James Rugemalira aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka

James Rugemalira aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Leo nimepita maeneo ya Mahakama ya Kisutu, Nikakuta Mkurugenzi wa kampuni ya VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira anatabasamu akiwa na ndugu zake wakipeana hugs na kuchumiana. Inaashilia kuna dalili nzuri leo Mzee wa Henken akaliona jua. Langu Dua.

_MG_0435.JPG
James Rugemalila(Kulia) na mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Harbinder Seth Sigh(Kushoto), wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi kabla ya kupanda kizimbani Mahakamani Kisutu Jijini Dar.

Tarehe 19 Jun, 2017 TAKUKURU wawafikisha mahakamani Seth Na Rugemalila kwa uhujumi uchumi. walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu wakishtakiwa kwa makosa sita ya uhujumu uchumi, likiwamo la kuisababisha Serikali hasara ya jumla ya takriban Sh358 bilioni.

Wakili wa Serikali, Paul Kadushi aliyataja mashtaka mengine yanayowakabili wawili hao kuwa ni kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na kuisababishia hasara Serikali.

Zaidi Soma:

1). TAKUKURU yawafikisha mahakamani Harbinder Sethi na James Rugemalira kwa kosa la Uhujumu uchumi

UPDATE:

Rugemalila yupo huru!

Mashtaka yake yameondolewa chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwanendo wa Makosa ya Jinai

F88F84A7-A607-45D0-B052-21500CB00B5A.jpeg


2B281E24-987B-49D4-BEEF-3CA376F330D3.jpeg
 
Wamuachie huyu mzee bwana.Hawa ndo Watanzania wanaotakiwa. Sio watu wanajiona wanyonge hadi kwenye nchi yao. Kama yeye asingevuta mpunga ina maana huu mpunga wote ungeenda nje ya nchi. Chuki tu za watu
 
Mimi nimemkubali, mzee ameona potelea Kwa mbali afie gerezani watoto wabaki na utajiri, hiyo ndio Tafsiri ya Kufa kiume
vijana tijifunze kupata hela ni jambo moja na kuilinda ni jambo jingine linahitaji uwe kauzu na roho ngumu
 
Huyu jamaa anastahili kuwa tajili, ana roho ngumu na kauzu kisawasawa.

Yule marehemu dhulumati kamchimba mikwara yote mzee kakaza bora afie jela kuliko kutishwa na mwehu.
Ndio nimejifunza kuacha mafisadi wafisadi mpaka kiwango cha 5G, kumbe tunapenda kupigwa kiasi hiki! Aliyenacho ataongezewa mara dufu hata kwa kuiba.
 
Back
Top Bottom