Janet Yellen: Washington yatatokea madhara makubwa Marekani ikijitoa China

Hukumsikiliza vizuri yule Mbunge wa Hong Kong kwenye video aliyokuwa anaongea na mtangazaji Mhindi. Ameeleza vizuri jinsi jinsi ambavyo IMF na World Bank wanakuwa misled na serikali ya China kwa kupewa data feki.
Kwa hiyo tuache taarifa za IMF na WB tuchukue maneno ya Mhindi na huyo mbunge wa HK? 🤭🤣🤣🤣
 
Kati ya US na China nani mchokozi? uyo US anafanya chokochoko kule TAIWAN, punguza mahaba kwa hao west na punguza chuki kwa China. China anachokozwa na US unataka aendelee kumwabudu??
 
Mkuu tuambie indicators za GDP ni zipi? Tuanzie hapa, Hizo video nyingi ni Propaganda.
 
Reactions: TPP
Hapo Yellen kasema vizuri kuwa itakuwa mbaya endapo Marekani atajiondoa China kiuwekezaji.

Kumbe uwekezaji mkubwa ni wa Marekani na wala haringi
Hilo mbona linafahamika, wakiondoka watakuja wengine kwenye production line ile ile, swali ni je hao watakaoondoka(wamarekani) wataenda kuwekeza wap bila kuathiri production line I.e. price of raw material, energy na supply route!
 
Uchumi wa China uliitegemea sana Marekani na ulijengwa wakati wa Hu Jintao. Huyu jamaa yeye amekuja na zile fikra za kizamani za anti-US zinafofuatwa na Putin na ameanza kuharibu nchi yake. Usitukane wakunga wakati uzazi ungalipo.
Mchina uchumi umeyumba sababu ya athari za corona, kipindi cha lockdown uzalishaji Ulishuka sana,, kwa sasa anarudi no maana hata serikali imeandaa stimulus package kwa makampuni yaliyopigika kipindi cha lockdown
 
Hapo Yellen kasema vizuri kuwa itakuwa mbaya endapo Marekani atajiondoa China kiuwekezaji.

Kumbe uwekezaji mkubwa ni wa Marekani na wala haringi
Na tukusaidie tu viwanda vingi vya marekani vipo china kwa sababu ya cheap energy, easy supply routes na sheria ngumu za mazingira ambazo zipo marekani, wamarekani wenyewe hawawezi kukubali hii kitu watamuondoq huyo babu kulinda uchumi wao!
 
Kati ya US na China nani mchokozi? uyo US anafanya chokochoko kule TAIWAN, punguza mahaba kwa hao west na punguza chuki kwa China. China anachokozwa na US unataka aendelee kumwabudu??
US iko Taiwan, Japan, Phillipnines, na Korea kwa tangu mwaka 1949. Kwa hiyo haijachoikoza, na hayo yalikuwa makubaliano baina ya Merakani na nchi hizo na ilikuwa ni kitu normal tu kabla ya chokochoko zilizoanza kufanywa na Rais wa Maisha.
 
Unazingua sana uelewa wako ni mdogo sana kwenye haya mambo. Mmelishwa sana Propaganda na US.
 
Mchina uchumi umeyumba sababu ya athari za corona, kipindi cha lockdown uzalishaji Ulishuka sana,, kwa sasa anarudi no maana hata serikali imeandaa stimulus package kwa makampuni yaliyopigika kipindi cha lockdown
Nimeshangaa kuna mwingine anashangaa China kuja na stimulus package. Kwenye uchumi hii ni kitu ya kawaida sana
 
Mkuu tuambie indicators za GDP ni zipi? Tuanzie hapa, Hizo video nyingi ni Propaganda.
Huyo mama ni mchina, na yeye mwenyewe ni mchumi. Ameweka takwimu za kutosha kukonyesha GDP halisi ya china ni ipi. Amefikia hata kusema kwa nini China bado ina njia ndefu kiuchumi kwa sababu ya kutokuwa na national brand yoyote inayotambulika duniani na kwamba viwanda vyote vya china vingi ni vya kuassemble parts zilzonunuliwa nje au kutoka kwenye viwanda vya nchi za nje na hata kueleza kuwa Huawei bado siyo national brand ya China. Mwishoni ametumia muda kujibu maswali kadhaa aliyokuwa anaulizwa na watazamaji wake na kayajibu vizuri sana.
 
Hujajibu SWALI nitajie indicators za GDP.
 
Achana na hizo video mdogo wangu zinakupoteza, China hawana National Brand inayotambulika duniani.? Kwaheri ndugu ntakua napoteza muda kubishana na wewe.
 
General Li Shangfu yupo chini ya vikwazo toka U.S toka 2018 kivipi anaweza zungumza na mwenzie wakati amewekewa vikwazo na US wenyewe ?
 
Unazingua sana uelewa wako ni mdogo sana kwenye haya mambo. Mmelishwa sana Propaganda na US.
Mimi nimewahi kuishi Hongkong, Japan, Korea na Marekani ingawa sijawahi kuishi Taiwan.

Historia ya kwa nini jeshi la Marekani liko kwenye maeneo iko wazi na hayakuaza leo. Kuwa US wana mktaba wa kulinda Japan baada ya kuiangusha mabomu ya atomiki mwaka 1948 na bado wanaheshimu mktaba huo. Baada ya Korea kugawanyika kati ya North na South na kupigana vita mwaka 1952 ahdi 1953, Urusi iliamua kuisidia sehemu ya North ambayo ilikuwa na viwanda Sana kusudi wajenge nchi ya kikomunist chini ya Kim Il Sung, Marekani ikailinda sehemu ya kusini ambayo ilikuwa maskini sana wakati huo ikiwa chini ya Syngman Rhee ikiahidi kujenga uchumi wa Capitalism. Vile vile baada ya vita ya China ya mwaka 1949, Chiang Kaishrk alipohamia Taiwani alisaidiwa na Marekani kujenga uchumi wa kicaptalist na kumwachia Mao kujenga uchumi wa kikomunist huko China bara. Kuanzia mwaka huo 1949 Marekani imekuwa inalinda visiwa vile vya Taiwan, ndiyo maana kwenye population ya wachina walioko marekani leo wengi ni wa kutokea Taiwan.

Kwa kufuata historia hiyo utaona wazi kuwa Marekani imeshakuwapo pale kijeshi kwa miaka zaidi ya 70 na maisha yalikuwa yanaenda vizuri tu sehemu zote bila msuguano. Tatizo lilianza wakato Rais wa Maisha alipoanza kunyang'anya maeneo ya bahari ya China sea kutoka kwa majirani zake akijenga visiwa artificial. Hii tabia ya kunyanganya maeneo ya majirani (conquests) ni tabia ya kizamani sana (barbaric) ambayo naona inafanywa na viongozi wa China na Urusi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…