Japo sio lazima kuhoji kila kitu kwa kuuliza maswali lakini mtu mwenye akili zake timamu ni lazima ajiulize. Ukimya wetu, msitufanye mazuzu kuna...

Na wengine wakanyatisha eti “Kuna watu walitaka VP asiwe predaa na walitaka kuhujumu katiba” na wengine wakasema eti “ndani ya hizo siku 5 kuna wahuni walichota fedha chumba kikuu cha fedha” na hii baada ya kuwa presdaa aliagiza ukaguzi maalum kwa miezi mitatu nyuma
Nyepesi zipo nyingi sana!

R.I.P kwandikwa, survive well Dr.Kakurwa
 
Pascal Mayalla, je ukipata uteuzi wowote, utaendelea kuhoji, au utakaa mezani na kula kwa nidhamu bila kupayukapayuka?
Hahah kasema ameshatuma maombi mengi ya kuomba mahojiano,anajibiwi asubiri Kuna folen.
Foleni ipi hiyo?🤔
Au ruti za Safari uguibuni ndo folen yenyewe?
Kupatwa kwa Tanzania.
 
Tutegemee nini ndugu mwandishi
Tutegemee umaskini endelevu.
Na hata akija mwenye maono ya kuikomboa nchi atapitia wakati mgumu kwani atakuwa na kazi kubwa sana ya kureform sector nyingi kwenye nchi maana almost kila sector ipi corrupted hakuna yenye afadhali.
Mwisho tutegemee kupitia kipindi cha mpito cha ku-expiriance taifa la ovyo hasa vijana mpka pale Tutakapo amua kubadilika sisi kisha kulibadilisha taifa.
 
Paskali, najua wauliza uli ujuzwe ukweli kama mwandishi wa habari.

Kuna tetesi tena kuwa tukio la mitambo kuzima actually ilikuwa tarehe 9 Machi, tarehe 12 kuwa confirmed na tarehe 17 kutangazwa.
Nchini kuna wafuatiliaji wa makini wa yale tanayotokea.
Lakini swali ni moja, je ukifahamu ukweli huo utaufanyia nini?

Kuna filamu moja iliyomuonyesha mwandishi wa habari kule Marekani akitafuta habari fulani ya kijasusi, iliyo leak magazetini.
Mwandishi alienda kwa afisa mwandamizi , juu kabisa serikalini, na akamwambia:
"I want to know the truth, and the public wants to know the truth"
Yule afisa mwandamizi akamjibu kwa mkato " You cant handle the truth"
Jamaa ikabidi aingie mitini tu.
Hata Jack Nicholson kwenye filamu ya "A Few Good Men" alimwambia Tom Cruise kwamba, You can't handle the truth" ingawa alifahamu juu ya kifo cha kijana Santiago.

Katika filamu hiyo kijana private Santiago aliuawa na wanafunzi wenzie akiwa mafunzoni Guantamano na maofisa waandamizi chini ya kanali Nathan Jessep (Jack Nicholson) ambae baada ya Santiago kuomba uhamisho yeye akaamuru kijana huyo apewe mafunzo ya code red yaani mafunzo makali ya kumwezesha mtu kufa.

Na baadae wavu ulipoanza kusogea washiriki wote walianza kutajana na baadae kanali Nathan alipatikana na hatia na kwenda jela.
 
Sasa hivi Princess Kate amepotea.
Waandishi wa habari UK wanasema wanamechishwa kabisa na hizi speculation. Wanataka Palace itangaze kitu definitive.
Sasa,nani unadhani atakuambia ukweli?
Umma bado wasimama na vyombo vya habari vitatu ambavyo ni Reuters, AP na PA, hivi si vyombo vya habari vya kupika majungu.

Vyombo hivi mara tu picha ilipowekwa hewani wao wakazikataa na kutoa tahadhari kwamba picha imechakachuliwa na hawatoiweka katika kurasa zao.

Hivyo ni jukumu la Buckingham Palace kuhakikisha picha ile ilotolewasiku ile ni picha halisi.
 
Tutegemee umaskini endelevu.
Na hata akija mwenye maono ya kuikomboa nchi atapitia wakati mgumu kwani atakuwa na kazi kubwa sana ya kureform sector nyingi kwenye nchi maana almost kila sector ipi corrupted hakuna yenye afadhali.
Mwisho tutegemee kupitia kipindi cha mpito cha ku-expiriance taifa la ovyo hasa vijana mpka pale Tutakapo amua kubadilika sisi kisha kulibadilisha taifa.
Na idadi ya watu ikifika milioni 140 tutageuka kuwa Haiti.
 
