Jamii na mtazamo hasi kuhusu kuoa/kuolewa

Jamii na mtazamo hasi kuhusu kuoa/kuolewa

Ningependa kuwakaribisha wadau wote wa Jamii Forums mtakaopendezwa kushiriki katika huu mjadala wenye maswali/changamoto kadhaa zenye kuhitaji majawabu kutoka kwenu.

Awali ya yote ningependa kufahamu haya kuhusu mtazamo wa jamii kuhusu kuoa au kuolewa kwa vijana wa kuanzia miaka 30 mpaka 40 na kuendelea:

1. Kwanini jamii inajenga tafsiri mbaya kwa vijana wa kiume na wa kike wenye umri kuanzia miaka 30 mpaka 40 na kuendelea ambao hawajaoa ua kuolewa, mfano wa tafasiri hizo ni malaya, mzinzi, mhuni n.k?

2. Kwanini jamii huamini kijana mwenye umri huo lazima awe ameoa au kuolewa?

3. Kwanini jamii za hutafsiri ndoa kama kasumba na siyo maamuzi binafsi?

4. Kwanini jamii haijawa tayari kupokea mabadiliko katika jamii inayotambua uwepo wa useja na maseja?

5. Kwanini jamii hutoa shinikizo kubwa kwa vijana wa rika hilo kuwaridhisha wao kuhusu swala zima la kuoa au kuolewa?

6. Kwanini jamii/familia hutafsiri kutokuolewa au kuoa ni kama laana, mkosi au aibu kwa familia?

7. Kwanini jamii hutafsiri vijana wa rika hilo ambao hawaja oa au kuolewa ni kuwa wana chembechembe za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja [ ushoga au usagaji ] au wana mapungufu katika mfumo wao mzima wa uzazi?

Mwisho: Ningependa kufahamu zaidi je, suala zima la kuoa au kuolewa ni suala la maamuzi binafsi ya mwanaume/mwanamke au ni maamuzi ya jamii?

Karibuni nyote kushiriki.
Jamii... ndio nani huyo hadi apangie watu maisha
 
Ishi utakavyo, jamii haiwezi kuja na pingu kukufunga kisa tu hujaoa/olewa. Ilimradi tu usitumie hiyo nafasi ya kutooa/olewa kufanya uzinzi (hata hapa jamii haitokufanya chochote zaidi ya kuongea tu). Besides, siku hizi mambo ya kufuatiliana yamepungua sana, labda kama bado mnaishi kwenye familia zenye mshikamano sana. Watu wanatafuta ugali, hawahangaiki sana na status zetu za mahusiano
Asante ndugu kwa mchango wako.
 
Kuoa au kuolewa ni maamuzi binafsi ikizingatiwa hata ukilala njaa, ukakosa kodi ya nyumba hakuna jamii itakayokuja kukunyanyua. Kikubwa ishi utakavyo na si watakavyo.
Sawa
 
Unaishi kwa kuiridhisha jamii? Poleeeee sanaaaaaa.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Dunia ilishatoka huko. Lol
Sijatoa hitimisho langu hivyo ila nimeuliza kuhusu changamoto ziwa kumbazo vijana wa rika la miaka 30 mpaka 40 na kuendelea kuhusu swala zima la kuoa au kuolewa na mtizamo wa jamii kuhusu hilo swala.

Mchango wako ni upi ndugu ? karibu
 
20221128_060135.jpg
 
Jamii... ndio nani huyo hadi apangie watu maisha
Jamii ni watu watuzungukao katika maisha yetu ya kila siku.

Mchango wako ni upi ndugu kuhusu maswali tajwa hapo juu ?
 
Kila hatua ya makuzi kun jambo unatakiwa ulifanye,Usipo fanya jambo kwa wakati lazima kuna athari itajitokeza.Utaona kuna mtu anafanya mambo hayafanani na umri wake
😂😂😂Ni kweli!! Na ukiruka stage lazima uje kuwa sugar daddy huku uzeeni
 
Kila hatua ya makuzi kun jambo unatakiwa ulifanye,Usipo fanya jambo kwa wakati lazima kuna athari itajitokeza.Utaona kuna mtu anafanya mambo hayafanani na umri wake
Ni athari zipi kijana wa hilo rika ata kumbana nazo asipo oa au olewa ?
 
kwa mimi kabla sijaingia kwenye hiyo inayoitwa ndoa kuna vitu vingi sana nitaangalia kabla yakuchukua maamuzi ya kumfuga mtoto wa mtu hadi kifo. Hii itanichukua muda mrefu sana naamini.
 
Jamii ni watu watuzungukao katika maisha yetu ya kila siku.

Mchango wako ni upi ndugu kuhusu maswali tajwa hapo juu ?
Nadhani ni vema kila mtu afanye lile linalompendeza yeye na nafsi yake bila kujali jamii itasemaje mradi hauvunji sheria za nchi.
 
Tafiti zangu kulingana na mtazamo wa jamii pamoja na familia kiujumla.

Ni hivi inategemea na Maisha yako mi nimeona kwa sana japo Kuna watu wanaonekane wahuni..kwa mfano ukiwa na pesa na msaada mkubwa kwenu watu wa nje wanaweza kukushauri suala la kuoa haraka ila familia mara nyingi hawaga haziwezi kukushinikiza labda wakutafutie mchumba kutoka kwenu jamii zao hii ni ishu ya kimaslahi usije ukawaacha solemba na wakakosa msaada.

Njoo sasa kwa kajamba nane unaweza kufosiwa maana upo upo tu home pesa huna wala hauna msaada umetoka ndevu mpaka za masikio kama paka shume ila Maisha chenga almost umegonga 30 hauna dira wala kazi ya kuelewa...Wanaweza kuforce uoe ila akili ikawe sawa upambane na Maisha hii kitu ndo jamii nyingi zinaaamini ukioa lazima upambane kweli kupata pesa
 
kwa mimi kabla sijaingia kwenye hiyo inayoitwa ndoa kuna vitu vingi sana nitaangalia kabla yakuchukua maamuzi ya kumfuga mtoto wa mtu hadi kifo. Hii itanichukua muda mrefu sana naamini.
Asante kwa mchango wako, kwa nini unahitaji upembuvi akinifu kuhusu hilo swala ?
 
Kwa nini ina tafasirika hivyo na si vinginevyo ?
Kipind icho kama Kijana wa kiume au wakike lazima uwe na ashki za kufanya mapenzi kama haujao ni basi utakuwa unafanya uzinifu au kujichukuliw sheria mikononi(punyeto)...ila ni ile hali ya kujua ni umri upi sahihi ila ukigonga above 30 ni hatar sana kama haujaoa
 
Nadhani ni vema kila mtu afanye lile linalompendeza yeye na nafsi yake bila kujali jamii itasemaje mradi hauvunji sheria za nchi.
Sawa umeeleweka ndugu, ushauri wako ni upi ndugu kwa jamii kuhusu aina ya mitazamo inayo zalisha changamoto nilizo uliza hapo juu ?
 
Back
Top Bottom