James Rugemalira aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka

James Rugemalira aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka

Huyu jamaa anastahili kuwa tajili, ana roho ngumu na kauzu kisawasawa.

Yule marehemu dhulumati kamchimba mikwara yote mzee kakaza bora afie jela kuliko kutishwa na mwehu.
Mwisho wa siku kaenda yeye
 
Mfanyabiashara James Rugemalira ameachiwa huru leo.



NOTE
MAHAKAMA NDIO ILITAKIWA ITOE UAMUZI MAPEMA KWAMBA HUYU MZEE HANA HATIA. NA SIO KUTOKA KWA KAULI YA RAIS. KWA KAULI YA MAREHEMU MAGUFULI ALIFUNGWA NA KWA KAULI YA RAIS SAMIA KAWA HURU. TANZANIA HAIWEZI KUISHI KWA KAULI ZA MTU ALIYEKO MADARAKANI. TUNAHITAJI KUBORESH MFUMO WETU WA KUTOA HAKI.
 
242024015_4207729819337960_588196995109426720_n.jpg

Muda huu kesi mahakamani, James Rugemalira ameachiwa huru kutokana na kuonekana kesi ina milolongo isiyoeleweka.

Mkurugenzi wa mashtaka DPP amefuta mashtaka ya uhujumu uchumi yaliyokuwa yanamkabili mfanyabiashara James Rugemalila na hivyo kusababisha mahakama kufuta kesi hiyo na kumuachia huru James Rugemalila-ITV
 
View attachment 1940085
Salaam Wakuu,

Leo nimepita maeneo ya Mahakama ya Kisutu, Nikakuta Mkurugenzi wa kampuni ya VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira anatabasamu akiwa na ndugu zake wakipeana hugs na kuchumiana. Inaashilia kuna dalili nzuri leo Mzee wa Henken akaliona jua. Langu Dua.

_MG_0435.JPG

James Rugemalila(Kulia) na mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Harbinder Seth Sigh(Kushoto), wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi kabla ya kupanda kizimbani Mahakamani Kisutu Jijini Dar.

Tarehe 19 Jun, 2017 TAKUKURU wawafikisha mahakamani Seth Na Rugemalila kwa uhujumi uchumi. walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu wakishtakiwa kwa makosa sita ya uhujumu uchumi, likiwamo la kuisababisha Serikali hasara ya jumla ya takriban Sh358 bilioni.

Wakili wa Serikali, Paul Kadushi aliyataja mashtaka mengine yanayowakabili wawili hao kuwa ni kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na kuisababishia hasara Serikali.

Zaidi Soma:

1). TAKUKURU yawafikisha mahakamani Harbinder Sethi na James Rugemalira kwa kosa la Uhujumu uchumi

UPDATE:

Rugemalila yupo huru!

Mashtaka yake yameondolewa chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwanendo wa Makosa ya Jinai

View attachment 1940204

View attachment 1940227
Mungu ni Mkubwa.
Kwa kweli ni aibu kubwa kwa wale waliokuwa nyuma ya uonevu huu.
Mungu atawalipa.
 
Bora wamwache huyo mzee ingawa hawakutakiwa kumuhangaisha miaka yote hiyo, kama ni pesa ya mboga alitoa mgao kwa vigogo kibao....
 
Back
Top Bottom