Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Katika dunia ya leo, tunashuhudia hali ya kushangaza sana ambapo watu wanaofanya maovu wanaheshimiwa na kutukuzwa, na wakati mwingine kuwa mfano wa kuigwa, watu ambao maisha na mienendo yao sio yenye staha katika maisha ya kawaida. Hali hii inanifanya nijiulize: Kuna jamii ina haki ipi katika kusimamia na maadili?
Mbona tunasherehekea watu waliovunja sheria na maadili, huku tukiwadhihaki na kuwaadhibu wale wanaojitahidi kufanya mema? Mtu akiwa fisadi na tapeli ndo anapata sifa na heshima nyingi, ila msema kweli anapewa adhabu kali.
Ni katika huu Ulimwengu utashuhudia watu wanaoshikilia nafasi kubwa katika jamii zetu kwa sababu ya kutenda maovu, na bado wanaheshimiwa na kutambuliwa kama mashujaa.
Katika jamii yetu, wapo watu wanaojulikana kwa kutenda vitendo vya kikatili, uhalifu au kushirikiana na mifumo mibaya ya utawala. Ingawa tabia zao ni za dhuluma na uharibifu, wengi wao wanapewa heshima na kutangazwa kama mfano bora kwa vijana.
Hii ni hali inayozua maswali kuhusu maadili ya kweli tunayopaswa kuhamasisha kwa watoto na vizazi vijavyo. Mfano mzuri, Kesi ya Ditopile Mzuzuri, je unadhani angekuwa Hamis muuza Mkaa pale Buza, hii kesi ingepewa uzito sawa na Ditopile? Kesi ya Lengai Ole Sabaya na kesi zingine?
Mfano mwingine wa wazi ni watu maarufu kutoka kwenye tasnia ya burudani, siasa na michezo. Baadhi yao wanajulikana kwa kushirikiana na tabia mbaya kama vile kutumia mihadarati, umalaya na wengine wakitukuza sifa za mahab kupitiliza. Lakini, badala ya kuonesha kuwa mwelekeo wao sio sahihi kwa jamii, sisi tunawasherehekea, tunawapa tuzo na nafasi kubwa katika jamii.
Watoto na vijana wanakuwa na picha potofu kuhusu mafanikio, wapo watoto wa kike ambao watakua wakijua maisha ya msanii fulani ndo maisha bora kwake akimaliza tu kidato cha nne. Watakua wakijua kwamba ili kuwa maarufu ama pesa, ni lazima ufanye mambo ya kuvutia hata kama ni kwenda kinyume na maadili ya kijamii.
Vijana wanapojitahidi kutekeleza matendo mema, kama vile kusaidia watu, kufanya kazi kwa bidii au kudumisha maadili ya familia, mara nyingi hawana sifa wala kutambuliwa wala kupewa pongezi.
Hii inawaumiza, kwani wanajua kuwa sio rahisi kujulikana kama mtu mzuri au mwenye maadili, lakini mtu anayeshindwa au kufanya maovu anaweza kupata umaarufu haraka. Hali hii inachangia kuporomoka kwa maadili katika jamii. Kuna mitaa vibaka wanaheshimika zaidi kuliko watu wa kawaida, wanaishi na wananchi kwa hofu kubwa sana.
Ni vema kukumbuka kuwa tunapoadhimisha watu wa aina hii, tunachochea mazingira ya kuvumilia vitendo vya ukatili na uovu, mambo kama unyanyasaji wa kijinsia, kuvunjika na kusambaratika kwa familia. Tunajenga jamii ambayo inavutiwa zaidi na umaarufu wa haraka kuliko mafanikio ya kweli yanayotokana na kufanya matendo mema.
Hii ni hatari kwa maendeleo ya jamii, kwani inaendelea kuchochea mifumo ya kijamii inayozunguka utamaduni wa uhalifu na dhuluma. Kwa sasa ni utamaduni wa kawaida kusikia mwanamke akisema kuwa yeye ni Escort, ili kupunguza ukali wa neno anajiuza.
Nchi yetu inahitaji jamii nzima kushirikiana pamoja ili kubadilisha mtindo huu wa utamaduni wa kuadhimisha maovu, na kusherekea machafu.
Tunahitaji kujenga mifumo itakayowatambua na kuwaenzi wale wanaofanya matendo mema, hata kama hawana umaarufu mkubwa. Ndani ya jamii kuna watu wanafanya mambo mema na yenye msingi na wala hawana muda wa kujionesha.
Watoto wanapaswa kujifunza kwamba kweli mafanikio yako katika kujitolea na kufanya mema, sio kwa kufanya mambo ambayo yanaenda kinyume na sheria na maadili ya jamii.