JamiiForums na FikraPevu, walaani nguvu inayotumika kuzuia uhuru wa maoni

JamiiForums na FikraPevu, walaani nguvu inayotumika kuzuia uhuru wa maoni

Chipsi yaipembeni

Senior Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
128
Reaction score
92
KAMPUNI ya Jamii Media, ambao ni wamiliki wa mitandao maarufu ya mijadala kwa jamii kupitia mitandao ya jamii,JamiiForums na FikraPevu nchini Tanzania, imelaani kitendo cha baadhi ya kundi/watu walioishambulia miundombinu ya kampuni hiyo na kuzuia kupatikana kwa huduma zake kwa siku kadhaa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo ndg Maxence Melo, tangu katikati ya mwezi Oktoba, 2015 mtandao wao pendwa wa JamiiForums ulianza kupata mashambulizi yaliyojulikana kama "DDOS Attack" mfululizo bila kikomo.

Amesema kwa kawaida yapo madaraja matatu tofauti ya mashambuzili (daraja la 3, la nne na la 7), na hivyo walipambana na mashambulizi kuanzia la daraja la tatu na la nne lakini waliokuwa wanataka kuhujumu miundombinu hiyo waligundua kuwa mashambulizi yao yamedhibitiwa, wakaamua kushambulia hadi daraja la 7 ambalo ndilo kubwa na la mwisho.

Muonekano wa picha unavyoonyesha jinsi miundombinu ya mtando huo ilivyoshambuliwa hadi kufikia Novemba mosi mwaka huu

Aidha, amesema mashambulizi ya DDOS Attack yanalenga kuzuia upatikanaji wa huduma na kufanya tovuti yoyote husuani ya mtandao wa JamiiForums kuzidiwa (kuchelewa kufunguka) na kutoa huduma kwa watumiaji.

''Walipoona tumeweza kudhibiti daraja la nne, walishambulia daraja la saba, sasa makampuni mengi yanayotoa huduma za kusimamia mtandao 'Server Hosting Providers' yanapoona unashambuliwa sana yanakufukuza kwa kuwa wewe unashambuliwa na kuvuruga miundombinu yao'' alieleza Maxence.

Amesema licha ya kampuni nyingi za kutoa huduma ya vihifadhi mtandao (Web Servers) kuogopa daraja la 7, yapo baadhi ya makampuni yanayoweza kukabiliana na hali hiyo.

"Hakuna mtoa huduma ambaye anakubali kuendelea kutoa huduma ya kuendelea kushikilia seva yako kama unaendelea kupata mashambulizi ya aina hii.

Picha hizi zinazoonyesha jinsi miundombinu ya mtando huo ilivyoshambuliwa hadi kufikia Oktoba 31, 2015

Mtandao wa JamiiForums unatajwa kuwa miongoni mwa mitandao ya kijamii inayosimamia uhuru wa habari, kuhabarisha na kushirikisha wananchi kwa habari na matukio katika kila nyanja.

Ni hivi majuzi, JamiiForums imetunukiwa tuzo ya Chombo Huru (Free Media) na taasisi ya Tanzania Media Foundation (TMF) kufuatia utendaji kazi wake unaoonekana kutoa fursa sawa kwa wote.
 
Hangera sana wakuu kwa kushinda Pambano hili
 
Chipsi yaipembeni


Pamoja na taarifa safi kama hii-ilifaa watoe na dokezo la wahusika wa mashambulizi hizi !.Washambuliaji ni wanatoka maeneo moja mbili tatu -mengine wasomaji watajitafakari nia ,wahusika na dhamira!

Poleni na ndiyo hivyo kutoa Elimu na kutafuta Uwazi ni jangaa la kidunia-Wachache wangependa waendelea kufaidi !



 
Last edited by a moderator:
Nadhani kukamatwa kwa vijana wa IT, kuvamia ofisi za LHRC na JF kuwa hacked vina uhusiano kukiwa na lengo la kuzuia jamii kupata taarifa huru kinyume na zile za NEC.

