Jamii na mtazamo hasi kuhusu kuoa/kuolewa

Jamii na mtazamo hasi kuhusu kuoa/kuolewa

Sawa umeeleweka ndugu, ushauri wako ni upi ndugu kwa jamii kuhusu aina ya mitazamo inayo zalisha changamoto nilizo uliza hapo juu ?
Ushauri ndio huo apo ndugu
 
Ningependa kuwakaribisha wadau wote wa Jamii Forums mtakaopendezwa kushiriki katika huu mjadala wenye maswali/changamoto kadhaa zenye kuhitaji majawabu kutoka kwenu.

Awali ya yote ningependa kufahamu haya kuhusu mtazamo wa jamii kuhusu kuoa au kuolewa kwa vijana wa kuanzia miaka 30 mpaka 40 na kuendelea:

1. Kwanini jamii inajenga tafsiri mbaya kwa vijana wa kiume na wa kike wenye umri kuanzia miaka 30 mpaka 40 na kuendelea ambao hawajaoa ua kuolewa, mfano wa tafasiri hizo ni malaya, mzinzi, mhuni n.k?

2. Kwanini jamii huamini kijana mwenye umri huo lazima awe ameoa au kuolewa?

3. Kwanini jamii za hutafsiri ndoa kama kasumba na siyo maamuzi binafsi?

4. Kwanini jamii haijawa tayari kupokea mabadiliko katika jamii inayotambua uwepo wa useja na maseja?

5. Kwanini jamii hutoa shinikizo kubwa kwa vijana wa rika hilo kuwaridhisha wao kuhusu swala zima la kuoa au kuolewa?

6. Kwanini jamii/familia hutafsiri kutokuolewa au kuoa ni kama laana, mkosi au aibu kwa familia?

7. Kwanini jamii hutafsiri vijana wa rika hilo ambao hawaja oa au kuolewa ni kuwa wana chembechembe za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja [ ushoga au usagaji ] au wana mapungufu katika mfumo wao mzima wa uzazi?

Mwisho: Ningependa kufahamu zaidi je, suala zima la kuoa au kuolewa ni suala la maamuzi binafsi ya mwanaume/mwanamke au ni maamuzi ya jamii?

Karibuni nyote kushiriki.
Hii ilikwenda mbali zaidi mpaka kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa waliambiwa watafute wanawake ili kulinda heshima zao wakiwa kwenye nafasi wanazogombea

Ila kuna mmoja alionekana na taulo anapiga mswaki ofisini asubuhi sijui status yake
 
Asante kwa mchango wako, kwa nini unahitaji upembuvi akinifu kuhusu hilo swala ?
nalazimika kuwa hivi kwasababu, nikichukua watu kumi walio ndani ya ndoa zaid ya nusu yao wanajuta kuwa ndani ya ndoa hizo, robo wanaamua kuficha hisia zao na kuamua kunitia moyo, waliobaki ndio wenye furaha. Hii inanitia mashaka sana. HII NI KUTOKA MAENEO NINAYOISHI NA KUFANYA KAZI.
 
Tafiti zangu kulingana na mtazamo wa jamii pamoja na familia kiujumla.

Ni hivi inategemea na Maisha yako mi nimeona kwa sana japo Kuna watu wanaonekane wahuni..kwa mfano ukiwa na pesa na msaada mkubwa kwenu watu wa nje wanaweza kukushauri suala la kuoa haraka ila familia mara nyingi hawaga haziwezi kukushinikiza labda wakutafutie mchumba kutoka kwenu jamii zao hii ni ishu ya kimaslahi usije ukawaacha solemba na wakakosa msaada.

Njoo sasa kwa kajamba nane unaweza kufosiwa maana upo upo tu home pesa huna wala hauna msaada umetoka ndevu mpaka za masikio kama paka shume ila Maisha chenga almost umegonga 30 hauna dira wala kazi ya kuelewa...Wanaweza kuforce uoe ila akili ikawe sawa upambane na Maisha hii kitu ndo jamii nyingi zinaaamini ukioa lazima upambane kweli kupata pesa
Kwa hiyo jamii zinajenga mtazamo huo kwa kuwa zina amini maisha yanatafutwa pekee kwa mtu kuoa au kuolewa si ndivyo ? Vipi kwa wale vijana wa hilo rika wenye maisha bora lakini hawa chukua uamuzi wa kufunga pingu za maisha na mtu yoyote maana yake wana tafasiriwa tofauti na jamii ?
 
Kipind icho kama Kijana wa kiume au wakike lazima uwe na ashki za kufanya mapenzi kama haujao ni basi utakuwa unafanya uzinifu au kujichukuliw sheria mikononi(punyeto)...ila ni ile hali ya kujua ni umri upi sahihi ila ukigonga above 30 ni hatar sana kama haujaoa
Vipi kwa wale walio chukua uamuzi wa maisha ya kiseja ni kuwa wanatafsiriwa na jamii katika njia isiyo sahihi si ndivyo ?
 
Hii ilikwenda mbali zaidi mpaka kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa waliambiwa watafute wanawake ili kulinda heshima zao wakiwa kwenye nafasi wanazogombea

Ila kuna mmoja alionekana na taulo anapiga mswaki ofisini asubuhi sijui status yake
Maana yake ni kuwa nao viongozi wanapata shinikizo la jamii kuoa/kuolewa ili kuiridhisha jamii ?
 
nalazimika kuwa hivi kwasababu, nikichukua watu kumi walio ndani ya ndoa zaid ya nusu yao wanajuta kuwa ndani ya ndoa hizo, robo wanaamua kuficha hisia zao na kuamua kunitia moyo, waliobaki ndio wenye furaha. Hii inanitia mashaka sana. HII NI KUTOKA MAENEO NINAYOISHI NA KUFANYA KAZI.
Nimekuelewa ndugu.
 
Vipi kwa wale walio chukua uamuzi wa maisha ya kiseja ni kuwa wanatafsiriwa na jamii katika njia isiyo sahihi si ndivyo ?
Ndio wanatafsiriwa tofauti ,ila mbaya ni ile uko age labda ya 30 kama mwanamke ameshazalishwa ni single mother na mwanaume nae kazlisha bila ya kuoa ni balaa.
 
Wenda kuna matatizo mbalimbali yamewakumba hawa vijana wa hilo rika kupelekea wao kuchukua huo uamuzi tofauti na jamii inavyo wa tafasiri.
 
Wenda kuna matatizo mbalimbali yamewakumba hawa vijana wa hilo rika kupelekea wao kuchukua huo uamuzi tofauti na jamii inavyo tafasiri

Ni kutokana na sababu mbalimbali binafsi za msingi alizo nazo kutekelezeka hilo swala.
Kama matatizo gani ukiachana na matatizo ya uzazi, na kama sababu gani? 🥴
 
Swali lilo pale pale, sababu gani hupelekea mtu kuchagua useja mbali na matatizo ya uzazi? 🥴
Useja ni hali ya mtu kuto kuoa au kuolewa, maisha haya watawa huya ishi na baadhi ya watu ndani ya jamii wasio fungamana na maswala ya kidini tofauti na watawa.

Sio kweli kuwa matatizo ya uzazi ndio shinikizo kuu la mtu kuwa mseja, kwa kuwa wapo pia wenye matatizo ya uzazi wake kwa waume walio walio chukua uamuzi wa kufunga pingu za maisha.

Ni hayo tu ninaweza kusema ndugu kuhusu swali lako ndugu.
 
Back
Top Bottom