Paskali, najua wauliza uli ujuzwe ukweli kama mwandishi wa habari.

Kuna tetesi tena kuwa tukio la mitambo kuzima actually ilikuwa tarehe 9 Machi, tarehe 12 kuwa confirmed na tarehe 17 kutangazwa.
Nchini kuna wafuatiliaji wa makini wa yale tanayotokea.
Lakini swali ni moja, je ukifahamu ukweli huo utaufanyia nini?

Kuna filamu moja iliyomuonyesha mwandishi wa habari kule Marekani akitafuta habari fulani ya kijasusi, iliyo leak magazetini.
Mwandishi alienda kwa afisa mwandamizi , juu kabisa serikalini, na akamwambia:
"I want to know the truth, and the public wants to know the truth"
Yule afisa mwandamizi akamjibu kwa mkato " You cant handle the truth"
Jamaa ikabidi aingie mitini tu.
Kujua ukweli kuna faida nyingi. Au hujui umuhimu wa historia?
 
Ni kawaida sana hii Pascal.
Je, unafahamu hata Siku ya Malkia kufa hupangwa?
Na siku ikifika Huchomwa sindano ilu afe bila maumivu?
Na akifa huwez kutangaza siku hiyo hiyo mpaka yafanyike maandalizi?

Kilichonishangaza mimi ni Ile siku aliyokufa Baba yetu wa Pili kazikwa siku Mbili baada ya kifo chake ila Kila kitu kilikuwa Tayari kimeandaliwa na bajeti na hata Vikao vyote vimekaa.

Hii inadhihirisha huenda hakuwa amefariki siku tuliyotangaziwa.
Kuna mtu alisikiliza hotuba ya Makamba alipokuwa anaongea na wana diaspora Italy? Makamba alisema wakati Magufuli akiwa rais, kuna kundi la viongozi wa CCM ambao walikuwa wanadharau ofisi ya Samia na Makamba, na walikuwa hawataki hata kuongea nao. Pia akasema mara baada ya Magufuli kufariki, hao watu walikuwa wanasema Samia hawezi kuongoza nchi. Akaendelea kuwa Samia baada ya kuapishwa, hakulipa kisasi bali aliwateua kwenye nafasi mbalimbali. Hao watu ndiyo walioficha kifo ambacho Paskal anahoji hapa. Wanajulikana. Ila hofu yao ilikuwa na mashiko. Nchi imeshamshinda.
 
Wanabodi,

Hapa duniani kuna fani mbalimbali za shughuli, na shughuli kuu ya kwanza duniani baada ya Mungu kumuumba binadamu, ilikuwa ni shughuli ya kutengeneza watoto au kuumba viumbe. Kwa vile Adamu na Hawa au Adamu na Eva, wao waliumbwa na Mungu mwenyewe, hivyo shughuli yao kuu ya kwanza ilikuwa ni kutengeneza watoto ili kujenga familia, kwa kuumba viumbe wengine!

Ile shughuli ya kutengeneza watoto ili kujenga familia, au uumbaji wa viumbe vipya, ndio shughuli kuu ya kwanza ya binadamu hapa duniani!, (the oldest professional) na viumbe wote, duniani kabla ya kuzaliwa ni lazima kwanza shughuli hiyo ifanyike, ndipo kiumbe kiumbwe, na ndipo kizaliwe, hivyo japo wengi wanahesabu siku ya kuzaliwa ndio siku yao ya kwanza duniani na watu wanasherehekea siku ya kuzaliwa, yaani birthday.

Hiyo siku ya kuzaliwa, ni siku tuu ya kuingia duniani, lakini sio siku ya kuumbwa!, siku unazaliwa, ujue uliumbwa miezi 9 nyuma!, kwa vile hata wazazi waliokuumba, hata mama aliyekubeba tumboni mwake, anakuwa hana uhakika halisi ni siku gani kiumbe kipya kimeumbika tumboni mwake, kwasababu anayeumba sio binadamu ni Mungu!, jukumu la binadamu ni kufanya tuu tendo la kuumba, lakini muumbani ni Mungu!. Nimeileta hadithi hii ya uumbaji ili kuelezea ndio shughuli kuu ya kwanza duniani.