Kwa upande mwingine sioni kwa nini niwape pole maana mlionekana mko upande wa team 'nchi haitolewi kwa karatasi' ndio mjitambue sasa.
 
Mashambulizi mengi ya kimtandao hayaepukiki. Lakin sasa ni wakat muafaka wa kuwa na plan B. Kusema tu unashambuliwa, haitoshi.
 
Ni kweli kabisa na inawezekana walioshambulia wamo humu humu JF.Kijana mmoja a genius(in IT)ambaye alikuwa mmoja wa washambuliaji, alinieleza jana jinsi walivyotumiwa kwa ajili ya ku-rig uchaguzi na kuhujumu JF.Walikuwa wanalipwa take home kwa siku T.sh1,000,000, everything else paid.Ni umafia kabisa,there is no other word you can describe the nature of the action.
Kuna wengine hapa mnatoa pole za kinafiki tu, Wanaoishambulia JF ndio hao hao mnaowatetea kila siku.
 
Nadhani kukamatwa kwa vijana wa IT, kuvamia ofisi za LHRC na JF kuwa hacked vina uhusiano kukiwa na lengo la kuzuia jamii kupata taarifa huru kinyume na zile za NEC.

Kwa upande mwingine sioni kwa nini niwape pole maana mlionekana mko upande wa team 'nchi haitolewi kwa karatasi' ndio mjitambue sasa.
Si kweli. Wale walipokamatwa mashambulizi yalikuwa hayajafikia hiyo hatua...
 
Hapa MWEZI WA KWANZA ROPES anaweza kuwa anahusika kwa kiwango cha juu...
 
mnabahati nyinyi hamkubakwa..
waulizeni UKAWA tallying station.
 
hakika lowasa alikuwa amejiandaa kushika nchi kwa gharama yoyete ili iwe chafu / safi hongera jeshi la police na TISS kwa ujumla
KUKAMATWA VIJANA WA (IT,HAKI ZA BINADAMU NA HILI LA KU ATTACK JF NAAMINI VINAUHUSIANO SANA)...
-TENA NI MKONO WA WENYE NYUMBA HUU MAANA KAMA INGEKUWA KIKUNDI CHA WATU BINAFSI MELLLO ANGEPATA SUPPORT YA WENYE NCHI KUWA TAFUTA POPOTE WALIPO NA WANGEWA WA ITSHA KAMA tallypoling na LHRC ..
BUT ni wao wenyewe wa SUTI sasa!!??
 
Nadhani kukamatwa kwa vijana wa IT, kuvamia ofisi za LHRC na JF kuwa hacked vina uhusiano kukiwa na lengo la kuzuia jamii kupata taarifa huru kinyume na zile za NEC.

Kwa upande mwingine sioni kwa nini niwape pole maana mlionekana mko upande wa team 'nchi haitolewi kwa karatasi' ndio mjitambue sasa.

aisee!! unafanya nini humu mkuu? ebu kuwa mtu mzima

tatizo lako unataka chochote kiandikwe na kupostiwa??

hauko fair

JF hawako biased wala upande wowote na wamethibitisha hilo kwa kuvamiwa

hoja yako haina mashiko, unaonekana uko nyuma ya wakati au hauoni reality
 
Utawala ambao haujiamini,huingilia mifumo ambayo ukweli hujadiliwa ili kuficha uovu wao.Mungu atasimama kwenye Haki.
 
Mbona mnakuwa na hofu ya kumtaja aliyewashambulia wakati anajulikana na aliyemtuma pia?
 
Ni ukweli usiopingika kuwa jamii forum ni mahali mahususi pa kupata taarifa za haraka.

Tunaungana nanyi ktk kuulaani uharamia huo. Kwa kuwa mnajua mnawindwa badilisheni mbinu zenu za kujihami.

Nawatakia kila la heri Jamii forum na watumiaji wote wa mtandao huu.
 
Back
Top Bottom