January Makamba: Sisi hatuzalishi mafuta

January Makamba: Sisi hatuzalishi mafuta

ni vituko tupu, wenye akili zao wameshaona wasiwatese raia wao, mfano ni zile nchi za ulaya ambazo ziko ndani ya EU, zimesema zitaendelea kuchukua mafuta na gesi Urusi, sie huku ngozi nyeusi sijui hata tunawaza nini. hatufungamani na upande wowote, mzigo uko Urusi, sijui ndo ya mikopo yanatuzuia?
 
Waziri wa Nishati January Makamba, amesema kwamba bei za mafuta nchini inatokana na gharama mbalimbali ikiwemo zile zilizotumika kununulia mafuta, gharama ya usafirishaji na gharama za biashara yenyewe hapa nchini.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 5, 2022, bungeni Dodoma, wakati kujadili hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kilindi, Omari Mohamed Kigua, ya kusimamisha shughuli za Bunge zilizokuwa zikiendelea ili kujadili hali ya mfumuko wa bei ya mafuta nchini.

"Wote tunajua bei za mafuta zimepanda duniani na sisi kama nchi sio wazalishaji wa mafuta tunanunua mafuta kutoka nje na sehemu kubwa ya bei ya mafuta inayopangwa nchini inatokana na gharama ya mafuta yenyewe, gharama ya kuleta, kodi na tozo mbalimbali na gharama za kufanya biashara yenyewe hapa nchini," amesema Waziri Makamba

View attachment 2212801
Moja ya Mawaziri wa hovyo kuwahi kutokea hapa nchi.
 
Wanaleta ghadhabu hawa, huyu hafai kukalia ofisi za Umma.

Waziri mwenye dhamana anakuja na majibu mepesi kwenye suala muhimu kama hili.

Kwa nini wasiindoe hizo tozo ili bei ya mafuta ishuke..

Bei ikishapanda kila kitu kinapanda muathirika ni mtumiaji wa mwisho.
Aliziondoa lakin Mama akazirejesha tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelezo marefu with a lack of substance in it. Mh Speaker kasema mara tatu imetosha.
Hahahaa Alafu bado anaendeleatu. Huyu kama wanampenda wangempa wizara hata ya michezo huko.

Magufuli aliona mbali sana.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Yani ile ishu ya kukataza mifuko ilimpa Credit sana ila daah jamaa mweupe sanaa kichwani
Watu walitii ike amri ya mifuko sababu ya Rais aliekuwepo!..

Kama unabisha mwambie makamba akataze kitu kingine uone kama kuna raia atatii
 
Kwani dictator Iddy Amini aliyesifika kwa kuua waganda ni kwamba aliua waganda wote?
Diakteta wako akikuachia kovu kubwa sana na litakutesa hadi unaingia kaburini!

Una stress nae kiasi kwamba hujawahi acha kumtaja kwenye hoja yeyote ile.

Sikuwahi kujua kama dikteta wako kakuachia stress kiasi hiki!
 
Waziri yupo smart sana kwenye majibu anayotoa shida wananchi wenye hasira kali hawataki kumwelewe ndio maana alisema au tatizo ni huu uwaziri[emoji23][emoji23] .
Jamaa yako ni takataka
 
Niseme wazi mm sio CCM na sio mshabiki wa kada yeyote wa CCM lakini naona tatizo kubwa ktk namna watanzania tunavyofikiri na kuchambua mambo.

Niwe straight, wale woote wanaomshambulia Makamba ni wapumbavu aheri ya mazezeta.
Hivi kuna neno amekosea hapo? Sisi tuna mafuta?
Au ni uongo kwamba bei haijapanda sokoni?
Kumuweka kwenye vitu vinavyoongeza gharama(tozo na kodi) ni sahihi? Yeye ni waziri wa fedha?
Wizara ya nishati ina amua kodi au tozo iwe kiasi gani kwenye mafuta?

Ukijibu hayo maswali ndipo utajua Wewe ni mpumbavu ama la
Wewe ni takataka kama huyo waziri wako!

Umeambiwa kuna kodi kwenye lita moja ytsa mafuta inayofikia elfu 1+

Wewe na Makamba mngekuwa na akili mngepeleka hoja kwenye balaza la mawaziri ili kuondoa hiyo kodi kupunguza makali
 
Makamba kapewa wizara ambayo iko beyond his capacity hiyo wizara inahitaji wajuzi hata kama Hawako bungeni Raisi atafute popote awape ubunge viti maalumu

Makamba yuko zero
Waziri sio lazima awe na uwezo wa kubeba cranes. Yeye ni kiongozi tu chini yake kuna wataalam wengi tu.

Failure yake ni failure ya hao wataalam na aliyewateua.
 
Wewe ni takataka kama huyo waziri wako!

