Japo anaonekana mtu wa kawaida tu ndani ya CCM, Humphrey Polepole sio mtu wa kawaida!, He is extra ordinary very powerful!

Japo anaonekana mtu wa kawaida tu ndani ya CCM, Humphrey Polepole sio mtu wa kawaida!, He is extra ordinary very powerful!

Siku za mbele zenyewe ndio hizi zimeanza... subiri jina kwenye cabinet...
P
Hahhaaaaa! Mkuu, mimi nimekwishakuwa Muumini wa UNABII wako kwa takriban miaka mitatu sasa.

Hao wengine achana nao. Nabii hakubaliki kwao, ila, sie tushakuelewa kitambo

OMBI; NAKUSIHI SANA UMTABIRIE MEMA BWANA TuntemekeSanga

Yuko chini ya Miguu yako. Na Mungu akubariki sana. [emoji41][emoji41]
 
Huwa namuelewa sana Polepole , Jamaa anajua sana kupanga hoja na kuzipangua

Anajua mikakati yote ,

Nape alikuwa anajua matusi ,

Unahitaji kina nape 10 umpate polepole mmoja
Naunga mkono jamaa ni Strategist mzuri mno yani hakuna kama polepole anavyo-manage utasema yeye ndo mwenyekiti wa chama.
nimeanza kumfatilia 2014 kuna hoja fulani alizipangaga zilinivutiaga sana nikajisemea katika watu wenye akili iliyotulia huyu jamaa.
 
Itapendeza sana akiwa WAZIRI wa Habari, michezo na utamaduni, namuombea Mungu afanikiwe kwani anaweza na anastahili sana kupewa dhamana ya uwaziri, namkubali huyo ni "JEMBE ULAYA"
 
Uongeaji wake unafanana na wa ule wa Baba wa Taifa.
Lolote lawezekana 2025-2035 kama Rais au Waziri Mkuu.
Kwa sasa anafaa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.
 
Paskali uko sahihi sana na kweli huyo Polepole ana nguvu sana ndani ya CCM. Sababu hasa ya Polepole kuwa na nguvu ndani ya CCM

1. Polepole ni mtu aliyesoma mambo ya ccm na kuyakariri vyema hasa sheria na miongozo ya chama.

2. Polepole hakuwa sehemu ya wanachama wezi kwani hakuwa kuwa kwenye sehemu ya ulaji ndani ya chama au serikali kabla ya Magufuli, hivyo kuwa katika kundi la wanaccm wachache wasio na kashfa.

Kwa sababu hizi hapo juu, Polepole ndio msiri na mshauri mkubwa wa CCM kuliko mwanaCCM yoyote. Hapo ndio nguvu zote za Polepole zilipo.
Naunga mkono hoja.
P
 
Kuna siku nilimsikia clouds kama wiki na nusu iliyopita,nikajiridhisha huyu mtu ana kitu kizito kichwani.

Namna alivyokuwa anaulizwa maswali na kujibu,namna anavyopangilia majibu na kuweka akiba ya maneno,nikajisemea hata labda alijua anakwenda kuulizwa kitu gani kabla hajatoka kwake asubuhi.

Tumezoea kumuita chakubanga,kwa maana ya mpiga domo kwa kazi hiyo,ila kosa kubwa tunalofanya kama watu wa upande B,ni kumchukulia kwa urahisi rahisi tu,mtu kama pole pole.
Naunga mkono hoja.
P
 
"CCM ndio chama tawala na kwa Tanzania, tukubali tukatae, CCM ni chama dola.

Tunapoelekea uchaguzi Mkuu wa rais na wabunge October 25, mgombea akiishapitishwa kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM, then huyo ndio tayari ni mshindi, zoezi la uchaguzi ni kukamilisha tuu taratibu za uchaguzi ili tuu kuhalalisha."
naunga mkono hoja!.
P
 
Uko sahihi kwa asilimia 200

Polepole ni strategist yaani anafahamu kupanga mikakati kitaalam.

Pili, Polepole ni coordinator mzuri tu anafahamu namna ya kuunganisha mpango, sera na mikakati.

Tatu, Polepole ni good communicator yaani anafahamu ni vipi azungumze na hadhira kulingana na aina ya hadhira hiyo.

Hivi vitu baadhi alikuwa navyo Nape Nnauye lakini akavurugwa kidogo kutokana na kukosa experience yaani uzoefu.

Naomba niishie hapo.
Naunga mkono hoja.
P
 
Pascal Mayalla hata usipoteuliwa kwenye hii serikali mpaka unaingia kaburini kupumzika fahamu kwamba Mungu alikupa kitu extra sana ambacho watu wengi hawana na wengine walitamani kuwa nacho.

si kila alieletwa duniani alipaswa kuwa mchungaji au padri wapo ambao hawana hizo title lakini ni zaidi ya mapadri na wachungaji,na si kila muandishi aina yako lazima apewe uongozi unaweza ukabaki hapo hapo na ukawa zaidi ya hizo nafasi watu wanadhani unazitafuta.

hakuna jambo jema na zuri chini ya jua kama kutumia kipaji na uwezo Mungu aliokupa kwa jamii iliyokuzunguka,pascal wewe ni zaidi ya unavyojiona yawezekana watayasema haya ukishatuaga ukiwa umelala pale kwenye nyumba yako ya milele,lakini mimi nakwambia angali u hai pascal you're blessed endelea hapo hapo.Hamna jipya chini ya jua kama ni uongozi ulionao wakuwa baba tu unakutosha mengine achia wananchi,simamia unachokiamini.
 
Hata Mimi kitambo tu hata kabla hajaingia kwenye CCM ,Ilikuwa channel Ten, alialikwa na Msigwa ,aisee Msigwa alitaka kukimbia

Pole pole ni Nyoko kwenye Kupanga na kupangua hoja ,anajua nini aongee na nini asiongee

Huyo Mbwa hafai kabisa , ni kati ya watu wachache niliowashuhudia wanaojua kujenga na kupanga hoja tena kwa unyenyekevu


Lisu anajua kupanga hoja na kupangua ,shida hana unyenyekevu


Polepole nashangaaga wanasema eti hajavaa viatu vya nape

Polepole ni namba nyingine kabisa ile, Angalia jinsi alivyokuja kupangua hoja ya Trillion 1.5 kwa ufasaha

Nape hawezi kile kitu .

Nape alikuwa bingwa wa siasa za majitaka, Nape ndio alidai lowassa kainunua Chadema Billion 5
Naunga mkono hoja.
P
 
Back
Top Bottom