JamiiForums: Unaweza kuwa VERIFIED, fuata hatua hizi

JamiiForums: Unaweza kuwa VERIFIED, fuata hatua hizi

Poleni sana.

Hakuna aliyewalazimisha. Hao unaoona wako Verified hawakombwa bali waliomba wenyewe.

Sisi tunaitikia hitaji lao kwa kuweka utaratibu rafiki. Tunatambua wapo wengi wasiotaka kuwa verified, nao ni haki yao!

Msitie shaka, unavyoamua kuwa JF ndivyo utavyohudumiwa
Asante sana kwa ufafanuzi.
 
Sasa mkuu hii sikama ile ya chanjo tuu ,itafikia pahala lazma uwe verified,sijapenda bora iyo tick wawekewe waliochanjwa
 
Poleni sana.

Hakuna aliyewalazimisha. Hao unaoona wako Verified hawakombwa bali waliomba wenyewe.

Sisi tunaitikia hitaji lao kwa kuweka utaratibu rafiki. Tunatambua wapo wengi wasiotaka kuwa verified, nao ni haki yao!

Msitie shaka, unavyoamua kuwa JF ndivyo utavyohudumiwa
Ni kama chanjo ya Corona au sio?.
 
Wakuu Verification Badge inaonekana kwangu? 😀
-
Maxence Melo hili ni wazo zuri sana, if don't mind the team inaweza kufanyia kazi ya kupunguza ukubwa wa badge na kuisogeza 2 space bars kuonekana kwa mbele kidogo ya herufi ya mwisho ya mhusika?

Thanks
 
Naam, badili jina mwenyewe kupitia hii link: https://www.jamiiforums.com/account/account-details
Mkuu Maxence nimeona hapo watu nwanahitajiwa kuweka identification sasa hamuoni kwamba ndio udukuzi wenyewe huu maana privacy ndio habari ya humu ndani ndiomaana hata kwenye ile figisu yako ya vyesi uliamua kutotoa siri hadi ikabidi segerea ihusike lakini ukakomaa, sasa napata tabu sana hapa unataka tena documents za kutambua member
 
Wakuu,

Kumekuwa na maombi kadha wa kadha ya watu kutaka kuwa verified.

Tumeona vema tuweke urahisi wa mtu kuomba kuwa verified badala ya utaratibu wa awali. Kuwa verified kwako ni kwa hiari yako. Unaweza kusoma Sera yetu ya Faragha kama una concerns zozote > Privacy policy ambayo ina ufafanuzi wa kina.

Kwa wanaotaka kuwa verified, utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:

Utabonyeza (ukiwa kwenye web browser) sehemu imeandikwa Account, kisha fuata utaratibu huu:

View attachment 1897917

Utabonyeza "Request Verification Badge". Utaweza kuona sehemu inakuja na eneo la kuweka ujumbe wa kuwasiliana nasi ukiambatanisha na copy ya ID inayothibitisha majina unayotaka yawe verified ni yako

View attachment 1897898

Ukishatuma request, vumilia kidogo kwani itakuwa processed na ikiwa ina changamoto progress itaonekana kwako baada ya sisi kuwasiliana nawe kuhusu ombi lako.

Profile yako au ya mdau mwingine, ukipeleka cursor itaonyesha maandishi haya (mfano):

View attachment 1898044

ILANI:
1) Kwa waliokuwa verified awali, huna ulazima wa kufanya mchakato huu, lakini ikikupendeza kujaribu - UNAKARIBISHWA
2) Unaweza kuwa verified ukiwa na ID yako ya JF (not a real name) endapo tutajiridhisha kuwa ID ni mtu tunayefahamiana naye na maudhui ya akaunti yake hayashushi hadhi ya badge husika; mfano wa waliokuwa verified kwa IDs kawaida ni Bujibuji na Madame B

Wanachama ambao ni VERIFIED wataonekana hapa: Verified Members

Asante
Haina mawaa
 
Hiyo inahitajika upload pande zote au hata mbele tu inatosha Kwa format ya jpd au png
 
Sijafanya process yoyote Ila nipo kwenye expart member, moderate. Nilipojiunga sikujua (out of ignorance) nikatumia jina halisi, kubadilisha jina inakuwaje?
 
Back
Top Bottom