TUSHIRIKISHANE JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"

Hongereni sana Mkuu, Mungu awatangulie katika kazi yenu hii. Mimi na Watanzania wenzangu tunazidi kuwaombea. Mwisho kabisa, Misahau kulifikia jimbo kubwa la Rais Magufuli Yaani Tanzania. Muwaulize Wananchi kama ahadi za Rais Magufuli zimetekelezwa kwa kiasi gani. Kama wananchi inabidi tujue mpango uliopo foreplan kuhusu Tanzania ya Viwanda.

Tunapaswa kujua ahadi za Rais Magufuli zimetekelezwa kiasi gani? Rais hata akiwa busy itabidi atoe maelezo hata kwa maandishi tuyaone.
 
Hongera mkuu Max, na crew mzima ya JF, Mungu awatie nguvu.

Kazi yenu itasaidia kufumbua wananchi kujua majukumu ya viongozi wao.

Maana kuna watu walikuwa wakienda nyumbani kwa wabunge ili kutaka misaada binafsi, kwa kujua nalo ni jukumu la mbunge.
 
Hii safi sana ...

Wazo langu hapa haina haja ya kuongeza wingi... Nyinyi wachache mlioanza muendelee kwanza mpaka matunda yaliyopangwa kufikiwa kwa asilimia za kutosha... Kisha kwenye mchakato mwingine ujao waheshimiwa watajileta wenyewe na hapa hawapiti hadi mchujo kwa wenye nia ya kweli ya maendeleo
 
Safi kabisaaaa! Mabadiliko siyo tunayoyaombea bali tunayojiletea!..
Hongera saana Maxence ingawa hukushirikisha wilaya zingine, polepole ndio mwendo!

Mbunge wetu Jackson Lweikiza kuna miradi ya maji Kata Ibwera kijiji cha Itongo. Kitongoji Bwagula
World Bank funded since 2015 or 2014, hakuna maji na majibu sahihi kwa wananchi hakuna.

Miradi ifuatiliwe phyisical ili kuwa na majibu sahihi.

Ubarikiwe!!
 
ni vizuri na wasiishie na majimbo hayo tu waendelee zaidi
 
Ni mradi mzuri kama hautachangamanishwa na siasa za kuchagua Upande pia mradi ungehusisha na wadau wengine wa maendeleo jimboni mfano wafadhili wa miradi mbalimbali wasio na malengo ya Kisiasa
 
Max mmetoka Bukoba hadi Nzega, mbona hamkupita hapa Rock City.

Hongereni sana kwa ubunifu huu, nauombea mradi udumu na kuleta matunda yaliyokusudiwa
 
Asanteni sana wana JF, hakika hiki ndicho kitu tunachokihitaji na kutegemea, vyombo vya habari vinawajibu wa kuzifikia pande zote, viongozi, wananchi huku wakiwagusa wote katika tofauti zilizopo.

Hii imedhihirisha kuwafikia wananchi ka wingi hata kama mnaongea na wachache wao lakini naamini wanatuwakilisha. Viongozi kuulizwa maswali ana kwa ana na wapigakura wao. HII NI MAENDELEO TOSHA {Atakachokijibu atakitekeleza}

ASANTE SANA JAMII FORUMS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…