Baada ya uumbaji shughuli kuu ya pili ni ujenzi wa familia, ulezi, makuzi na shughuli mbalimbali za kuendesha maisha na humu ndimo mwisho wa siku kunakuja kuibuka fani mbalimbali, wa mama wa nyumbani, wapishi, wasaidizi wa kazi, wake, vijakazi, waalimu, madaktari, madereva, wajenzi, wahubiri, matatibu, hata wanga, wachawi na washirikina, zote ni fani.

Kila fani, ina misingi yake mikuu, msingi mkuu wa fani ya ualimu ni kufundisha wengine, msingi mkuu wa fani ya udaktari ni kutibu na kuokoa maisha, msingi mkuu wa fani ya uongozi ni kuwaongoza wengine, msingi mkuu wa fani ya uandishi wa habari ni kuripoti, kueleza ukweli, ili kuueleza huo ukweli, mwandishi yeyote mzuri wa habari, ni lazima awe na uwezo wa kuhoji, mimi kwa sasa nimekuwa ni mtu mzima, lakini enzi zangu za ujana, nikiwa newsroom enzi zangu za kipindi changu cha Kiti Moto, kuna watu walikuwa wakialikwa, wanakimbia!, kilichokuwa kinawafanya wakimbie si uoga tuu wa kuogopa kuhojiwa maswali magumu.

Mahojiano yangu ya mwisho ya maswali magumu, ni yale niliyoyafanya ile siku ya tarehe 4 November, pale mahali, ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kualikwa pale, na ndio ikawa mara yangu ya mwisho, kilichobakia ni barua zangu tuu za kuomba mahojiano ambazo sikuwahi kujibiwa mpaka wengine wameitwa walikoitwa, na mimi nikiendelea kuziandika tuu kuomba mahojiano, na kuendelea kusubiri na kusubiri, angalau msaidizi wa sasa she is very gentle kwa kukueleza lazima uwe na subra sana maana barua za maombi ya mahojiano ni nyingi, foleni ni ndefu ila tunaendelea kusubiria, na hata tukipata fursa, siku hizi, tumeishajizeekea hatuna tena yale maswali magumu ya type ya kiti moto!.

Pamoja na jukumu kuu la mwandishi wa habari ni kuhoji na kuripoti ukweli, lakini sio lazima kila ukweli uripotiwe, kabla ya mwandishi wa habari kuripoti chochote, anapaswa afanye tathmini ya kitu kinachoitwa kwa Kiingereza Objectivity, yaani huu ukweli ninaotaka kuuripoti, ukijulikana, utaidaidia jamii?, hivyo ukikutana na tukio la ukweli kabisa, lakini ukaona ukweli huo ukijulikana, hautaisaidia jamii, wewe kama mwandishi makini, unapaswa kuuhifadhi ukweli huo na kutouripoti, ukweli ambao hautasaidia kitu jamii husika. Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

Tarehe, 12 mwezi March, mwaka 2021, mimi nikiwa ni mshitiri wa akaunti ya mtandao wa YouTube wa mwandishi mmoja Mtanzania anayeishi ughaibuni, alipandisha kwenye mtandao wake, taarifa ya kutokea kifo cha kiongozi fulani wa nchi fulani, lakini viongozi wa nchi hiyo, wameamua kufanya siri!.

Mwandishi huyo, alisema, yeye amepenyezewa taarifa hiyo na jamaa zake ambao ni watu wa "sehemu", na wameamua kumpenyezea yeye, kwa vile na yeye alikuwa ni mtu wa "sehemu", kabla ya kuikimbia nchi na kutokomea ughaibuni, baada ya kushikwa sikio, na watu wenzake wa "sehemu" kuwa wanaitafuta roho yake, ndipo akaamua kukimbilia ughaubuni kuinusuru roho yake ndio maana mpaka sasa bado yupo, vinginevyo angeisha kuwa mavumbi siku nyingi!.

Taarifa ya msiba huo ikasababisha sintofahamu kubwa huku nyumbani!, mara Balozi wetu wa Zimbabwe ambaye na yeye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa ile IOdara ya "sehemu", akatoa taarifa kukanusha!, mara Waziri Mkuu wa JMT akatoa taarifaa, jamaa yuko ana chapa kazi mnataka aende Kariakoo!, mara VP wa nchi hiyo akjatumwa Tanga kwenda kumwakilisha bosi wake kwenye tukio!.

