Januari Makamba kukataliwa na Wajumbe 1,463 kati ya 1,915 inatoa taswira gani kisiasa?

Januari Makamba kukataliwa na Wajumbe 1,463 kati ya 1,915 inatoa taswira gani kisiasa?

Kiburi, kijisikia ana akili kuliko wengine, kuwa na baba anaeongea pasipo breki, kujulikana kuwa protegee wa Kikwete, kujisikia kuwa ndio raisi ajae, kusikia kwamba aliweka mashari apewe wizara gani na wafukuzwe wateule wa Magufuli Tanesco na wizarani, matatizo ya umeme, majibu ya uongo anapohojiwa au kuulizwa maswali, visingizio vya kumlaumu Magufuli katika kukatika umeme, kuwa na dada tapelitapeli, suala la kreni nk.
Dah, hivi chuki na uzushi huu kwa binadamu mwenzenu huyu ni kwa ajili ya miaka hii hii sitini tunayoishi na kufa au wenzetu mna zaid?!!!
 
Umeua!! Hiyo ya kujisikia kuwa ndiyo Rais ajaye nimeipenda. Kwa Tanzania ukipania sana U-Rais kamwe huwezi kupata.
Wote waliopania hawakuwahi kuwa Marais wa Tanzania. Mungu humdondoshea usiye mtarajia.

A H Mwinyi alipata badala ya Salim Ahmed Salim aliyekuwa anatakiwa na Nyerere. 1985

B W Mkapa alipata badala ya John Malecela na Horace Kolimba waliokuwa wanapendwa na Mwinyi. 1995

Jakaya Kikwette alipata badala ya Fredrick Sumaye, Mwandosya na Kigoda waliokuwa favourites wa Mkapa. 2005

Magufuli alipata badala ya Bernard Membe aliyekuwa ameandaliwa na Kikwette baada ya kumuengua rafiki yake wa muda mrefu Edward Lowassa. 2015.

Samia Suluhu alipata baada ya Magufuli kunyakuliwa na Ziraili licha ya kujiwekea mazingira ya kuwa Rais wa maisha.
 
Wasira naye alikuwepo kwenye kinyanganyiro? Alipata hata kura tatu?
Alikua anagombea ili iweje maana sioni Kama analo jipya lakutuambia.
Ulikuwa huna haja ya kuchangia mada hii kama hukufuatilia Mkutano Mkuu wa CCM!!
 
Kwa taarifa yako Wasira kapata zaidi ya kura 400 na yupo kwenye NEC ya CCM. Unajivunia damu ya CHADEMA kumbe damu yenyewe Ina leukemia
Hongera zake Babu yangu wasira. Nakumbuka Kuna kipindi tulikua nae upinzani. Enzi za NCCR Mageuzi, enzi za Mabere Marando (hili jina utafikiri Ni la utani kwa wanaojua kisukuma)
 
Acha na na namba, sistystem ikutaka uwe rais unaenda tu.. lowasa alikuwa na watu kumzidi rais ilikuwaje???
Kuna tofauti sana kuwa na watu uliowahonga fedha na watu ambao hujawahonga fedha!
Mara nyingi kuna watu huwa wanaamini wana watu kwa kuwapa rushwa ila ni bora zaidi ukawa na watu waliokuchagua wenyewe nafsini mwao!
Kwa sehemu kubwa Lowassa alitumia fedha kuwashawishi watu ndo maana aliangukia pua!
Nadhani umenielewa!
 
Bashungwa na Makamba nani aliyezaliwa na kukulia CCM? kwanini Bashungwa apate 720 na sio Makamba?

..bashungwa anasifiwa kwasababu wizara ya ulinzi haifuatiliwi na kuchunguzwa kama wizara nyingine.

..kule wanakula rushwa na kufanya madudu kadiri wanavyotaka na hakuna mtu wa kuwakoromea.
 
Januari Yusuph Makamba, Mwanasiasa kijana mwenye ushawishi mkumbwa ndani ya Chama cha Mapinduzi ambaye Mwaka 2015 aliingia 5 bora ya wagombea wa Urais.

