Jana ulikuwa ni mkutano wa CCM uliovalishwa vazi la CHADEMA

CHADEMA limebaki jina tu. Ila imechoka chakaliii.

Unapandisha jukwaani mianasiasa iliyokula IMESHIBA inaongea ikihema JUU JUU.

Sura zile zile kwa miaka 15 Sasa.

Stori zile zile.

Siasa zile zile.

Hakuna JIPYA.

Wewe una jipya gani?. Baki na CCM yako hujalazimishwa.
 

Mbowe kaboronga Jana, lakini ujinga wa mbowe usiulete CHADEMA. Lissu akichemka Basi itabidi niachane na siasa.
 
Uko sahihi kabisa. Na maana yake ni kwamba hana sifa za kuwapigania wananchi anaowaaminisha kwamba atawaletea ukombozi. Musa wa nchi hii kwa kipindi hiki alikuwa JPM. Wao wakamuona adui. Sasa wamepoteza dira. πŸ˜€πŸ˜€ na badoooo

JPM alikuwa Mussa gani?. Mussa hakuwa mbaguzi na muuaji dhidi ya raia wake. Kapamabana na CHADEMA mpaka kafa.
 
Uko sahihi kabisa. Na maana yake ni kwamba hana sifa za kuwapigania wananchi anaowaaminisha kwamba atawaletea ukombozi. Musa wa nchi hii kwa kipindi hiki alikuwa JPM. Wao wakamuona adui. Sasa wamepoteza dira. πŸ˜€πŸ˜€ na badoooo

Sifa unazo wewe muoga uliyejificha ukisubiria Mbowe akusemee.
 
Kama kweli ccm wamempongeza Mbowe, basi kazi imeisha. Hatuna upinzani tena, tuna waungaji mkono juhudi za Samia
 

Punguza kelele Kama sio mpinzani. Mbowe Mbowe, wakati upo CCM juzi mlimwita gaidi, leo mnajifanya kukasirika kwanini hajaisema CCM.
 
"Hakukuwa na sababu za kumtaja Rais, achilia mbali kumsifia"

Hiyo kauli mara nyingi inatoka kwa cowards, wanaoendekeza siasa za kuvizia, wakidhani mwenyekiti wa Chadema kumtaja na kumsifia Samia, basi Chadema itapoteza umaarufu wake.

Hayo kwangu ni mawazo mgando yaliyopitwa na wakati, kama hamuwezi kurekebishana wenyewe kati yenu, au kutoa shukrani kwa mpinzani wenu, hizo ni siasa mfu zilizopitwa na wakati, hamjui hata kwenye siasa kuna fair play.
 
JPM alikuwa Mussa gani?. Mussa hakuwa mbaguzi na muuaji dhidi ya raia wake. Kapamabana na CHADEMA mpaka kafa.
Una ushahidi wa mauaji aliyoyafanya?
Hata hivyo ni kweli musa hakuua lakini waliokengeuka walikufa jangwani na wengine ardhi ilifunguka ikawameza!

Na maadui waliokuwa kikwazo cha safari yao, walizamishwa baharini. Sio wote ni waisrael wanaohitaji kuvushwa, wengine walikuwa wafilisti wanaozuia safari...hakuna budi wauwawe ili safari iendelee
 

Yeye ndio alizamishwa ndio maana kafa kwa aibu. Leo watu wanafanya mikutano kwa amani Tena kwa kusindikizwa na Polisi.
 

Maneno mengi bila maana. Mbowe ukimfuata kichwa kichwa hautamuelewa. Wewe jifanye mchambuzi wa kila kitu utakula za uso. Mkutano mmoja eti ulikuwa mkutano wa ccm. Una akili kweli?. Kama Kuna jambo hulijui kaa kimya, usioneshe ujinga wako.
 
Watu wanamsikiliza Kiongozi.
Atakachoongea Kiongozi Mkuu ndio kinasikilizwa.
Hao wengine hatuwazingatii sana

Kiongozi gani? Mbowe kaongea kwa nafasi yake lakini msimamo wa CHADEMA unajulikan. CHADEMA itawasumbua Sana Kama mtaingia kichwa kichwa bila kutafakari.
 
Watetezi wa wananchi kwa sasa ni team magu tu, wapinzani washalambishwa asali.πŸ˜€πŸ˜€
Hawaoni hata haja ya kuzungumzia mfumuko wa bei, mikopo isiyo na tija, safari na ziara za viongozi ndani na nje ya nchi. Wao ni kupongeza tu!

Wewe ulikuwepo Jana?. Tatizo umesikiliza hotuba ya Mbowe pekee. Mbona Viongozi wengine wameongelea issue za wananchi?. Msitumie kauli ya Mbowe. Jana mlisema mkutano hata kuja mtu wamekuja watu mnadai mkutano wa CCM .
 
Aisee Taikon ktk mabandiko yako yote hili umesema mambo ya maana sana

Sasa na wewe anzia hapa usirudi tena kule kwenye laana za wazazi
 
Mbowe ule ni wajibu wake cheo na hadhi aliyonayo inakwenda sambamba na maswahibu anayopitia

Kuwekwa jela sio sababu eti asitimize uamuzi wake

Yeye anapaswa kuendelea kutimiza kama anadhani kafanya part yake na akae kando Taikon akachukue gurudumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…