Kwa vile nchi yetu ni nchi ya JMT yenye pande mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, wenzetu kule Zanzibar, toka baada ya kuipokea taarifa hiyo Machi 12, wao walisitisha shughuli zote na ratiba zote za kiserikali za shamra shamra na kufuta ziara zote, huki sisi huku bara tukiendelea as if nothing happened!.

Na baada ya siku 5 tangu nilipopokea taarifa hii, ndipo Taifa tungatangaziwa rasmi kuhusu msiba huo mzito!. Taarifa hiyo iliishitusitusha dunia na Watanzania wote kuhusu msiba wa mkuu wa nchi, laki kwa wale ambao tulipokea taarifa ya msiba huu siku 5 kabla, sio kuwa hatukushitishwa na taarifa rasmi ya msiba, bali sasa tulisumbuliwa na shauku ya kuhoji ukweli ni upi kuhusu msiba huu, ni ile taarifa ya siku tsano zilizopita au taarifa rasmi ndio ukweli wenyewe?, Watanzania wana haki ya kuelezwa ukweli wa nini haswa kilitokea kama ukweli ukweli huo unaelezeka, ila kama ukweli huo haulezeki, then Watanzania bado tuna haki ya kuelezwa kuwa ukweli tarehe halisi ya tukio lile haielezeki ila ile Machi 17 ndio tuichukulie ndio tarehe rasmi ya kutangazwa tukio, kwasababu hata tarehe 25 Desemba, inayatangazwa ndio siku ya kuzaliwa Masiha, ni siku tuu iliyoteuliwa, lakini siku rasmi ya kuzaliwa Masiha, sio hiyo tarehe 25 Desemba, bali ndio siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake.

Familia nyingi za Kiafrika, haswa sisi watu wa Kanda ya Ziwa, tukilewa huwa tuna kelele sana, hivyo ndani ya familia nyingi, huwa tunashuhudia kuna siku baba amepata kinywaji na kikamkolea, anarudi amelewa, anapgizana kelele na Maza, na kuna sometimes Maza anatembezewa kichapo, watoto mnajua, lakini hamuwezi kuuliza, wala kutangaza, inabaki ni siri za familia, ila watoto wa kizazi cha kisasa kizazi cha kuhoji, siku zote huwa wana dukuduku, kimetokea nini hadi Maza atembelee kisago?!.

Sasa kwa tukio kubwa kama lile la tarehe 17 Machi, kama ni kweli lilitokea tarehe 12 Machi, na watu wakakaa na mtu wao siku 5 nzima ndipo waje watutangazie, dukuduku ya kuhoji, walikuwa wanafanya nae nini siku zote 5?. Bado naendelea kusisitiza kuzingatia issues za morality kwenye kuusema ukweli Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

Kutokana na kutoelezwa ukweli ni nini haswa kilitokea, wazushi nao wanapenyezea hapo hapo agenda zao, eti baada ya kutokea kilichotokea ile tarehe 12, haikutangazwa kwasababu kuna kiongozi mmoja wa kidini wa imani fulani, aliwahakikishia anaweza kumrejeshea uhai wake, na akakubaliwa, hivyo hizo siku tano toka tarehe 12 Machi tukio lilipotokea, hadi tarehe 17, lilipotangazwa, juhudi za kumpambania maisha yake, zilikuwa zinaendelea, na baada ya juhudi zote kushindikana ndipo sasa tukatangaziwa rasmi!.

Sisi kizazi cha kuhoji, bado tuna dukuduku, kwa ule msemo wa sterling hauwawi, kama sterling wa filamu alikuwa amelala toka Machi 12, mpaka tulipotangaziwa ile Machi 17, who was running the show?, ni nani walimweleza Waziri Mkuu aseme Mwamba anachapa kazi?!, ni nani walimpangia VP safari ya Tanga ili kumzuga, as if nothing happened, wakati wenzetu upande wa pili wa Zanzibar wao waliahirisha kila kitu?!.

