Kwenye haya mambo ya ufuska na kukosa unyoofu, kutofanya kitu hadharani wakati unakifanya nyuma ya pazia ndiyo fake modesty yenyewe hiyo.
Na maadam wote wanafanya, inawezekana anayefanya hadharani akawa na maadili makubwa zaidi ya anayefanya kwa kificho.
Kwa sababu angalau anayefanya hadharani hafichi, hadanganyi, hajifanyi kuwa msafi wakati ni mchafu, anakuonesha wazi alivyo.
Anayefanya kwa kificho, zaidi ya hayo mabaya anayoyafanya, anafanya baya lingine la kuficha mabaya yake, mumuone msafi, wakati ni mchafu.