Japo sio lazima kuhoji kila kitu kwa kuuliza maswali lakini mtu mwenye akili zake timamu ni lazima ajiulize. Ukimya wetu, msitufanye mazuzu kuna...

Nyepesi zipo nyingi sana!

R.I.P kwandikwa, survive well Dr.Kakurwa
 
Pascal Mayalla, je ukipata uteuzi wowote, utaendelea kuhoji, au utakaa mezani na kula kwa nidhamu bila kupayukapayuka?
Hahah kasema ameshatuma maombi mengi ya kuomba mahojiano,anajibiwi asubiri Kuna folen.
Foleni ipi hiyo?🤔
Au ruti za Safari uguibuni ndo folen yenyewe?
Kupatwa kwa Tanzania.
 
Tutegemee nini ndugu mwandishi
Tutegemee umaskini endelevu.
Na hata akija mwenye maono ya kuikomboa nchi atapitia wakati mgumu kwani atakuwa na kazi kubwa sana ya kureform sector nyingi kwenye nchi maana almost kila sector ipi corrupted hakuna yenye afadhali.
Mwisho tutegemee kupitia kipindi cha mpito cha ku-expiriance taifa la ovyo hasa vijana mpka pale Tutakapo amua kubadilika sisi kisha kulibadilisha taifa.
 
Hata Jack Nicholson kwenye filamu ya "A Few Good Men" alimwambia Tom Cruise kwamba, You can't handle the truth" ingawa alifahamu juu ya kifo cha kijana Santiago.

Katika filamu hiyo kijana private Santiago aliuawa na wanafunzi wenzie akiwa mafunzoni Guantamano na maofisa waandamizi chini ya kanali Nathan Jessep (Jack Nicholson) ambae baada ya Santiago kuomba uhamisho yeye akaamuru kijana huyo apewe mafunzo ya code red yaani mafunzo makali ya kumwezesha mtu kufa.

Na baadae wavu ulipoanza kusogea washiriki wote walianza kutajana na baadae kanali Nathan alipatikana na hatia na kwenda jela.
 
Sasa hivi Princess Kate amepotea.
Waandishi wa habari UK wanasema wanamechishwa kabisa na hizi speculation. Wanataka Palace itangaze kitu definitive.
Sasa,nani unadhani atakuambia ukweli?
Umma bado wasimama na vyombo vya habari vitatu ambavyo ni Reuters, AP na PA, hivi si vyombo vya habari vya kupika majungu.

Vyombo hivi mara tu picha ilipowekwa hewani wao wakazikataa na kutoa tahadhari kwamba picha imechakachuliwa na hawatoiweka katika kurasa zao.

Hivyo ni jukumu la Buckingham Palace kuhakikisha picha ile ilotolewasiku ile ni picha halisi.
 
Na idadi ya watu ikifika milioni 140 tutageuka kuwa Haiti.
 
Kujua ukweli kuna faida nyingi. Au hujui umuhimu wa historia?
 
Kuna mtu alisikiliza hotuba ya Makamba alipokuwa anaongea na wana diaspora Italy? Makamba alisema wakati Magufuli akiwa rais, kuna kundi la viongozi wa CCM ambao walikuwa wanadharau ofisi ya Samia na Makamba, na walikuwa hawataki hata kuongea nao. Pia akasema mara baada ya Magufuli kufariki, hao watu walikuwa wanasema Samia hawezi kuongoza nchi. Akaendelea kuwa Samia baada ya kuapishwa, hakulipa kisasi bali aliwateua kwenye nafasi mbalimbali. Hao watu ndiyo walioficha kifo ambacho Paskal anahoji hapa. Wanajulikana. Ila hofu yao ilikuwa na mashiko. Nchi imeshamshinda.
 
Mkuu Paskali,

Wajitahidi kutaka kufanya kazi yako ya uandishi wa habari za kiuchunguzi ila umekosa nyenzo sahihi.

Pia hata huyo mwenzio wa huko Ughaibuni nae amekosa nyenzo muhimu kutengeneza "documentary" ya kilichotokea ingawa ni miaka yakaribia mitatu sasa.

Lakini nakuhakikishia ukiweza kutengeneza Documentary ya juu ya tukio lile kwa ufanisi huku ukishirikiana na mwenzio wa huko ng'ambo, basi mtakuwa mmefanya yasowezekana.

Isitoshe hapa hueleweki wataka kufanya interviwe kuhusu progress ya raisi wa sasa na kujua atakidhi vipi matarajio ya watanzania?

Au wataka kufanya mahojiano yanohusu tukio lile?

Kama ni kuhusu tukio lile nakuhakikishia hutapata nafasi na utawekwa chini huko kwenye orodha.

Njia sahihi andaa documentary na ingia kazini provided uko cleared na mazee.

Jikite kwenye You Tube, huko ndiko kwenye pesa sasa hivi.
 
HAPANA KUBWA.
 
Yeah ukisoma kwenye Uzi wa Yoga yote wameelezewa
 
Kwa bandiko kama hili mkuu p, naomba jitahidi kuwa nao makini. Maana unaweza kuwa na maadui wengi huko kuliko huku. Kwa mtu mwenye busara kuambiwa ukweli na mtu mwenye nia njema ni furaha kwake maana anapata nafasi ya kujirekebisha. Lakini kwa mtu ambaye ni kinyume chake ukimwambia ukweli ANAKUFANYA KUWA ADUI YAKE.
 
Mkuu Mayalla kulikoni?
Naona leo umeongea kwa uzalendo sana!
Huyu ndo Mayalla tunayemfahamu.
Siyo yule wa siku za hapo katikati aliyetaka kugeuka "chawa"!
Ahsante sana kwa bandiko hili Mkuu.
 
kaka paskali kama unataka mabadiliko kawahoji kule kule juu, wewe uliona wapi wake wa maraisi wanalipwa mafao hawa watu wana uhuru wa manyani wanafanya wanachotaka, wao ndio sheria sheria ndio wao tuliwapenda wenyewe wacha tuendelee kuisoma namba, wewe uliona wapi mtu hupati haki mahakamani hupati haki ngazi yoyote ya mkoa au wilaya hadi ngazi ya kijiji halafu tatizo lako anakuja kulitatua mwenezi wa chama tena kwenye mkutano wa hadhara nchi ya maajabu hii, tuwavumilie tu ni ndugu zetu waliopofuka na kupotoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…