Hitimisho
Japo sio lazima kuhoji kila kitu kwa kuuliza maswali, kakini likitokea jambo lisilo la kawaida, mtu yeyote mwenye akili zake timamu, sio lazima ahoji au kuuliza, lakini ni zazima ajiulize ilikuwaje na ilitokeaje tokeaje?!. Huu ukimya wetu, wa ku observe things, to note things bila kuongea, au bila kuuliza, naomba kusitafririewa kuwa ni mazuzu!, kunapotokea vitu ambavyo Watanzania wanapaswa kuambiwa ukweli, Watanzania tuambiwe ukweli bila kujali ukweli huo ni mtamu au mchungu kiasi gani, ukimya wa Watanzania kutohoji hoji kila kitu, kusitafsiriwe kuwa Watanzania ni mazuzu, kunapotokea jambo, tuelezwe tuu ukweli, tutaelewa. Natoa wito kwa viongozi wetu, mnapoona watu hawahoji hoji sana kama enzi zile, mjue ni wameamua kutohoji hoji sana, na sio kuwa hawaoni, au hawajui, hivyo viongozi wetu msituchulie poa, mkatuona kama mazuzu!, Watanzania sio mazuzu!, kuna siku itafika, ukweli bayana utajulikana, hawa watu watawaonaje?.

Ukweli Usemwe

Paskali
Mkuu Paskali,

Wajitahidi kutaka kufanya kazi yako ya uandishi wa habari za kiuchunguzi ila umekosa nyenzo sahihi.

Pia hata huyo mwenzio wa huko Ughaibuni nae amekosa nyenzo muhimu kutengeneza "documentary" ya kilichotokea ingawa ni miaka yakaribia mitatu sasa.

Lakini nakuhakikishia ukiweza kutengeneza Documentary ya juu ya tukio lile kwa ufanisi huku ukishirikiana na mwenzio wa huko ng'ambo, basi mtakuwa mmefanya yasowezekana.

Isitoshe hapa hueleweki wataka kufanya interviwe kuhusu progress ya raisi wa sasa na kujua atakidhi vipi matarajio ya watanzania?

Au wataka kufanya mahojiano yanohusu tukio lile?

Kama ni kuhusu tukio lile nakuhakikishia hutapata nafasi na utawekwa chini huko kwenye orodha.

Njia sahihi andaa documentary na ingia kazini provided uko cleared na mazee.

Jikite kwenye You Tube, huko ndiko kwenye pesa sasa hivi.
 
HAPANA KUBWA.
Nimekusoma kote ila nimeona nibakie kule kwenye hadithi, hasa hasa pale uliposema binadamu hatuumbi, kazi ya uumbaji ni ya Mungu, kwangu nimeona hapo ndipo penye jambo.

Nionavyo mimi, binadamu tunaumba, lakini uumbaji wetu ni tofauti na ule uumbaji wa Mungu, Mungu alimuumba Adamu kwa namna yake bila kukutana mtu mume na mtu mke, kisha tena akaenda kumuumba Eva toka kwenye ubavu wa Adamu, bila kukutana mtu mme na mtu mke.

Baada ya hapo akaenda kumuumba Yesu Kristu, bila kukutana mtu mume na mtu mke, mimba ya Yesu Kristu iliingia kwa uwezo wa roho mtakatifu, baada ya Mariamu kupewa ujumbe na malaika atabeba mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu.

Sasa ukiitazama hiyo mifano hapo juu, utaona uumbaji wa Mungu haukuwa ukifanana kwa namna yoyote na huu uumbaji wetu, sisi tunaumbana kwa kukutana kimwili kama ambavyo wanyama wengine wote huumbana, tena kukutana kwetu kunasababishwa na tamaa zetu za kimwili.
 
Kuna mtu alisikiliza hotuba ya Makamba alipokuwa anaongea na wana diaspora Italy? Makamba alisema wakati Magufuli akiwa rais, kuna kundi la viongozi wa CCM ambao walikuwa wanadharau ofisi ya Samia na Makamba, na walikuwa hawataki hata kuongea nao. Pia akasema mara baada ya Magufuli kufariki, hao watu walikuwa wanasema Samia hawezi kuongoza nchi. Akaendelea kuwa Samia baada ya kuapishwa, hakulipa kisasi bali aliwateua kwenye nafasi mbalimbali. Hao watu ndiyo walioficha kifo ambacho Paskal anahoji hapa. Wanajulikana. Ila hofu yao ilikuwa na mashiko. Nchi imeshamshinda.
Yeah ukisoma kwenye Uzi wa Yoga yote wameelezewa
 
Kwa bandiko kama hili mkuu p, naomba jitahidi kuwa nao makini. Maana unaweza kuwa na maadui wengi huko kuliko huku. Kwa mtu mwenye busara kuambiwa ukweli na mtu mwenye nia njema ni furaha kwake maana anapata nafasi ya kujirekebisha. Lakini kwa mtu ambaye ni kinyume chake ukimwambia ukweli ANAKUFANYA KUWA ADUI YAKE.
 
