Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Tatizo Kuna watu wanadhani wanajua kila kitu. Kilichototea JKCI, Ni Dr. Longopa kukaimishwa kazi alizokuwa anafanya Dr. ******* ambae ana kazi maalumu kwa sasa.
 
Wewe una matatizo. Unafikira za kimihemko. Kutompenda JPM kusiwe ni kikwazo cha kuwa na fikra huru. Utapata ugonjwa wa moyo maana unaye hadi 2025.
Kuna baadhi ya watu wanachuki mpaka wanaongea mambo ya kijinga jinga bila kujua kama niya kijinga!
 
Hata huko India yaani ngumi hatariiiii mabarabarani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kiwango kikubwa nakubaliana na angalizo lako!
 
Mtu akikuletea dini haina maana kuwa yeye hana dhambi na Mungu anamsikia zaidi yako!

Kukuletea dini haina maana kuwa yeye ni zaidi yako!
Papa anafanya pasaka kwa streaming, seuse wewe uliyeletewa.Makanisa yamefungwa Rome na Vatican, Misikiti na Hija za Maka. Sisi tunadhani wenzetu hao ni Wajinga katika imani

Utasema nini katika Ukatoliki zaidi kumshinda Mkatoliki Papa?
 
Mimi nimeongelea mambo yaliyo halisi, wewe unatuletea nadharia!
Uwaambie watu kuwa maisha ya ulaya watu wanakaa na kulipwa mishahara tu, hawafanyi kazi kama Tz!
Huwaelezi watu kuhusu Employment Insurance.
Unadanganya eti Upweke ndiyo maana wanaweka karantini!
Huo ndio uhalisia kweli.

Mtu aliyesoma bandiko lako hapo juu na anayeishi nchi za magharibi huenda atapatwa na mambo mawili.

Moja, anaweza kuwa depressed kabisa hata kuhitaji dawa akifikiri kiwango cha viongozi kama wewe.
Pili, anaweza kuangua kicheko na kujichafua kama si kuzimia.

Hakuna grey area
 
😀😀😀😀😀😀😀 umeongea point za kusimumua sana...ukweli ndiyo huo...

Za kwako sometimes changanya na za mbayuwayu, anayewaambia wasali yeye msafara wake unatembea na ambulance 2, madaktari bingwa, tank la sanitaiza, am sure na vifaa tiba vyote muhimu...

Everyday is Saturday.......................😎
 
Soma aya ya mwisho ya bandiko lake. Anajirudi kwa kujua kaongopa sana , kapotosha sana na kadanganya sana. Nafsi inamsuta

Huyu bw anafanya exploitation ya Watanzania. Sijui analipwa nini lakini si bure.
Hizi kazi za kumfurahisha mtu ni ngumu sana, kuna wakati unatakiwa ujitoe fahamu. Ni ngumu kwakweli
 
Acheni ujinga wenu nyie majuha wa Lumumba!! Hivi kwanini mnakuwa na ujinga wa kudhani Magufuli anachukiwa?!

Mimi na wewe nani mwenye akili ya kipuuzi?

Hakika ni mjinga tu ndie anayeweza kuamini eti coronavirus haiwezi ku-affect watu makanisani na misikitini!!

Hakika ni mjinga tu ndie anayeweza kutetea suala la kutaka ndege kutoka nje na watalii waendelee tu kuingia Tanzania wakati nchi yenyewe hata uwezo wa kukabiliana na majanga haina!!

Kwa bahati mbaya, wakati mnaendelea kutetea ujinga, wenzenu huko duniani sio wajinga ndo maana ndege nyingi duniani zime-cancel international flights!

Hivi umeshawahi kujiuliza kingetokea nini endapo waitaliano na wenyewe wangekuwa wapumbavu kama sisi na kuendelea kuingia Tanzania kwa sababu Italy ni one of Tanzanian Tourism Destination; especially Beach Tourism!

Hivi umeshawahi kujiuliza tungekuwa na hali gani endapo ndege kutoka Iran na Wa-Iran wangeendelea kuingia Tanzania kama ilivyo ada?

Hivi umeshawahi kujiuliza tungekuwa kwenye status gani endapo Wamarekan wangeendelea kuingia?

