Japan: Waziri Mkuu wa zamani, Shinzo Abe afariki dunia baada ya kushambuliwa kwa risasi

Japan: Waziri Mkuu wa zamani, Shinzo Abe afariki dunia baada ya kushambuliwa kwa risasi

Btw huyo Mzee alipo stahafu ange pumzika tu , unaweza kukuta serikali iliyopo madarakani ndio imeamua kumtoa kafara Kwa sababu Bado alikuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini kwake Wakaona kuwa anaweza kuleta mageuzi
 
Kuna Bwn Mmoja aliwahi mvamia mzee Mwinyi akampiga makofi. Mzee mwinyi kwa uungwa akamsamehe ila sheria ilichukua mkondo wake akafungwa nadhani alimaliza kifungo chake. Nakumbuka chanzo Mzee Mwinyi alihimiza masuala ya uzazi wa mpango.

Kuna watu wana depression.
Yule msela,alikufa soon baada yakutoka jela,ukute wazee wa makumbusho walilala nae mbele

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
.
Screenshot_20220708-140145.jpg
 
Dah Shinzo yamemkuta, mpigaji ni sniper, amepiga kwenye moyo kabisa.

Wenzetu hasa nchi kama Japan, ukishastaafu unakuwa mtu wa kawaida tu.

Ukiwa PM unakuwa mtumishi tu, na ukistaafu unakuwa EX-mstaafu.
 
Bunduki iliyotumika ni ya kienyeji, katika shambulizi la umbali mfupi, jambo linaloashiria kuwa 'motive' ni yake binafsi [mshambuliaji].
 
Haina maana kuanzisha uzi ili kukaba nafasi kama huna taarifa kamili.. Atakuja mwingjne mwenye taarifa kamili na zinazoelezeka na uzi wako utaunganishwa huko kama reply ya kawaida
Kweli kabisa. Bora ifanyike ivyo
 
wale wa kwa lisu waliishia kupalaza paraza tu gari ogapa Sana sniper anasimama mbele au nyuma hiyo 💯 itaondoka na wewe
 
Mtu anayeshukiwa kumpiga risasi Waziri Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe ametambuliwa na vyombo vya habari vya Japan kama Tetsuya Yamagami mwenye umri wa miaka 41, mkazi wa mji wa Nara.

Anaripotiwa kuwa mwanajeshi wa zamani wa Kikosi cha Kujilinda cha Majini cha Japan, jeshi la wanamaji la nchi hiyo, lakini wizara ya ulinzi haijathibitisha rasmi hili.

Mtangazaji wa shirika la serikali la Japan NHK aliripoti kuhusu Yamagami akiwaambia polisi kuwa ‘’hajaridhika na Abe na alitaka kumuua.’’

Mshukiwa sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi.

Walioshuhudia walisema walimwona mtu akiwa amebeba kile walichotaja kuwa ni bunduki kubwa na kumfyatulia risasi Abe mara mbili kwa nyuma.

Picha zilizopigwa wakati mshukiwa anakamatwa zinaonyesha kile kinachoonekana kama silaha iliyoboreshwa.

Haijulikani ni vipi mpiga risasi huyo alikuja kujua kuhusu kuhudhuria kwa Abe kwenye kampeni mapema, kwani ziara hiyo ilithibitishwa jana usiku.
Chanzo;DW
Soma zaidi:

Shinzo Abe: Waziri Mkuu wa zamani wa Japan auawa kwa kupigwa risasi katika hafla ya kampeni
 
Back
Top Bottom