January Makamba kuitwa Rais ajaye na ukaribu wa familia yake na Mange Kimambi kumemponza na kutumbuliwa nafasi yake ya Waziri wa Mambo ya Nje

January Makamba kuitwa Rais ajaye na ukaribu wa familia yake na Mange Kimambi kumemponza na kutumbuliwa nafasi yake ya Waziri wa Mambo ya Nje

Bado wa fedha. Ndio alitakiwa awekwe pembeni wa kwanza. Hao ndio wapigaji hatari. Japo nahisi something fishy. Inaweza kuwa trik kuandaliwa kwa ajili ya uchaguzi ujao
 
Kuna jopo la mabalozi wa zamani kina Balozi Ombeni Sefue na Peter Kallaghe lilitumwa kufanya uchunguzi Wizara ya Mambo ya Nje, likakuta madudu mengi sana.
Ina maana ni wizara moja tu iliyochunguzwa?.....
 
Hawa wametolewa ili wa focus na goli la mkono 2025. Hawa ndo campaign coordinators na mafundi wa njia za panya.
Nape/ Makamba makampeni meneja. goli la mkono .this time sidhani mama atakubali dhambi hiyo ninamuona kuwa ana hofu ya Mungu. si ya kinafiki
 
Hizi ni porojo... Kama Kuna madudu washtakiwe kwa ubadhirifu au makosa mengine? Hapa mmekosea sana sababu tunaanza kampeni za kutaka urais rasmi
Kuna mambo ya kisiasa nimeyataja hapo juu.

Rais Samia anateua na kutengua watu sana kiasi kwamba viongo,i wanakosa hata muda wa kufanya kazi.

Ingawa watu kama Nape Nnauye walijitakia wenyewe.
 
Kila nyakati zina mtu wake. Unategemea wazee wa 1995 ndo wawe bench la ufundi Leo?
Kuna kina Makala, Makonda, Ma DED wote nchi nzima hawa ndio waiba kura na hata Jiwe aliwahi kusema kama DED unalipwa na Serikali ya CCM alafu utangaze mpinzani mshindi anakulima kichwa

Wizi wa kura CCM mbona unaeleweka kabisa Mkuu wala Chama hakimtegemei kilaza kama NAPE au January. Nape alishindwa kuibia majibu kidato cha nne akala D kama zote. January nae alifutiwa mpaka matokeo hivo hana kipaji cha kuiba kura

Wazee hawaendi front, ni makada ndio wanaiba swala la kuiba kula ni collective effort sio kweli kwamba kuna watu fulani CCM ndio mabingwa wa wizi, Kina January wanaweza kufukuzwa CCM na bado Chama kikashinda.
 
Hawa wahuni Kuna kitumwendazake aliona akawatimua, Sasa imedhihirika kweli Ni wahuni. Imagine Makamba alitaka aibe pesa kwa kisingizio Cha kujenga magorofa Nairobi wakati Bumbuli hakuna hata gorofa moja.
Bumunda limehusika Sana na gharama kubwa za vifurushi na ulevi usio na tija Hadi kamponza yule mhaya.
Kama mama anataka tuendelee kumuunga mkono atuondolee Mwigulu mmiliki wa timu za mpira na kampuni za mabasi na huyu aliyeamua kuwaumiza wakulima wa miwa msomali ambaye hata uraia wake Ni wa mashaka. Bashir aliyebadilisha jina na kujiita Bashboy.
Commemts za leo zinastarehesha sana kwa kweli.

Sijawahi kurudia kuisoma comment ya mtu mara mbili mbili kwa utamu wake kama zilivyo za leo.
 
ni nani anayemuita huyo mwizi wa mitihani rais ajaye? mtu mshenzi na fisadi mwenye tamaa isiyoelezeka kama huyo makamba atakuwa rais wa wapi? huyo ataendelea kuutafuta bila kuupata milele
 
Nape hasa kauli ya juzi imemponza, ni sawa na kusema chama chake kinaiba kura na hakijawahi kushinda.
Hakuna MTU anayesema ukweli Kama mtoto mdogo na mlevi. Juzi nape alikua amelewa chakari ndio akaongea ukweli wa rohoni mwake.
Kama waziri mzima na mwenezi mstaafu akisema CCM HAIJAWAHI kushinda kihalali Ila wanaiba kura, Mimi Ni Nani nisiamini?
Kusema ukweli kuliliponza Levi.
 
Hukuona madudu aliyoyaanzisha ya kutaka kugeuza wizara ya mambo ya nje kuwa wizara ya uwekezaji wa kujenga magorofa Kenya?
Licha ya hayo. Madudu aliyofanya tanesco Ni zaidi ya kunguni.
Umeme ulikua ushuke Bei mashine zikiwashwa lkn ndio kwanza makato yametoka elfu na Mia tano mpaka elfu mbili.
Umeme huo unatumia maji, maji Wala sio dizeli lkn unapanda Bei.
 
Kuna uwezekano mkubwa rais Samia Suluhu Hassan ametengua iteuzi wa January Makamba kwenye nafasi ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki kutokana na kuitwa rais ajaye na mashabiki zake wa kusiasa hasa kwenye mitandao yake ya kijamii

Pia mahusiano ya dada yake Mwamvita Makamba na mwanaharakati wa kwenye mitandao ya kijamii Mange Kimambi yaweza kuwa sababu nyingine ya kupigwa ngwara January kwenye nafasi yake hiyo

Rais Samia Suluhu Hassan amefanyamabadiliko madogo kwenye baraza lake la mawaziri na kuwapiga ngwara baadhi ya mawaziri akiwa Makamba

Kabla ya utenguzi huo wa rais Julai 21, 2024 January makamba alikuwa akitumikia nafasi ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki

Uchunguzi unaonyesha kuwa Makamba kila akiposti kitu kwenye kurasa zake za kijamii wachangiaji wake wakubwa wanapenda kukomenti rais ajaye au my president au president material

Inawezakana Makamba hajawatuma washabiki wake hao kuandika hivyo au kumuita hivyo wanapokutana naye au pengine ni mbinu zake za kisiasa kuwajenga watu hao wafanye hivyo

Hata humu jukwaani Jamii Forums kuna post nyingi zilizo andikwa kuhusu January Makamba kwamba ni rais ajaye au "president material"

Mara chache Makamba alikuwa akiwaeleza mashabiki zake hao wa kisiasa kwa kukanusha kuwa urais 2025 mpaka 2030 ni wa rais aliyepo madarakani Samia kumaliza muda wake na kwamba yeye kama kufikiria kuwania nafasi hiyo ni baada ya kipindi hicho cha mwisho cha urais wa Samia

Pengine hali hiyo imemtisha rais Samia na kumuweka Makamba benchi kwanza kwenye uwaziri ili ampunguze kasi na kusahaulika kwenye ulimwengu wa siasa za Tanzania

Kwenye ukaribu wa dada yake Mwamvita na Mange Kimambi kuna uwezekana pengine kumemponza kutokana na kudaiwa kuwa ndiye anayempa Mange taarifa nyingi za ndani ya Serikali na ofisi ya rais
Kwa mantiki hiyo Kafulila naye ajiandae kutumbuliwa kwani kuna watu wanamtaja taja sana kuhusu urais
 
Vipi kuhusu kujiuzulu Kwa karibu wake.
 
Back
Top Bottom