Kila taaluma (profession) ina masharti na miongozo yake ya kiufundi. Kwa mfano, sekta ya usafiri wa anga/ndege imekubaliana kuwa lugha ya sekta ni kiingereza. Hivyo, dunia yote marubani, wafanyakazi ndani ya ndege (crews), waongoza ndege (atc), n.k. wote lazima wawe na uwezo wa kuwasiliana kwa kiingereza fluently. Hii ni kwa sababu ya kuhakikisha usalama (safety of navigation/flight safety).
Sheria zetu zimedadavuliwa kikamilifu kwa kiingereza na wanasheria wetu ikiwa ni pamoja na mahakimu wanasomea taaluma hiyo kwa kiingereza. Peleka madai yako kwa Kiswahili wao watayachakata kwa kiingereza na kukupa mrejesho kwa kiswahili.
Tuache ujinga. Ndio maana majirani zetu wa Kenya wamekamata fursa kibao kimataifa hata za kufundisha kiswahili chao (kibovu) kwa vile tu wamejiendeleza kwenye lugha nyingine: kiingereza, kifaransa, kijerumani, n.k. Sisi tumeshikilia Kiswahili TU. Utamfundisha nani Kiswahili namna hiyo?