Jamii na mtazamo hasi kuhusu kuoa/kuolewa

Jamii na mtazamo hasi kuhusu kuoa/kuolewa

Ningependa kuwakaribisha wadau wote wa Jamii Forums mtakaopendezwa kushiriki katika huu mjadala wenye maswali/changamoto kadhaa zenye kuhitaji majawabu kutoka kwenu.

Awali ya yote ningependa kufahamu haya kuhusu mtazamo wa jamii kuhusu kuoa au kuolewa kwa vijana wa kuanzia miaka 30 mpaka 40 na kuendelea:

1. Kwanini jamii inajenga tafsiri mbaya kwa vijana wa kiume na wa kike wenye umri kuanzia miaka 30 mpaka 40 na kuendelea ambao hawajaoa ua kuolewa, mfano wa tafasiri hizo ni malaya, mzinzi, mhuni n.k?

2. Kwanini jamii huamini kijana mwenye umri huo lazima awe ameoa au kuolewa?

3. Kwanini jamii za hutafsiri ndoa kama kasumba na siyo maamuzi binafsi?

4. Kwanini jamii haijawa tayari kupokea mabadiliko katika jamii inayotambua uwepo wa useja na maseja?

5. Kwanini jamii hutoa shinikizo kubwa kwa vijana wa rika hilo kuwaridhisha wao kuhusu swala zima la kuoa au kuolewa?

6. Kwanini jamii/familia hutafsiri kutokuolewa au kuoa ni kama laana, mkosi au aibu kwa familia?

7. Kwanini jamii hutafsiri vijana wa rika hilo ambao hawaja oa au kuolewa ni kuwa wana chembechembe za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja [ ushoga au usagaji ] au wana mapungufu katika mfumo wao mzima wa uzazi?

Mwisho: Ningependa kufahamu zaidi je, suala zima la kuoa au kuolewa ni suala la maamuzi binafsi ya mwanaume/mwanamke au ni maamuzi ya jamii?

Karibuni nyote kushiriki, pia ningeomba tujikite kwenye maswali tajwa.
Kutokuolewa au kutokuoa husanabishwa na jamii, hivyo nashauri jamii ilitazamie hili na ijisahihishe, mlengwa hausiki na lawama zotezote jamii ijitafakari tu
 
Kitendo cha wao kuwa single mom halafu bado wanatafuta ndoa ndiyo chanzo cha wao kutukanwa
Kisa cha mtu kutukanwa ni nini kwa kutafuta ndoa? Wengine wanatukanwa hata bila kuitafuta hiyo ndoa wanaonekana ni kama kundi la walemavu. Na unakuta hata hao wanaowatukana wamelelewa na wanawake wa design hiyo tena waliokua na tabia mbovu kuliko za hawa wanaotukanwa.

Sidhani kama wao kutafuta ndoa ndo sababu ya kutukanwa unless kama mada huwa huzielewi
 
Kutokuolewa au kutokuoa husanabishwa na jamii, hivyo nashauri jamii ilitazamie hili na ijisahihishe, mlengwa hausiki na lawama zotezote jamii ijitafakari tu
Hakika
 
Back
Top Bottom