Japan ni kama wamesahaulika katika Ulimwengu wa Vita na Silaha?

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Hawa jamaa huwaoni wakionesha onesha silaha zao. Huwasikii wakitishiana na mtu au kupiga mkwara.

Lakini rudi miaka ya nyuma katika vita utawasikia kwa uzuri. Nenda kawaulize wachina. Watakuambia. Jamaa kwenye technology ni wazuri sana. Na hawana ubabaishaji. Wanatengeneza vitu vya ukweli na wana akili sana.

Lakini mbona hawasikiki kwenye uwanja wa vita na silaha?ni wameamua wao kufanya kimya kimya au wameamua kukaa pembeni na habari hizo?
 
Yaani unatamani uwasikie kwenye uwanja wa vita🤔😭

Nadhani ifike sehemu watu muwe mnashangaa nchi kusikika kwenye vita na sio kushangaa kutokusikika kwake.

Vita sio suala la kushabikia, it's a tragic thing! Please, God forbid!
 
Sasa hivi wanajenga jeshi lao tena upya ila sio kwa ukubwa.

Wana udhibiti mkubwa wa marekani, I know marekani analinda usalama wake hawezi ruhusu Japan awe tishio kiulinzi usalama wake utakuwa mashakani pia.

Pia ana udhibiti mkubwa wa kimikataba yeye na mwenzake ujerumani.

Hata China anamdhibiti katika ule ukanda wao na bara la Asia wanajeshi zuri Japan ila sio tishio sana kama miaka ya nyuma ambao mpaka usalama wa majirani zake ulikuwa mashakani.

Sasa hivi akijaribu kuleta ubabe wake wa kijinga kwa majirani zake Korea zote mbili na China atapigwa mpaka achakae
 
Yaani unatamani uwasikie kwenye uwanja wa vita🤔😭

Nadhani ifike sehemu watu muwe mnashangaa nchi kusikika kwenye vita na sio kushangaa kutokusikika kwake.

Vita sio suala la kushabikia, it's a tragic thing! Please, God forbid!
Dogo ungeacha watu wenye akili waje kuchangia. Huwezi elewa hapa
 
Baada ya Vita ya pili ya mabepari ( nyie huita ya Dunia) Japan waliachaba na kuwekeza Sana kwenye jeshi na kuwekeza Kwa maendeleo ya watu...ila Huwa najiuliza kwanini USA hakumpiga German na nuclear kaenda Kwa mjapani? Wazungu wabaguzi sanaaaa...
Nenda kasome chanzo cha Japan kupigwa Nuclear. Si suala la ubaguzi labda hujui issue nzima ilikuaje. Kama unakifahamu Kimalkia.

A number of factors contributed to the United States' decision to drop atomic bombs on Japan. One reason was Japan's unwillingness to surrender unconditionally. Japan wanted to keep their emperor and conduct their own war trials and did not want to be occupied by U.S. forces.

By attacking Pearl Harbor Japan believes that it can severely cripple the U.S fleet and buy them time in the Pacific and Southeast Asia. So not only would they be able to launch their attacks without interference from the U.S they would also have time to dig in defensively and consolidate their gains.
 
Baada ya Vita ya pili ya mabepari ( nyie huita ya Dunia) Japan waliachaba na kuwekeza Sana kwenye jeshi na kuwekeza Kwa maendeleo ya watu...ila Huwa najiuliza kwanini USA hakumpiga German na nuclear kaenda Kwa mjapani? Wazungu wabaguzi sanaaaa...
Unafahamu sababu ya marekani kuamua kushiriki moja kwa moja vita vya pili ?
 
Amejikita kwenye kutengeneza na Land Cruiser na IST
 
Habari za kujisafisha tu na historia unasema Japan wali attack naval base USA ,je Hitler aliyekuwa anaua wayahudi Kwa sumu na mjapani nani alitakuwa ku surrender? Na upo vitani una surrender ovyo? Nani alikuwa na impact kati ya Hitler na Japan? Hivi vitabu vya wazungu ni overated na baadaye Hitler aliruhusiwa kwenda Argentina na kufa kifo Cha kawaida kabisaa..
 
Hitler hakuwahi kuvamia Marekani ila Japan alifanya hivyo.
Na ndîo chanzo cha USA kuipiga Japan
 
Baada ya Vita ya pili ya mabepari ( nyie huita ya Dunia) Japan waliachaba na kuwekeza Sana kwenye jeshi na kuwekeza Kwa maendeleo ya watu...ila Huwa najiuliza kwanini USA hakumpiga German na nuclear kaenda Kwa mjapani? Wazungu wabaguzi sanaaaa...
Sio kwamba vita ilikua imeisha na Hitler hata haikujulikana kama aliuawa kwenye lile shambulio la Ikulu au alitoroka muda mfupi kabla ya shambulio!
 
Hitler alivamia Marekani? Alishambulia Marekani? Mbona hupendi kujisomea unaandika kwa hisia na wakati kila kitu kipo wazi dunia ya sasa? Ingia google search for infos siyo kucheck Porno tu dogo. Ndo maana unachanganyikiwa kwa vitu vidogo sana ambavyo hutakiwi kutumia nguvu.
 
Mkuu kazi uliyotupa ni ngumu xnaa
Mara tuende miaka ya nyuma (time machine hatuna)
Mara tukamuulize mchina ,hiv kwel hata ww waeza mfata mchina umuulize jinsi walivyopigwa ?
 
Wazeee ni wengi kuliko vijana, hakuna anayetaka kuzaa na hawapendi wahamiaji. Hakuna wapiganaji, na waliopo ni kucheza games na kuendesha Subaru Impreza, Supra GR au Nissan GT-R tu.

Kwa kifupi ni generation ya bata
 
Dogo unafahamu ushenzi wa Japan Asia huyo mjerumani hakufikia level ya wajapan uliza kwa nini wachina,wakorea na sehemu kubwa ya Asia hawawapendi wajapan wana historia chafu.
 
Baada ya Vita ya pili ya mabepari ( nyie huita ya Dunia) Japan waliachaba na kuwekeza Sana kwenye jeshi na kuwekeza Kwa maendeleo ya watu...ila Huwa najiuliza kwanini USA hakumpiga German na nuclear kaenda Kwa mjapani? Wazungu wabaguzi sanaaaa...
Wakati USA anampiga Japan…..German na Italy walikuwa tayari wamepigwa na kuchakazwa….techinically vita ilikuwa imeisha ulaya…
Ila japan alikuwa bado anakipiga na alikuwa tishio kwa Marekani, kama utakumbuka Japan alishapiga USA kwenye visiwa vyake na maeneo makubwa ya bahari yalikuwa yanathibitiwa na Japan….
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…