Jamvi la Wanawake: Mabinti mmewafanya nini hawa wanaume huu mwaka, mbona wana hasira hivi?

thread inahusu nini?

Malalamishi yapo jinsi zote ndio maana yakazaliwa maneno kama wanaume wote ni mbwa , hata hapo juu pia umelalamika kuwa wanaume hawaamni kama kuna kukataliwa , na mimi nakuambia ni hao wa kwenye cycle yako ndio wapo hivyo na sio wote.
 
Hapa kuna tatizo la kuchanganya wavulana na wanaume πŸ€”
Kabisa. Ila siyo wavulana tu. Kuna baadhi yetu wanaume ambao wana fikra potofu pia; japo binafsi naamini wengi wa aina hii ni wale "traditionalists" au ambao hawana exposure au elimu dunia ya kutosha au uzoefu na wanawake productive. Hao huwezi wabadilisha kwa slogans za 1995 Beijing World Conference on Women tu peke yake, kama baadhi ya wachangiaji hapa wanavyojaribu kuuaminisha umma wa JF.
 
Yeah naunga mkono hoja
 
Zamani niliamini wanaume hawaumii mala ya kwanza kuona mwanaume analia nilishangaa
Pia nilidhani wanaume wana akili sanaaa heh nikaja kugundua wengine ni wajinga kupindukiaπŸ™Œ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…