January Makamba: Sisi hatuzalishi mafuta

January Makamba: Sisi hatuzalishi mafuta

Hii nchi sasa hata tufunge na kuomba ni kupoteza muda tu, twende hivyo hivyo
 
Sawa... swali la muhimu ni kwanini Znz bei 2600 na hapa Dar ni 3100? Bila kutueleza hivyo, maana yake kuna kitu cha ziada, maana Zanzibar hawazalishi mafuta
Kumbe zenjibai mafuta ni Tshs 2,600 na dah kweli haya maisha hatari sana
 
Ila kwahii kauli waziri kakosea. Hili sio jibu lakutupa sisi. Inamaana Zanzibar ambako mafuta ni 2600 wao wanazalisha mafuta?
Ametukosea sana waziri.
sidhani hata kama anajuwa bei ipo chini Oman oh sorry Zanzibar
 
Hawa vijana wamemuuzia Samia mbuzi kwenye gunia kiasi kwamba anaamini hadithi zao kuhusu matatizo ya Umeme nchini! Akihojiwa na AZAM TV Rais alisikika akisema matatizo ya umeme yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uchakavu wa miundombinu yake!! Hii hadithi mara ya kwanza tulianza kuisikia kutoka kwa January kama justification ya hoja yao ya kuponda utendaji wa serikali ya Magufuli kuwa mitambo haikuwa inafanyiwa maintenance hivyo uchakavu wa mitambo!!

Samia ameamini uongo huo kwasababu ukienda kwenye budgets za TANESCO za miaka ilyoipita Wakati wa Magufuli na hata kabla ya hapo shirika lilikuwa linatumia fedha nyingi sana kwa matengenezo ya mitambo!! Hivyo hii hoja ya uchakavu wa mitambo inatumuka ili shirika litengewe fedha nyingi za kununua mitambo mipya kwani huko ndio kwenye 10% zao!! It is very unfortunate that she is being easily duped by these inexperienced wannabes.
Unataka tukuchague wewe utazuia kukatika kwa umeme na kushusha bei za mafuta?
 
Makamba kapewa wizara ambayo iko beyond his capacity hiyo wizara inahitaji wajuzi hata kama Hawako bungeni Raisi atafute popote awape ubunge viti maalumu

Makamba yuko zero
Wewe una kapacity gani kumzidi Makamba? Jitokeze hadharani uombe Kazi hiyo afu tuone utakavyoshusha bei ya mafuta na kuzuia kukatika kwa umeme.
 
Sawa... swali la muhimu ni kwanini Znz bei 2600 na hapa Dar ni 3100? Bila kutueleza hivyo, maana yake kuna kitu cha ziada, maana Zanzibar hawazalishi mafuta
Unaelewa maana ya gharama za uendeshaji hapa Nchini?

Zanzibar na Bara ni sawa?

Kwani ni mafuta pekee ndio yako chini huko Zanzibar? Mbona ni vitu karibu vyote ukiacha vyakula bei ni chini na hazijaanza leo?

Au wewe hujawahi nunua au kuagiza mtu akuletee bidhaa kutoka Zanzibar?
 
Ukifanya breakdown ya bei ya mafuta, nusu ya gharama unazolipa ni matozo ya serikali, sijui kwanini hawaoni wao ndio wanaoongezea wananchi mzigo
Hayo matozo yanaenda kuhudumia Msumbiji au?

Serikali haina akili za kindezi kama wewe.
 
Hata sijui tuite kupwaya, au kiuhalisia jamaa sio smart kama anavyolazimisha watu tuamini, hii wizara ni nyeti sana, bila kuwa mtu mwenye upeo, mafuta yatafika elfu 5 kwa lita, japo tayari Kigoma ni elfu 5 kwa sasa.

Kigoma haijafika hiyo bei ya elfu 5
 
Hayo matozo yanaenda kuhudumia Msumbiji au?

Serikali haina akili za kindezi kama

Tunachozalisha ndio kinatakiwa kufidia hayo mafuta tunayonunua kwa kukipandisha bei kwa wazalisha mafuta, hivi ili halijui?
Baadhi ya viongozi wetu wamechoka kufikiri, au hawataki kufikiri, wakiteuliwa wanafanya sherehe, linapokuja suala la kufanya kazi wanaona kama wanatusiadia vile, kwamba ni hisani wanatupatia.
 
Ukimwangalia na kumsikiliza kwa makini, majibu yake yana jeuri fulani na ya kujiamini kupita kiasi.

Hayalingani naa ukubwa wa tatizo, ni majibu ya majivuno ya aina yake. Ni kama anawaza kuwa hizi ni kelele tu na hazimsumbui.

Hana hofu ya kutumbuliwa na hakuna wa kumtumbua.

Ni jeuri ya aliyemweka pale.
100% true, jamaa hana hofu yoyote, hakuna wa kumgusa.
 
Baadhi ya viongozi wetu wamechoka kufikiri, au hawataki kufikiri, wakiteuliwa wanafanya sherehe, linapokuja suala la kufanya kazi wanaona kama wanatusiadia vile, kwamba ni hisani wanatupatia.
Ndio umejibu hoja zangu? Na wewe saidia kufikiri,unataka serikali ifanye nini?
 
Nouma sana, kiukweli hata kama tunasema jiwe alikuwa na chuki ila kwa huyu jamaa hakukosea kumtosa mazima.
Kimsingi Huyo Jamaa ninamchukia sana. Ana udini Mwingi SAna. Angalia Mpaka Sasa limejifanya Liko Kimya Ila likawa linashupalia Kampuni ya Mayanja Construction.
.
Hangaya ana Kituo Cha Tv Huko Kwao Ila halisemi kwamba Huyo Mama Anafanya biashara

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Huyu jamaa sufuri kabisa, majibu mepesi kwenye mada ngumu, kwani hatujui kama hatuzalishi mafuta? We need solutions emediately!!!🙃☹
 
Back
Top Bottom