Umeambiwa kuna kodi kwenye lita moja ytsa mafuta inayofikia elfu 1+

Wewe na Makamba mngekuwa na akili mngepeleka hoja kwenye balaza la mawaziri ili kuondoa hiyo kodi kupunguza makali
Mkuu hata miaka mitano bado umeshafilisika huwezi kununua lita moja kwa elfu 3?

Si juzi tu mlikuwa well of?
 
Wewe ni takataka kama huyo waziri wako!

Umeambiwa kuna kodi kwenye lita moja ytsa mafuta inayofikia elfu 1+

Wewe na Makamba mngekuwa na akili mngepeleka hoja kwenye balaza la mawaziri ili kuondoa hiyo kodi kupunguza makali
Ni sawa, mimi na makamba ni taka taka tunakupelekesha Wewe mwenye akili
Utanunua tu kwa bei inayopangwa na takataka halafu utapata jibu nani taka nani mwerevu

Kuna mada nyingine ziko juu ya uwezo wa Watu wenye akili finyu kama Wewe.
Ni rahisi tu kusema ondoa,hujiulizi ukishaondoa hilo gap kwenye budget litazibwa na nini?
Tupe majibu basi mwerevu namna tutakavyoziba hiyo deficit
 
Huu mjadala kuhusu personality ya Makamba hauna maana. Ni bure, ni ubatili, ni kujilisha upepo. Mfumo wa CCM unaompa Rais madaraka yote juu ya nchi ndio uliomuweka hapo alipo. Aringe, ajivune, adharau, aharibu, aongope ni uamuzi wake na wa bosi wake. Hakuna Mtanzania mwingine mwenye sauti juu yake.

Huo ndio msiba mkubwa sana wa taifa hili. Ndio mada ya kujadili. Sio kipara, nasibu, tambo wala nyodo za Makamba. That’s too low. Rise up and fix the systems. Kama hamjajifunza kutoka historia ya nchi bado mnasubiri “masihi” mwingine wa kuongoza nchi hii hakika mtakuwa watu wa maombolezo hadi kiyama.
 
Sisi tunazalisha msururu wa kodi na tozo
Waziri wa Nishati January Makamba, amesema kwamba bei za mafuta nchini inatokana na gharama mbalimbali ikiwemo zile zilizotumika kununulia mafuta, gharama ya usafirishaji na gharama za biashara yenyewe hapa nchini.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 5, 2022, bungeni Dodoma, wakati kujadili hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kilindi, Omari Mohamed Kigua, ya kusimamisha shughuli za Bunge zilizokuwa zikiendelea ili kujadili hali ya mfumuko wa bei ya mafuta nchini.

"Wote tunajua bei za mafuta zimepanda duniani na sisi kama nchi sio wazalishaji wa mafuta tunanunua mafuta kutoka nje na sehemu kubwa ya bei ya mafuta inayopangwa nchini inatokana na gharama ya mafuta yenyewe, gharama ya kuleta, kodi na tozo mbalimbali na gharama za kufanya biashara yenyewe hapa nchini," amesema Waziri Makamba

View attachment 2212801
 
Huu mjadala kuhusu personality ya Makamba hauna maana. Ni bure, ni ubatili, ni kujilisha upepo. Mfumo wa CCM unaompa Rais madaraka yote juu ya nchi ndio uliomuweka hapo alipo. Aringe, ajivune, adharau, aharibu, aongope ni uamuzi wake na wa bosi wake. Hakuna Mtanzania mwingine mwenye sauti juu yake.

Huo ndio msiba mkubwa sana wa taifa hili. Ndio mada ya kujadili. Sio kipara, nasibu, tambo wala nyodo za Makamba. That’s too low. Raise up and fix the systems. Kama hamjajifunza kutoka historia ya nchi bado mnasubiri “masihi” mwingine wa kuongoza nchi hii hakika mtakuwa watu wa maombolezo hadi kiyama.
Mkuu, umezungumza ukweli mchungu. Wengi wanapenda kuyasikia yale tu ambayo wanapenda kuyasikia, kinyume chake huanza kutoa nyongo.
 
Unaelewa maana ya gharama za uendeshaji hapa Nchini?

Zanzibar na Bara ni sawa?

Kwani ni mafuta pekee ndio yako chini huko Zanzibar? Mbona ni vitu karibu vyote ukiacha vyakula bei ni chini na hazijaanza leo?

Au wewe hujawahi nunua au kuagiza mtu akuletee bidhaa kutoka Zanzibar?
Labda hujaelewa my bigger point. Serikali inajaribu kujivua lawama kwenye issue ya mafuta, as if issue kubwa ni Vita ya Ukraine, imekuwaje Zanzibar bei iko chini? Sawa kuna gharama za uendeshaji, ni zipi hizo mpaka tofauti ni 500?
 
Back
Top Bottom