Wanabodi,

Hapa duniani kuna fani mbalimbali za shughuli, na shughuli kuu ya kwanza duniani baada ya Mungu kumuumba binadamu, ilikuwa ni shughuli ya kutengeneza watoto au kuumba viumbe. Kwa vile Adamu na Hawa au Adamu na Eva, wao waliumbwa na Mungu mwenyewe, hivyo shughuli yao kuu ya kwanza ilikuwa ni kutengeneza watoto ili kujenga familia, kwa kuumba viumbe wengine!

Ile shughuli ya kutengeneza watoto ili kujenga familia, au uumbaji wa viumbe vipya, ndio shughuli kuu ya kwanza ya binadamu hapa duniani!, (the oldest professional) na viumbe wote, duniani kabla ya kuzaliwa ni lazima kwanza shughuli hiyo ifanyike, ndipo kiumbe kiumbwe, na ndipo kizaliwe, hivyo japo wengi wanahesabu siku ya kuzaliwa ndio siku yao ya kwanza duniani na watu wanasherehekea siku ya kuzaliwa, yaani birthday.

Hiyo siku ya kuzaliwa, ni siku tuu ya kuingia duniani, lakini sio siku ya kuumbwa!, siku unazaliwa, ujue uliumbwa miezi 9 nyuma!, kwa vile hata wazazi waliokuumba, hata mama aliyekubeba tumboni mwake, anakuwa hana uhakika halisi ni siku gani kiumbe kipya kimeumbika tumboni mwake, kwasababu anayeumba sio binadamu ni Mungu!, jukumu la binadamu ni kufanya tuu tendo la kuumba, lakini muumbani ni Mungu!. Nimeileta hadithi hii ya uumbaji ili kuelezea ndio shughuli kuu ya kwanza duniani.

Baada ya uumbaji shughuli kuu ya pili ni ujenzi wa familia, ulezi, makuzi na shughuli mbalimbali za kuendesha maisha na humu ndimo mwisho wa siku kunakuja kuibuka fani mbalimbali, wa mama wa nyumbani, wapishi, wasaidizi wa kazi, wake, vijakazi, waalimu, madaktari, madereva, wajenzi, wahubiri, matatibu, hata wanga, wachawi na washirikina, zote ni fani.

Kila fani, ina misingi yake mikuu, msingi mkuu wa fani ya ualimu ni kufundisha wengine, msingi mkuu wa fani ya udaktari ni kutibu na kuokoa maisha, msingi mkuu wa fani ya uongozi ni kuwaongoza wengine, msingi mkuu wa fani ya uandishi wa habari ni kuripoti, kueleza ukweli, ili kuueleza huo ukweli, mwandishi yeyote mzuri wa habari, ni lazima awe na uwezo wa kuhoji, mimi kwa sasa nimekuwa ni mtu mzima, lakini enzi zangu za ujana, nikiwa newsroom enzi zangu za kipindi changu cha Kiti Moto, kuna watu walikuwa wakialikwa, wanakimbia!, kilichokuwa kinawafanya wakimbie si uoga tuu wa kuogopa kuhojiwa maswali magumu.

Mahojiano yangu ya mwisho ya maswali magumu, ni yale niliyoyafanya ile siku ya tarehe 4 November, pale mahali, ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kualikwa pale, na ndio ikawa mara yangu ya mwisho, kilichobakia ni barua zangu tuu za kuomba mahojiano ambazo sikuwahi kujibiwa mpaka wengine wameitwa walikoitwa, na mimi nikiendelea kuziandika tuu kuomba mahojiano, na kuendelea kusubiri na kusubiri, angalau msaidizi wa sasa she is very gentle kwa kukueleza lazima uwe na subra sana maana barua za maombi ya mahojiano ni nyingi, foleni ni ndefu ila tunaendelea kusubiria, na hata tukipata fursa, siku hizi, tumeishajizeekea hatuna tena yale maswali magumu ya type ya kiti moto!.

