Jamhuri msipoandaa Mawakili mkaendelea kubebwa na Majaji na Mahakimu tutaendelea kukodi Mawakili wa kigeni milele

..Maza naye si hakufanya vizuri form 4.

..sidhani kama CCM mnaweza kuwacheka CDM kuhusu suala hilo.
Chadema ndio sera yenu ilikua elimu elimu elimu sisi CCM haikuwa hiyo mliimba elimu tukadhani mwenyekiti Taifa atakuwa Profesa Baregu na katibu Dr Lwaitama kumbe hamna kitu kelele tu za kutapeli watanzania
 
Walikuwa wanamtegemea mkono advocate, siku hizi alipotea, ndo maana mkulima wa nabari na wale wakandarasi wa bagamoyo walipiga hela ya kufa mtu baada ya kushikilia ndege
 
Usiwaamshe waliolala mwisho utalala wewe, msemo wa wahenga, matokeo ya kayumba, kata na elimu bure.
Sasa hivi wanajisifia vituo vya afya vya tozo ambavyo vinafanywa very local and un proffesionaly, no consultant no contractors, hi nchi proffesion zimekufa
 
Hiyo ikiuwa Sera ya Chadema lakini hadi leo Mwenyekiti Mbowe ni division zero form Six na katibu mkuu ni Mnyika form four

Hiyo elimu elimu elimu sijui walikua wakimwambia nani
Winston Churchill, nina mashaka sana kwa ulivyo hivyo kama unaweza hata ukamfahamu, alikuwa na elimu gani na kwa nini hadi leo hii ndio amekuwa the best performing PM in UK history.

Unashindwa hata kuelewa kwamba elimu na kipawa cha uongozi ni vitu viwili tofauti. Haya mnasema Magufuli alikuwa na PhD, sasa kama ni kweli ilikuwa ni ya halali ilimsaidiaje kwenye utawala wake wa kiimla?

Huyu rais wa sasa unafahamu Educational Background yake vizuri. Tatizo mkishawekwa humu kuponda wale wapinzani wa ccm basi hamtumii kabisa akili ktk kuhalalisha hizo "Wages" mnazolipwa kwa kuandika umbeya humu. Very hopeless.
 
..muulize Maza kama alifaulu, halafu urudi tujadili matokeo ya Mbowe.

Cc tindo
.
Narudia sera ya CCM sio elimu kama nyie wenye hiyo sera ndio mujibu kwa nini mwenyekiti wenu Chadema Taifa ni division zero form Six?
 
Sina shida na Winston Churchill au yeyote nauliza nyie Chadema wenye sera ya Elimu elimu elimu kwa nini mwenyekiti wa Chadema Taifa ni division zero secondary?
 
lugha kuu ya Mahakama ndio ipi hiyo?
inamaana hadi leo hii Lugha yetu ya Kiswahili haina Maana mbele ya Mahakama zetu za Tanzania?!
Pamoja na sheria kupitishwa na Bunge!!
Waziri wa Katiba na Sheria Prof: Kabudi yuko.wapi kuhakikisha kiswahili kinatumiwa na Mahakama.
Sisi Watanzania tutaelewaje hiyo inayo daiwa kuwa lugha kuu ya Mahakama?!!
Yaani kwa hali hii natamani Magufuli afufuke, inamaana Magufuli alivyo kuwa anasisitiza Kiswahili kitumike hawa viongozi walikuwa wanamkejeli tu!?
wakati akiwa hai sheria ilipitishwa haraka bila kuchelewa, leo hii nini kikubwa hicho kinacho chelewesha Mahakama kutokutumia Lugha ya Kiswahili?!
hizi Mahakama kweli zinawatumikia watanzania au zinawatumikia wazungu?
 
Hakuna wakili competate anaweza kukubali kufanya kazi serikalini..reference nzuri ni huyo kibatala na Lisu sidhani kama wamewahi kuajiriwa serikalini kama mawakili.
 
Kwa taarifa yako uwezo huo mdogo unaouona kutoka mawakili wa serikali ni karibia watendaji wote wa serikali wako hivyo. Rejea alichokisema Prof Assad. Tazama uwezo wa viongozi wetu na watendaji wa serikali, ndio maana unaona matumizi makubwa ya nguvu, maana ni watu wasio na uwezo, na ili waweze kuficha udhaifu wao, inabidi watumie nguvu kubwa. Nadhani umeona hata taarifa ya jana ya DCI kuhusu kijana Hamza, unajua kabisa tuna vyombo vya dola vyenye uwezo duni mno wa kutenda mambo.
 

Magufuli alikuwa hajui kiingereza ndio maana akawa analazimisha kiswahili ili kuficha udhaifu wake. Hao waliopitisha hiyo sheria sio kwakuwa walikuwa wanaamini atakacho, bali walikuwa wanamuogopa kutokana na ulevi wake wa madaraka.
 
Magufuli alikuwa hajui kiingereza ndio maana akawa analazimisha kiswahili ili kuficha udhaifu wake. Hao waliopitisha hiyo sheria sio kwakuwa walikuwa wanaamini atakacho, bali walikuwa wanamuogopa kutokana na ulevi wake wa madaraka.
sasa sisi wananchi tusio jua kizungu hatutakiwi kudai haki mahakamani?!
Mbona kama Mahakama zetu zinatubagua?!
kwa hiyo kiingereza ndio Lugha inayo takiwa na Mahakama?
kwani hao majaji kweli ni watanzania ambao wanataka watanzania wapate haki yao?
Mbona SADC wamepitisha matumizi ya lugha ya kiswahili ktk shughuli zake zote pamoja na kumbukumbu? vipi mahakama zetu zigome kutumia kiswahili ktk kumbukumbu zake?
naomba nisaidiwe
 
Mkuu, ongea taratibu. Unamjua aliyeipenda hiyo hoja ya kiswahili kitumike kwenye mahakama zetu? Hata kama is no more, lakini linda Legacy yake.
 
Kwa kawaida mawakili wa serikali siyo lazima wa pass bar exams. Huwa wanakuwa excempted na wanakuwa registered conditionally ili waweze kupractice.
 
Lugha ya mahakama ni kiswahili na kiingereza.
Mawakili kupendelea kutumia kiingereza hawajalazimishwa, ni mazoea ya kitaaluma.
Pia mwananchi wa kawaida anaweza kutumia lugha ya kiswahili anapodai haki yake mahakamani
 
Mawakili wa serikali wanategemea jeshi la polisi na maagizo kutoka juu kushinda kesi.
 

Waulize kawawa au msekwa alikuwa elimu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…