Uchaguzi 2020 James Mbatia: Chama chetu cha NCCR Mageuzi kinakwenda kuwa chama kikuu cha upinzani nchini

Uchaguzi 2020 James Mbatia: Chama chetu cha NCCR Mageuzi kinakwenda kuwa chama kikuu cha upinzani nchini

Huyu naye bule kabisa, kwanini asiseme NCCR ni chama kinachoenda kuchukua Dola kwenye uchaguzi ujao. Kwa maneno yake haya inadhihilisha kuwa tayari kuna makubaliano kati ya NCCR na chama kingine kitakachochukua dola

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yuko sahihi maana yeye anawaza kuwa mpinzani,wenzake wanataka kuongoza nchi ila kwa mtazamo huu kwa wale waelewa hawezi kupata chochote maana ana mawazo mgando ya kuwa chama kile milele kitaendelea kuongoza nchi jambo ambalo si kweli, maana Mungu pekee tu ndiye atakaye tawala milele hakuna zaidi yake.
 
Haya ndio mapandikizi yanayojionyesha wazi, why asiseme kiankwenda kuchukua Dola?
Kwa hiyo yeye ana fight kuchukua nafasi ya CDM na sio CCM?
 
Chama kikuu cha upinzani sponsored by chama tawala... 😀

Bongo nyoso..

Everyday is Saturday.................... 😎
 
Kwa akili hizi za mbatia basi CCM watatawala milele.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilidhani angesema chama chake kitashika nchi kumbe anachopigania ni kushindwa na kuwa chama kikuu cha upinzani? What a backward mind?

Kweli Mbatia ni hohe hahe kama Mrema. Anajipendekeza kwa Magufuli ili kura za CHADEMA ziibwe apewe yeye na kuwa KUB
 
Ndo kwanza ninaskia chama cha upinzani chenye malengo ya kuwa tena chama cha upinzani.
 
Musoma uko watu wanaamia NCCR mamia kwa mamia.
Mbeya ni mafuriko.
Mwanza ndo usiseme.
Mikoa ya kaskazini mashariki ndo home sasa kwa NCCR ni nyomi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbatia usidanganye watu hapa. tulio karibu nawe tunakujua sana linapokuja suala la maslahi binafsi. hujaanza leo wala juzi.

NCCR siyo chama cha upinzani...ni tawi letu CCM.
 
Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi Mheshimiwa Sana James Mbatia amesema chama chake kinakwenda kuchukua nafasi yake na kuwa chama kikuu cha upinzani nchini. Mbatia amesema baada ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Tanzania mwaka 1995 NCCR Mageuzi kilikuwa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Mbatia amesema kuwa chama chake kimefanya utafiti na kugundua sababu zilizokifanya chama chake kuwa na wabunge wachache.

Chama cha NCCR- Mageuzi kinaelekea kurudi kwenye nafasi yake ya kuwa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, kama ilivyokuwa baada ya uchaguzi mkuu wa kwanza ndani ya mfumo vwa vyama vingi uliofanyika mwaka 1995" James Mabatia, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa

Hapo vipi? Akili bado kuwarudia?
 
Hawara ya ccm
 
Back
Top Bottom