumbuka alipoenda ikulu alihakikishiwa kupewa wabunge 20 wa bure!!! can you imagine?

Juzi spika kwa kiburi akasema Mbowe harudi! unajua ni kwa nini? washapanga nani arudi na nani asirudi kwa kuwa si haki ya wananchi tena kuchagua. Jeshi la polisi litahakikisha ushindi wa mezani unapatikana wether you like it or not.
 
UKAWA sasa = na UKIWA

Sasa Kwa mwaka huu kuna watu watajajuta Kwa kuwa washabiki wa Vyama kulikopindukia, kama wengine hatujawabeba machela Kwa vipigo vya wananchi wenye hasira Kali kwa kuwanyima Kura!!!

Yetu macho
Usiwasingizie wananchi katika dhambi zenu.
Tumeshuhudia uvunjwaji wa makusudi wa Sheria na Katiba ya nchi, uonezi na uminywaji wa haki kwa zaidi ya miaka minne.

Yote mnayoshirikiana kupanga gizani na SHETANI wenu yatakuja kwama vibaya vilevile kama ya wenzenu walioota na kujivunia kujenga mnara wa Babeli.

Nakuombea uje kuwa hai na kushuhudia nguvu ya Mungu wa haki itakavyo ufikisha mwisho ulaghai na ukandamizaji wenu, mnaojivunia kwa sasa. AMEN
 
Mama Tanzania ana shidaa sana.!!
Labda wapewe ubunge wa viti maalumu.
 
Ningependa aseme ni njia gani itakayotumika kukifanya NCCR kuwa tena chama kikuu cha upinzani nchini.

Kwasababu kama ni mtaji wa watu naamini hana, na yeye mwenyewe analijua hilo, sasa ningependa awe na ujasiri wa kutuambia hiyo sababu nyingine ni ipi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Huko mara kakusanya wanachama zaidi ya elfu 30 bado tu huamini?
 
Back
Top Bottom