Thanks God, wakati nyie mnaleta siasa na kutetea wanasiasa, wenzenu wanaendelea kutumia akili zao sawasawa na ndio maana pamoja na kuwaambia waendelee kuja, ndo kwanza waliopo wanahangaika kuondoka!!

Lakini hata huko duniani watu wenye akili za kijinga kama hizi, hivi sasa ndio walioathirika zaidi!!!

China, as Ground Zero for COVID-19, baada ya Dr. Li Wenling kutoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu a very strange virus, akalaaniwa China kote na watu aina yenu! Kama hiyo haitoshi, mamlaka za China zikamsimamisha kazi.

Kila mmoja anafahamu what happened to China!

Iran nako, wakati mambo China Fire na bila kujali muingiliano wa kiuwekezaji kati ya China na Iran, wenye mamlaka Iran wakatangaza wazi kwamba nchi hiyo haina mpango wa kufunga mipaka yake, na Rais wa Iran nae akanukuliwa akisema:-
We have no plan to quarantine any district or any city. We only quarantine individuals. If an individual has early symptoms, that person must be quarantined.
Na leo kila mwenye akili anafahamu what's going on in Iran!

Spain nao, kwa kujua they don't share a border with Italy, wakadhani wapo salama!! Wakati hali ni tete nchini Italy, wao ndo kwanza wakawa wanaendelea kufurahia burudani ya soka inayowakutanisha maelefu viwanjani!!

Kama hiyo haitoshi, Dr. Fernando Simon... Head of Medical Emmergency in Madrid, nae akanukuliwa akisema "Spain will only have a handful of cases"

Hapa chini ni video ya Dr. Fernando akizungumzia issue ya COVID-19 baada ya mambo kuwa yameshaharibika!


Kama hufahamu Kihispania, tumia Google Translate kusoma maoni ya Spaniards uone hivi sasa wanavyomlaani kwa kuleta mzaha hapo kabla... mzaha ambao mnaoleta nyie na Magufuli wenu!

Leo hii Spain keshampita Iran na anamfukuzia Italy!

Hata Donald Trump nae alikuwa analeta masihara wakati coronavirus inaanza kushika kasi! Ni couple of days ago alikuwa anaita Chinavirus, leo hii US ndie ina mostly infected COVID-19 patients.

Sasa endeleeni tu kutetea ujinga !!!
 
Tufungulie shule na vyuo tukasome..muda unakwenda huu..

.
 
Binafsi sijaona kosa la mtoa mada

nafikili wachangiaji wengi wanashindwa kujua hoja hasa ya mada

mtoa mada haconclude kwamba njia aliyoitumua Magufuri ndio sahihi! la hasha!
anachomaanisha ni kwamba njia hii ni sahihi kwa mazingira yetu, kutokana na nguvu ya kiuchumi tuliyonayo

Na isitoshe Corona si tishio sana kwa afrika(nisiulizwe kwanini tafadhari) hivyo kutofanya total lock down haitokua na athari kubwa kama kwa wenzetu

Lakini njia sahihi kwa nchi zenye uchumi mzuri ni Total Lock down kama inavyoshauriwa na wataalamu.
 
Mkuu;
Wewe unadhani angefanyaje ili kukabiliana na hili janga la COVID-19?
 
Hujaelewa msingi wa mada yangu!
 
Mbona utaratibu upo wazi,mgeni ygyote au mtalii toka nje ni lazima akae Karantini 14 says kabla ya kwenda popote huku vipimo vikihusika kuthibitisha afya yake mara 3 zaidi .
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona utaratibu upo wazi,mgeni ygyote au mtalii toka nje ni lazima akae Karantini 14 says kabla ya kwenda popote huku vipimo vikihusika kuthibitisha afya yake mara 3 zaidi .

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi unadhani kuna effectiveness yoyote kwenye hilo suala?! Hebu msome huyu mama aliyekuwa anawalalamikia abiria pale JNIA:-

​

Utaona hiyo tweet ni ya juzi tu hapa!! Na usisahau, mtoto wa Mbowe alikutwa COVID-19 positive sio kwamba alisafiri nje bali alikutana na mtu kutoka nje ambae alikuwa positive!

Na huyo mtu kutoka nje kapitia viwanja hivyo hivyo unavyoamini kuna utaratibu wa quarantine dhidi ya COVID-19!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…