Pamoja na jukumu kuu la mwandishi wa habari ni kuhoji na kuripoti ukweli, lakini sio lazima kila ukweli uripotiwe, kabla ya mwandishi wa habari kuripoti chochote, anapaswa afanye tathmini ya kitu kinachoitwa kwa Kiingereza Objectivity, yaani huu ukweli ninaotaka kuuripoti, ukijulikana, utaidaidia jamii?, hivyo ukikutana na tukio la ukweli kabisa, lakini ukaona ukweli huo ukijulikana, hautaisaidia jamii, wewe kama mwandishi makini, unapaswa kuuhifadhi ukweli huo na kutouripoti, ukweli ambao hautasaidia kitu jamii husika. Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

Tarehe, 12 mwezi March, mwaka 2021, mimi nikiwa ni mshitiri wa akaunti ya mtandao wa YouTube wa mwandishi mmoja Mtanzania anayeishi ughaibuni, alipandisha kwenye mtandao wake, taarifa ya kutokea kifo cha kiongozi fulani wa nchi fulani, lakini viongozi wa nchi hiyo, wameamua kufanya siri!.

Mwandishi huyo, alisema, yeye amepenyezewa taarifa hiyo na jamaa zake ambao ni watu wa "sehemu", na wameamua kumpenyezea yeye, kwa vile na yeye alikuwa ni mtu wa "sehemu", kabla ya kuikimbia nchi na kutokomea ughaibuni, baada ya kushikwa sikio, na watu wenzake wa "sehemu" kuwa wanaitafuta roho yake, ndipo akaamua kukimbilia ughaubuni kuinusuru roho yake ndio maana mpaka sasa bado yupo, vinginevyo angeisha kuwa mavumbi siku nyingi!.

Taarifa ya msiba huo ikasababisha sintofahamu kubwa huku nyumbani!, mara Balozi wetu wa Zimbabwe ambaye na yeye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa ile IOdara ya "sehemu", akatoa taarifa kukanusha!, mara Waziri Mkuu wa JMT akatoa taarifaa, jamaa yuko ana chapa kazi mnataka aende Kariakoo!, mara VP wa nchi hiyo akjatumwa Tanga kwenda kumwakilisha bosi wake kwenye tukio!.

Kwa vile nchi yetu ni nchi ya JMT yenye pande mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, wenzetu kule Zanzibar, toka baada ya kuipokea taarifa hiyo Machi 12, wao walisitisha shughuli zote na ratiba zote za kiserikali za shamra shamra na kufuta ziara zote, huki sisi huku bara tukiendelea as if nothing happened!.

Na baada ya siku 5 tangu nilipopokea taarifa hii, ndipo Taifa tungatangaziwa rasmi kuhusu msiba huo mzito!. Taarifa hiyo iliishitusitusha dunia na Watanzania wote kuhusu msiba wa mkuu wa nchi, laki kwa wale ambao tulipokea taarifa ya msiba huu siku 5 kabla, sio kuwa hatukushitishwa na taarifa rasmi ya msiba, bali sasa tulisumbuliwa na shauku ya kuhoji ukweli ni upi kuhusu msiba huu, ni ile taarifa ya siku tsano zilizopita au taarifa rasmi ndio ukweli wenyewe?, Watanzania wana haki ya kuelezwa ukweli wa nini haswa kilitokea kama ukweli ukweli huo unaelezeka, ila kama ukweli huo haulezeki, then Watanzania bado tuna haki ya kuelezwa kuwa ukweli tarehe halisi ya tukio lile haielezeki ila ile Machi 17 ndio tuichukulie ndio tarehe rasmi ya kutangazwa tukio, kwasababu hata tarehe 25 Desemba, inayatangazwa ndio siku ya kuzaliwa Masiha, ni siku tuu iliyoteuliwa, lakini siku rasmi ya kuzaliwa Masiha, sio hiyo tarehe 25 Desemba, bali ndio siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake.