Hivi majuzi tumeona kwenye uchaguzi wa kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) akishika nafasi ya 11 kwa kupata kura kiduchu 452 kati ya kura 1915 kwa tasfiri nyepesi wajumbe 1,463 walimkataa kwenye sanduku la kura.

Ni nini hasa kimemdondosha kisiasa kijana huyu machachari kutoka 5 bora za Urais 2015 hadi nafasi 11 na kushindwa hata kuingia 10 bora licha ya taarifa kudaiwa ndiye mgombea aliyetumia pesa nyingi kuliko wagombea wote wa NEC.

Wizi,uchawi na na kifo cha aliendoka
 
Dah, hivi chuki na uzushi huu kwa binadamu mwenzenu huyu ni kwa ajili ya miaka hii hii sitini tunayoishi na kufa au wenzetu mna zaid?!!!
Babake alisema wao hawafi, miaka 60 ya kuishi wewe umeitoa wapi? Unataka kuwapunja?
 
Kwa msiofahamu ni kwamba January Alipata kura nyingi zaidi ya hizo isipokuwa busara ilitumika kupunguza tension ya kisiasa na ndio maana kura nyingi akapewa mtu ambaye hafahamiki na Hana athari zozote kwa siasa za kitaifa.
Ndiyo awekwe wa 11. Hata kama ni kupunguza tension.
 
Dah, hivi chuki na uzushi huu kwa binadamu mwenzenu huyu ni kwa ajili ya miaka hii hii sitini tunayoishi na kufa au wenzetu mna zaid?!!!
Tatizo ukipenda, chongo utaita kengeza

Kila nililotaja hapo juu naweza kukupa mfano

Na kama unafahamiana nae muulize labda kwa jambo moja. Muulize ule mlolongo wote uliomfanya sio tu waziri, pia waziri wa Nishati. Muulize ilikuwaje hadi kupewa kwanza uwaziri, pili wa nishati. Je Samia ndio alimchagulia wizara? Nani walihusika katika kuwa kwake waziri?

Pili muulize ilikuwaje alipopewa uwaziri kina Tito Mwinuka ikabidi waondoke waje kina Maharage Chande. Nani alileta hiyo ajenda? Kama ni yeye alitumia ushawishi gani hadi Raisi akakubali? Nani walimuunga mkono kumshawishi Samia? Nini alichofanya au anachofanya Maharage Chande ambacho Mwinuka hakuwa anafanya? Tanesco imekuwa bora zaidi?

Kwa hiyo kama ni chuki unaziongelea hapa, labda ushauri wako kampe huyo January kwanza, ndio uje kutuambia sisi. Unachukia hadi watu waliokufa na kusema hutaki kufanya kazi na walioteuliwa nao, uko sawa wewe!

Tanesco inaongozwa na aliekuwa mkurugenzi wa Vodacom sijui, Wizara ya nishati inaongozwa na mtu ambae background yake hasa ni kuandika hotuba za Kikwete, kasomea fasihi sijui. Halafu tunapata matokeo madudu kabisa mnasema acheni chuki binafsi. Kuna watu mnafanya utani na nchi hii.

Watu kama January uwepo wao katika baraza la mawaziri na connection zao kwa baba yake na kina Kikwete unamfanya Samia awe kiongozi weak, na hilo Samia anapaswa kulitambua, na nitasema hata mbele yake.
 
kwenye kura 1915 unapata kura 452,kura 1463 azijakupa kura inamaana hao wapiga kura 1463 ambao ni wengi awakuamini au awakutaki.lakini mtu anatangazwa kashinda ilhali waliomchagua ni wachache.

ingekaa sawa kama mgombea apate walau 50%+1 ya wapiga kura hapo utaona mwanga wa uchaguzi mzuri.
 
Kuna tofauti sana kuwa na watu uliowahonga fedha na watu ambao hujawahonga fedha!
Mara nyingi kuna watu huwa wanaamini wana watu kwa kuwapa rushwa ila ni bora zaidi ukawa na watu waliokuchagua wenyewe nafsini mwao!
Kwa sehemu kubwa Lowassa alitumia fedha kuwashawishi watu ndo maana aliangukia pua!
Nadhani umenielewa!
Ndg katika siasa bila pesa wewe si kitu..hiv unafikiri january makamba hajatoa pesa...
 
Back
Top Bottom