ichumu lya
JF-Expert Member
- Aug 11, 2016
- 2,651
- 2,790
Mbona mnamruka aliyewakamata? Walikamatwa na Kikwete sio Magu.Kwa hio mama Samia anafurahia kuona mashehe wake wanaendelea kusota lupango.
Aaaa nilisahau yeye na meko ni mwili mmoja
haki ni haki iwe kwa yeyote.Me zamani nilikuwa ninadhani kuwa kupata haki mahakamani ni kule kuachiwa huru, nilikuwa najidanganya.
Kumbe hata kupatikana na hatia na kufungwa ni haki pia!
subra ni ngumu lakini ina malipo makubwa sana, wenye kusubiri wapo pamoja na Mwenyezi MunguMwaka wa 9 huu sheikh.....
Kwanini wasifungwe? Hivi kwanini wakae mahabusu bila sababu ya msingi? Mahakama iwahukumu kwa makosa yao sio kuwaweka watakaa miaka mingapi? MahabusuKama kweli walifanya vitendo ya kigaidi wanastahili vifungo kwa mujibu wa sheria.
Ogopa ugaidi ni hatari ,just imagine WTC ilivyoshuka na kuua watu 3000+ ,kama kweli walifanya vitendo vya ugaidi waendelee kusota tu mahabusu ila kama si kweli watatoka tu maana ushahidi utakuwa hakuna.
kuna mzee mmoja kaishi USA miaka 21...na kipindi tukio la 9/11 alikuwepo kule anakwambia lile tukio limetabiriwa kutokea toka zamani sana sio eti ni ugaidi kama tunavyo karirishwa huku,ile ni mipango ya wazungu kuuhadaa ulimwengu tu.2021 bado unaamini WTC ni shambulia la kigaidi? Like seriously???
kwa nini wasihukumiwe kufungwa hata maisha kuliko kuwekwa mahabusu miaka 9,hauoni kama kuna walakini mkuu?Uwaheshimu Wauaji wasio na Utu wenyewe?
Hahaha, hizi akili hizikuna mzee mmoja kaishi USA miaka 21...na kipindi tukio la 9/11 alikuwepo kule anakwambia lile tukio limetabiriwa kutokea toka zamani sana sio eti ni ugaidi kama tunavyo karirishwa huku,ile ni mipango ya wazungu kuuhadaa ulimwengu tu.
Heee!!kwa hiyo wasingeshangilia serikali isingekata rufaa?!!daaa, mawazo mufuWana wamekata Rufaa
Na nyie mlizidi...mlishangilia ushindi wa yale mashitaka yaliyotolewa mapema.....
Angalia sasa wanakatia rufaa ngoma ianze upyaa....
Wewe utakuwa namatatizo ya akili,mwendazake kawakuta hao mashehe walishakamatwa siku nyingi,leo unamsingizia kitu ambacho yeye amemkuta ?,kwa kweli upumbavu ni mzigoHiyo ni danganya toto tu ili isionekane mwendazake alikuwa na mkono.
Mbona hiyo case ishakwisha tangu ujasiri wa kukiri mapungufu Mar 17 ulipopatikana?
Ni suala la muda tu.
Kabla ya mashekh kukamatwa kulikuwa na vitendo vya uhalifu kama mapadri kumwagiwa tindikali na makanisa kuchomwa moto. Ila walipokamatwa mpaka leo hii ni amani, hakuna padri au kiongozi yoyote kamwagiwa tindikali na makanisa hayajachomwa moto mpaka leo.
Kinachoogopesha zaidi, hawa watu wakiachiwa huru huenda kitaibuka kikundi cha Islamic State km Msumbiji, Nigeria na Somalia .
Kwani babu seya nae ndie aliyemkamata?Kwani ndio aliwakamata?
Bismillahir Rahmaanir Rahiim
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA
LEO TAREHE 28.04.2021, SERIKALI IMEKATA RUFAA MAHAKAMA YA RUFAANI DHIDI YA MASHEIKH
Tarehe 23.04.2021, Mahakama Kuu ilitoa hukumu ya ushindi kwa Masheikh wa kesi 14, Kati ya 25, zilizokuwa zinawakabili Masheikh.
Baada ya uamuzi huo shauri lilipangwa liendelea leo kwa kusikilizwa kesi 11, zilizobaki.
Katika hali ya kuonesha nia ya Serikali ya kuendelea na msimamo wake dhidi ya Masheikh hao leo hawakufika Mahakamani kama ilivuotarajiwa na badala yake wametuma hati ya kukata rufaa dhidi ya hukumu iliyowapa ushindi wa kesi 14, Masheikh.
Kufuati hatua hiyo shauri hilo litasitishwa kuendelea Mahakama Kuu mpaka litakaposajiliwa Mahakama ya Rufani na kukapangiwa Majaji wa kusikiliza na hatimaye kutolewa uamuzi.
Wito wa Shura ya Maimamu Tanzania kwa wananchi ni ule ule wa kuwa karibu na kesi hizi kubwa ili kuona na kupata fursa ya kutafakari mgumo wetu wa sheria, uongozi na mustakbali wa Taifa letu .
Ibrahim Z. Mkondo
Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania.
0713118812
Sina chuki nao ila nachukia vitendo vyao. Wakiwa wengi tu wanapitisha sharia zao. Ushawahi kuhudhuria kwenye mahubiri ya kiislam ya mijadala? Wameweka mjadala kabisa kuhusu uchambuzi wa Biblia na Quran.Ila wee jamaa unawachukia sana waislamu, mada kama hizi huwa hukosekani na kutoa maneno makali. Mungu akuongoze
Kwanini wasifungwe? Hivi kwanini wakae mahabusu bila sababu ya msingi? Mahakama iwahukumu kwa makosa yao sio kuwaweka watakaa miaka mingapi? Mahabusu
Sheria za Tanzania zina walakini mwingi. Anza kupambania sheria kwanza, maana raia wengine ni zaidi ya miaka 15 bado hukumu zao hajizotoka.kwa nini wasihukumiwe kufungwa hata maisha kuliko kuwekwa mahabusu miaka 9,hauoni kama kuna walakini mkuu?