Jamhuri msipoandaa Mawakili mkaendelea kubebwa na Majaji na Mahakimu tutaendelea kukodi Mawakili wa kigeni milele

Hee wanatetemeka tena,na lugha hawajui.. Serikali kiujumla watu wengi ni incompetent Wala sio uongo imagine wanakosea hadi kuandaa hati za mashitaka.
 

Kila taaluma (profession) ina masharti na miongozo yake ya kiufundi. Kwa mfano, sekta ya usafiri wa anga/ndege imekubaliana kuwa lugha ya sekta ni kiingereza. Hivyo, dunia yote marubani, wafanyakazi ndani ya ndege (crews), waongoza ndege (atc), n.k. wote lazima wawe na uwezo wa kuwasiliana kwa kiingereza fluently. Hii ni kwa sababu ya kuhakikisha usalama (safety of navigation/flight safety).

Sheria zetu zimedadavuliwa kikamilifu kwa kiingereza na wanasheria wetu ikiwa ni pamoja na mahakimu wanasomea taaluma hiyo kwa kiingereza. Peleka madai yako kwa Kiswahili wao watayachakata kwa kiingereza na kukupa mrejesho kwa kiswahili.

Tuache ujinga. Ndio maana majirani zetu wa Kenya wamekamata fursa kibao kimataifa hata za kufundisha kiswahili chao (kibovu) kwa vile tu wamejiendeleza kwenye lugha nyingine: kiingereza, kifaransa, kijerumani, n.k. Sisi tumeshikilia Kiswahili TU. Utamfundisha nani Kiswahili namna hiyo?
 
Kutetea uongo nikazi
 
Fungua hiyo smartphone yako kisha iweke kwa kiswahili kisha uone ilivyo ngumu kuitumia, hapo ndio utajua hujui. Huko SADC wamepitisha kiswahili kama fashion, lakini hakuna mtu ana muda nayo. Kiswahili ni lugha ya kupigia Majungu na ushirikina, sio zaidi ya hapo.
 
Narudia sera ya CCM sio elimu kama nyie wenye hiyo sera ndio mujibu kwa nini mwenyekiti wenu Chadema Taifa ni division zero form Six?
Ebu tuwekee na CV ya dikteta Samia.
 
Mawakili mna waonea bure tu. Polisi wamebumba kesi, wao wanapelekewa waende nayo mahakamani, unategemea waseme nini?
 
Sina shida na Winston Churchill au yeyote nauliza nyie Chadema wenye sera ya Elimu elimu elimu kwa nini mwenyekiti wa Chadema Taifa ni division zero secondary?
Ndiyo sababu tunataka ajiendeleze zaidi. Na msisitizo utakuwa elimu elimu elimu
 
Heti wakili wa serili anamwambi jaji, nisamehe pale nimesahahu, so unakuja mahakani fanya nini, Kama hujajiandaa mpaka utegemee msaada wa jaji pumbavu kabisa
 
Ungekuwa na akili timamu ungeishauri serikali ya CCM kutenga bajeti ya kutosha kuhakikisha vitabu vyote vya sheria vinatafsiriwa kwa kiswahili. Sasa serikali ya kidikteta inapitisha sheria ili kuwafurahisha akina Msukuma na Kibajaji bila ya kutenga fedha za kuwezesha sheria kufanya kazi!

Ujinga mtupu!
 
Naomba itokee wakati nikiwa hai bado...
..Siku ikitokea ndege ya Marekani imezuiliwa hapa nchini, Attorney General wa Marekani atalazimika kukodi mawakili wa Kitanzania wakasimamie kesi ktk mahakama za hapa kwetu.
 
Hapa hakuna ubishi. Alikiri mwenywe kwenye clip! Tatizo la Tanzania wenye akili hawana hamu ya kuongoza nchi. Nchi tumewaachia failures. Kama mtu alishindwa fomu 4, anaongozaje nchi lakini?
..Maza naye si hakufanya vizuri form 4.
 
Hapa hakuna ubishi. Alikiri mwenywe kwenye clip! Tatizo la Tanzania wenye akili hawana hamu ya kuongoza nchi. Nchi tumewaachia failures. Kama mtu alishindwa fomu 4, anaongozaje nchi lakini?

..kwa hapa Tz viwango vya taaluma na ufundishaji ktk mashule yetu sio vya kuaminika.

..wakati mwingine wanafunzi wanaanguka siyo kwasababu hawana uwezo, bali kutokana na mazingira yenyewe ya shule.

..mimi namfahamu Mtanzania mmoja alifaulu form 4, akapata zero form 6, akaenda kusomea uganga usaidizi, baadae Muhimbili Medicine, na sasa hivi ana PhD.
 
Na mimi namfahamu mmoja wa aina hii. Tofauti ni kuwa hana PhD.
..mimi namfahamu Mtanzania mmoja alifaulu form 4, akapata zero form 6, akaenda kusomea uganga usaidizi, baadae Muhimbili Medicine, na sasa hivi ana PhD.
 
Lazima wameze ulimi,serikali ya ccm imejaa vilaza ....mpka bungeni
 
Sa mbona kesi nying serikali hua inaangukia nose👃??
 
Ngoja aje cc YEHODAYA hapend kusikisia habar kama hii 🤣🤣
 
Magufuli alikua hapendi kimombo kwa sababu hakijui.
 
Nimepitia maelezo ya Mawakili wa Jamhuri na maelezo ya Mawakili wa utetezi binafsi naona Mawakili wa Jamhuri wajipange vizuri. Wajiandae, wasome sheria kwa undani, wapitie references kuhusiana na kesi. Kuna maelezo mengine ingawaje mimi siyo Mwanasheria lakini dhahiri unaona wanachoeleza kuna kasoro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…