Jana nimeenda club kwa mara ya kwanza, nimetoka nduki baada ya kuuziwa maji 4000/=

Wewe ni shujaa kwa nini ujisikie aibu na huzuni? Ulimbukeni wa kutaka sifa hauna faida yoyote...Eti maji ununue kwa shikingi elfu nne!

BORA ELFU TATU INAYOBAKI NIINGIE MTAANI NIMPE OMBAOMBA kuliko kumpa over profit nyang'au fulani
 
Issue ni Ku-play smart Watz wengi starehe zao za kimasikini Sana ngono na pombe.

MTU bahili na smart yeye sio MTU wa. anasa bali bata.
Exactly [emoji1666] niliwahi kufika hapo the Cask, kiukweli ni sehemu expensive na kama mtu kipato chake ni kidogo si sehemu sahihi, bora aende sehemu nyingine ambapo hayo maji ya 4000 utayapata kwa 700 au walau buku. Nakumbuka last year October tulipita hapo but tulikuwa kikazi, chakula watu 4 and drinks ilikuwa karibia laki moja na ushee hivi..
 
Ungekunywa tu hayo maji ingekusaidia sana kuutikisa umasikini
 
Ni kwel mkuu mfano hapo samak samak kweny hako ka VIP kao unaweza jihisi hauko daslam due kuna ka ubarid flan iv....na nlichoona kingine ni kama wanawahudumia zaid wagen kutoka nje
Bilashaka ndo hivyo,wakiweka bei sawa na sehemu za kawaida,hata wakwapua simu,waleta vΓΊrugu na watu wengine wasiowastaarabu,watajazana humo,dawa ni kupandisha bei vitu,ili watu tujichuje kutokana na vipato.
 
Duh Sasa hapo ukijaribu kuiga upate sifa unaumia lazima.
 
Chai..
Lakini poa tu..
 
Niliendaga kitambaa cheupe kuangalia EPL daah mule sijaiona starehe yoyote zaidi ya makelele, halafu na hili joto la Dar,Mimoshi ya Shisha,watu shazi,huku mziki. Nilichemka nilikaa nusu saa na kuondoka pamoja nilitoa 10k mlangoni.Nikatafuta chaka jingine la kutizama mpira, ila kuhusu mademu mule kuna sampuli za kila aina mademu wakali
 
Mshua ulifanya kitu Cha kishujaa sana ni vyema ulichekwa lakini ulisevu maokoto Yako kuliko ungekubali kutumia kwa kuhofia aibu[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…