Familia nyingi za Kiafrika, haswa sisi watu wa Kanda ya Ziwa, tukilewa huwa tuna kelele sana, hivyo ndani ya familia nyingi, huwa tunashuhudia kuna siku baba amepata kinywaji na kikamkolea, anarudi amelewa, anapgizana kelele na Maza, na kuna sometimes Maza anatembezewa kichapo, watoto mnajua, lakini hamuwezi kuuliza, wala kutangaza, inabaki ni siri za familia, ila watoto wa kizazi cha kisasa kizazi cha kuhoji, siku zote huwa wana dukuduku, kimetokea nini hadi Maza atembelee kisago?!.

Sasa kwa tukio kubwa kama lile la tarehe 17 Machi, kama ni kweli lilitokea tarehe 12 Machi, na watu wakakaa na mtu wao siku 5 nzima ndipo waje watutangazie, dukuduku ya kuhoji, walikuwa wanafanya nae nini siku zote 5?. Bado naendelea kusisitiza kuzingatia issues za morality kwenye kuusema ukweli Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

Kutokana na kutoelezwa ukweli ni nini haswa kilitokea, wazushi nao wanapenyezea hapo hapo agenda zao, eti baada ya kutokea kilichotokea ile tarehe 12, haikutangazwa kwasababu kuna kiongozi mmoja wa kidini wa imani fulani, aliwahakikishia anaweza kumrejeshea uhai wake, na akakubaliwa, hivyo hizo siku tano toka tarehe 12 Machi tukio lilipotokea, hadi tarehe 17, lilipotangazwa, juhudi za kumpambania maisha yake, zilikuwa zinaendelea, na baada ya juhudi zote kushindikana ndipo sasa tukatangaziwa rasmi!.

Sisi kizazi cha kuhoji, bado tuna dukuduku, kwa ule msemo wa sterling hauwawi, kama sterling wa filamu alikuwa amelala toka Machi 12, mpaka tulipotangaziwa ile Machi 17, who was running the show?, ni nani walimweleza Waziri Mkuu aseme Mwamba anachapa kazi?!, ni nani walimpangia VP safari ya Tanga ili kumzuga, as if nothing happened, wakati wenzetu upande wa pili wa Zanzibar wao waliahirisha kila kitu?!.

Hitimisho
Japo sio lazima kuhoji kila kitu kwa kuuliza maswali, kakini likitokea jambo lisilo la kawaida, mtu yeyote mwenye akili zake timamu, sio lazima ahoji au kuuliza, lakini ni zazima ajiulize ilikuwaje na ilitokeaje tokeaje?!. Huu ukimya wetu, wa ku observe things, to note things bila kuongea, au bila kuuliza, naomba kusitafririewa kuwa ni mazuzu!, kunapotokea vitu ambavyo Watanzania wanapaswa kuambiwa ukweli, Watanzania tuambiwe ukweli bila kujali ukweli huo ni mtamu au mchungu kiasi gani, ukimya wa Watanzania kutohoji hoji kila kitu, kusitafsiriwe kuwa Watanzania ni mazuzu, kunapotokea jambo, tuelezwe tuu ukweli, tutaelewa. Natoa wito kwa viongozi wetu, mnapoona watu hawahoji hoji sana kama enzi zile, mjue ni wameamua kutohoji hoji sana, na sio kuwa hawaoni, au hawajui, hivyo viongozi wetu msituchulie poa, mkatuona kama mazuzu!, Watanzania sio mazuzu!, kuna siku itafika, ukweli bayana utajulikana, hawa watu watawaonaje?.

Ukweli Usemwe

Paskali
Mkuu Mayalla kulikoni?
Naona leo umeongea kwa uzalendo sana!
Huyu ndo Mayalla tunayemfahamu.
Siyo yule wa siku za hapo katikati aliyetaka kugeuka "chawa"!
Ahsante sana kwa bandiko hili Mkuu.
 
kaka paskali kama unataka mabadiliko kawahoji kule kule juu, wewe uliona wapi wake wa maraisi wanalipwa mafao hawa watu wana uhuru wa manyani wanafanya wanachotaka, wao ndio sheria sheria ndio wao tuliwapenda wenyewe wacha tuendelee kuisoma namba, wewe uliona wapi mtu hupati haki mahakamani hupati haki ngazi yoyote ya mkoa au wilaya hadi ngazi ya kijiji halafu tatizo lako anakuja kulitatua mwenezi wa chama tena kwenye mkutano wa hadhara nchi ya maajabu hii, tuwavumilie tu ni ndugu zetu waliopofuka na kupotoka.
 
Back
Top Bottom