Jamii na mtazamo hasi kuhusu kuoa/kuolewa

Jamii na mtazamo hasi kuhusu kuoa/kuolewa

Useja ni hali ya mtu kuto kuoa au kuolewa, maisha haya watawa huya ishi na baadhi ya watu ndani ya jamii wasio fungamana na maswala ya kidini tofauti na watawa.

Sio kweli kuwa matatizo ya uzazi ndio shinikizo kuu la mtu kuwa mseja, kwa kuwa wapo pia wenye matatizo ya uzazi wake kwa waume walio walio chukua uamuzi wa kufunga pingu za maisha.

Ni hayo tu ninaweza kusema ndugu kuhusu swali lako ndugu.
Sawa lakini hujajibu swali 🥴
 
Hawa sio vijana tena, hawa ni watu wazima.
Kwani umri wa kijana kwa mujibu wa WHO ni miaka mingapi mpaka mingapi ? Na umri wa mtu mzima ni kuanzia miaka mingapi mpaka mingapi ?
 
Sababu gani hupelekea mtu kuchagua useja? 🥴 Umetoa sababu moja, mtu kuchagua utawa 🥴
Sababu nyingine inaweza kuwa ni mrengwa kuhitaji utulivu zaidi wa kuwa pekee maishani utakao mfanya kukamilisha mipango yake kwa ustadi zaidi tofauti akiwa na mke au mme mfano mwana sayansi na mwana fizikia Nikola Tesla.
 
Wenye miaka 30s na hatujaoa njooni tuongee hapa
 
Nadhani ni vema kila mtu afanye lile linalompendeza yeye na nafsi yake bila kujali jamii itasemaje mradi hauvunji sheria za nchi.
Didiiiiiii hapa umetishaaaa mnoooo. Unataka zawadi gan?
 
Jamii ina paswa kubadili mtazamo wake.
 
Tumekubaliana hakuna kuoa, kauli ya kipumbavu sana. Mtu anakwambia hivyo wakati yeye ana mke na familia yake.

Muhimu za kuambiwa changanya na zako.
Bora umewastukia watu wa Jf. Wengi ni changamsha genge. Wanakuja hapa na mada za ubabe kumbe majumbani wanachofanywa na wake zao utawahurumia na kwenye ndoa wanasugua gaga mwaka wa 10 na zaidi ila humu ni wababe na wanawashauri wenzao wasioe😅

Akili kumkichwa
 
Ningependa kuwakaribisha wadau wote wa Jamii Forums mtakaopendezwa kushiriki katika huu mjadala wenye maswali/changamoto kadhaa zenye kuhitaji majawabu kutoka kwenu.

Awali ya yote ningependa kufahamu haya kuhusu mtazamo wa jamii kuhusu kuoa au kuolewa kwa vijana wa kuanzia miaka 30 mpaka 40 na kuendelea:

1. Kwanini jamii inajenga tafsiri mbaya kwa vijana wa kiume na wa kike wenye umri kuanzia miaka 30 mpaka 40 na kuendelea ambao hawajaoa ua kuolewa, mfano wa tafasiri hizo ni malaya, mzinzi, mhuni n.k?

2. Kwanini jamii huamini kijana mwenye umri huo lazima awe ameoa au kuolewa?

3. Kwanini jamii za hutafsiri ndoa kama kasumba na siyo maamuzi binafsi?

4. Kwanini jamii haijawa tayari kupokea mabadiliko katika jamii inayotambua uwepo wa useja na maseja?

5. Kwanini jamii hutoa shinikizo kubwa kwa vijana wa rika hilo kuwaridhisha wao kuhusu swala zima la kuoa au kuolewa?

6. Kwanini jamii/familia hutafsiri kutokuolewa au kuoa ni kama laana, mkosi au aibu kwa familia?

7. Kwanini jamii hutafsiri vijana wa rika hilo ambao hawaja oa au kuolewa ni kuwa wana chembechembe za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja [ ushoga au usagaji ] au wana mapungufu katika mfumo wao mzima wa uzazi?

Mwisho: Ningependa kufahamu zaidi je, suala zima la kuoa au kuolewa ni suala la maamuzi binafsi ya mwanaume/mwanamke au ni maamuzi ya jamii?

Karibuni nyote kushiriki, pia ningeomba tujikite kwenye maswali tajwa.
Useja na maseja ni nini daah kitu mpya kwangu
 
Back
Top Bottom