James Rugemalira aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka

Huyu jamaa anastahili kuwa tajili, ana roho ngumu na kauzu kisawasawa.

Yule marehemu dhulumati kamchimba mikwara yote mzee kakaza bora afie jela kuliko kutishwa na mwehu.
Duh! Mwhehu tena. Hapo upipo uko chini ya ulinzi!!!
 
Mtu kauza kampuni yake, kalipa na Kodi kwa Kayafa, hapo kosa lake nini?
Shida ilikuja pale tulipotaka waliohusika wawajibishwe, nadhani unakumbuka mkutano ule wa bunge ulienda hadi saa 4 usiku, huku mbowe akitahadharisha kuwa tutaenda kuwa failed state.
Baada ya muda kikwete alimuwajibisha mama tibaijuka.
Ikiwa hakukuwa na shida basi tuseme tulikosea kuomba waliohusika na escrow kuwajibishwa, na mama tibaijuka aombwe msamaha kwa kufutwa uwaziri
 
Mimi nimemkubali, mzee ameona potelea Kwa mbali afie gerezani watoto wabaki na utajiri, hiyo ndio Tafsiri ya Kufa kiume
vijana tijifunze kupata hela ni jambo moja na kuilinda ni jambo jingine linahitaji uwe kauzu na roho ngumu
"it takes talent to make money,but it takes brain to keep it"

Rugemealira msimamo Kama che Guevara
 
Kama jamaa yako alikuwa mkweli. Mbona hakuwakamata Simba trust ?!. Yule alikuwa mnafiki tu.

Jamaa yangu gani? Ukweli hauna ujamaa wala kupepesa macho, hata hivyo amejifunza kuwa malipo ni hapa hapa kwa ubaya wake.

Kuna mtu anaitwa Simba Trust? Au sijakuelewa. Kampuni ni watu na washirika wake ni watu.
 
Hii kesi alie loose ni singa singa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ndio alikuwa mlengwa ...
Ruge tatizo lake ni kuchanganya pesa zake safi kuchanganywa na chafu ......

Ni dhahiri kuwa kuna raia wengi wapo nyuma ya nondo kwa mizengwe mama endelea kufungua milango yao.....
 
Kama kweli Mungu amsimamie na wadhalimu wooote waendelee kupatwa na yale ambayo yalimpata mwendazake. Huwezi kuonea watu ukaishi Mungu sio binadamu. Mungu amtetee huyu mzee aendelee kuona watesi wake wanavyopakatika
Kwa nchi hii ilivyo hasa wakati ule wa awamu ya 4, ni vigumu kwangu kuamini kuwa hawa majamaa walibambikiwa kesi. Kapuku kama mimi nawewe kushangilia kuachiwa kwao ni mapema sana, ngoja Lissu aje atupe za ndani ndani. Tumezoea kupigwa na tuendelee kupigwa. Upinzani una ajenda nzuri za kampeni 2025. Na kwa speed hii mgombea yeyote wa CCM akipata 50% aende kwa mganga!

DPP mpya kasimikwa, mwanasheria mkuu mpya kasimikwa leo kesi iliyokuwa ngumu kama chuma inalainishwa kama keki...Mmmmmmmm. Watanzania ndio waliwao.
 
Mawazo finyu sn
 
Akifungwa wew utapata nn!?
 
Huyu ndio mwanaume... Unakufa na siri gerezani. Ukitoka unakula nchiii.... Nimempenda kiukweli.
 
Ukijifunza akili na miemko ya watanzania wala hupati shida.

Yaani unaweza kufanya lolote mpaka kuwaumiza watakuchukia kwa muda mfupi then wanageuka kukuonea huruma yaani.

👉🏾Chukua maisha ya maasai yaani yeye kila mtu ni rafiki, ndivyo ilivyo kwa mtanzania 🤓!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…