Jamvi la Wanawake: Mabinti mmewafanya nini hawa wanaume huu mwaka, mbona wana hasira hivi?

Unaelewa, naelewa…. You are only arguing for the sake of it.

I hope umesoma kichwa cha huu uzi, my first reply ilikuwa kumwambia mleta mada kuwa: Sio kwamba tumewafanyia nini wanaume ndio maana wanatupopoa mawe humu, bali ulimwengu uko hivi kwa mwanamke toka kuumbwa kwako: Maana sio kuhusu tulichofanya recently bali ni muendelezo.
 

Kwamba kwakua wanaume wenzetu mababu zetu wa kale wanasemekana kuwakandamiza bibi zetu basi tukubali tu lawama zenu dhidi yetu kwa niaba ya mababu zetu kwasababu tu sisi ni kizazi chao?
 
Kwamba kwakua wanaume wenzetu mababu zetu wa kale wanasemekana kuwakandamiza bibi zetu basi tukubali tu lawama zenu dhidi yetu kwa niaba ya mababu zetu kwasababu tu sisi ni kizazi chao?
Nani amesema hayo?

Unaelewa nini kuhusu mabadiliko ya kijamii na mapokeo? Unajua kuwa mitaani wanawake wanawakosea wanaume na wanaume wanawakosea wanawake? Sasa mjibu mleta mada kwanini platform kama JF Nyuzi za kuwasema jinsia ya kike ni nyingi kuliko kinyume chake.

I would like to hear from you…. Usilete mtazamo shallow/narrow nimeshapita huko siku nyingi, napenda kujadili mizizi sio matokeo.
 
am not generalize just my experience . Wanawake ni wabinafsi na very complicated unashindwa kujua nini hasa anataka.
generalize ❌
generalizing ✅
Je, wewe ulikua tayari kuhamia mkoa anakofanyia kazi?
Namuambia acha kazi kaa hapa nitakuhudumia amekataa hawezi kua mama wa nyumbani tu . Ok acha kazi nina kiasi hapa naweza nikakufungulia biashara hataki kisingizio ilikua ndoto yake kufanya hiyo kazi.
Kwani ulifikiri wakati mnasoma chuo pamoja, yeye alikua anajifurahisha tu na hayuko interested kufanya kazi kwenye taaluma yake?

Ulishawahi kumuuliza kama anataka kufanya biashara? na kama anataka ni ya aina gani? na je una uwezo nayo?
Yani kama sio yeye alikua anasema my deream ni kua na “ health and happy family “ 😂
Yeye ni binadamu na inawezekana ana ndoto zaidi ya moja. Hiyo haimaanishi "a healthy and happy family" siyo ndoto yake pia.
 
We are now telling men that we have brains, we have platforms, we will talk back and fight back, we won’t endure, we won’t shrink sawa?

Hii mada ilikuwa inahusu hilo.
Na hii ndo sababu ukombozi dhidi ya mwanamke wa kiafrika utachukua muda mrefu kuliko inavyohitajika. Mmekaa kimashindano sana. Yaani mtu unashindana na nobody. Unaweka nguvu mahali ambapo nguvu haihitajiki. Mnafurahisha sana nyie viumbe.
 

Ok. Jibu langu kwa maswali ya mleta mada ni kama ifuatavyo: baadhi ya hoja za wanaosadikika kuwa ni wanaume ambao wameandika kukosoa au kuwakashfu wanawake ni batili kwasababu zinakinzana na uhalisia. Mfano, kusema a woman has nothing to offer to her male partner but a "pussy" siyo tu ni tusi bali pia ni kujidanganya. Mwanamke hata ambaye hana ajira rasmi ambaye anahudumia familia tu bado ana mchango mkubwa sana, sometimes kuliko hata huyo mumewe mwenye ajira. Ajira zenyewe za kibongo nyingi hazilipi vizuri kiasi cha kusema kwamba wewe mwenye ajira una mchango kuliko asiye na ajira. Lakini pia wapo wanawake ambao baadhi ya yanayondikwa hapa jukwaani dhidi ya wanawake yanawaelezea kwa usahihi kabisa.

Back to your original comment. Jibu lako kwa mtoa mada lina uhalisia mdogo sana na haliakisi hicho unachokiita root cause etc. Kusema kwamba wanaume wanaoandika kutukana kukashfu au kudharau women wanasukumwa na hisia za kupoteza power inaweza kuwa kweli, ila ni kwa wanaume wachache sana. Binafsi naamini hata wanaume abusive wengi hawasumbuliwi na inferiority or superiority complex. Chanzo kikuu cha abuse kwa Tz ni mila potofu na kukosa elimu nzuri. Siyo gender ya mwanaume. Wenyewe hao so-called abusers wengi ni wahanga pia wa mila na elimu potoshi. Watu wa hivyo wanabadilishwa kwa empathy, proper education, and time. And, yes, time heals. Huwezi wabadilisha kirahisi kwa kejeli, mipasho, au hata sheria.
 
Kuwa binadamu wa hovyo haijalishi jinsia, kuna wadada wenye tabia zisizofaa, kuna wakaka wenye tabia zisizofaa.

Kwenye mifano mbona kuna wanawake wametulia, wanawatunzia familia kwa uaminifu ila wakaka mnatoka na kwenda kuchepuka na mabaamedi au vibinti vya chuo na wengine wanaleta magonjwa nyumbani au watoto wa nje ya ndoa - humu JF kuna confession nyingi za namna hiyo, na huwa mnacheka tu mnachukulia poa.

kila kundi lina bad apples zao, haimaanishi wote ni wabaya.
 
Thanks for pointing that out, I tried kusahihisha kichwa cha uzi ila mods wakagoma kubadili.

Nilirealize baada ya kupost kwamba nimefanya blame shifting na kuwavika mabinti responsibility ya bad behaviour ya wanaume. Hiyo si sawa na nafikiri ni residue ya internalised misogyn ambayo wengi wetu tunaibeba subconsciously na sometimes ina-slip up kutukumbusha bado tuna safari ndefu ya ku-unlearn.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…