Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Sawa, mi sikatai kuwa hiyo ilikuwa ni kipimo cha imani kwa Ibrahim na familia yake, hata Quran imeelezea hivo
 


Kwa Waislam au Watu ambao wanataka kupotosha kuhusu Wapi Mlima Moria ulipo na kutaka kuhusisha na Mecca.

Moria ni Eneo lilikuwa Jerusalem, Wakati wa Ibrahim anakaa Kaanani Jerusalem ilikuwa ni Nchi ya Jebusites.

Hili Eneo kwenye hii Ramani lilioandika Haram El Sharif ndipo kuna ile inaitwa Dome of the Rock, ndani yake kuna Jiwe linalosemekana Ibrahim alimlaza Isaka, Ndio maana inaitwa Dome of the Rock, this is proof kuwa Quran in most cases ni fabricated document
 
Hayo ni maoni yako,...lakini Biblia haijasema kwamba Isihaka ndiyo mtoto wa pekee wa Ibrahim......so kwa akili ya kawaida tu utajua kwamba Ismail ndiyo amewahi kuwa mtoto wa pekee wa Ibrahim kabla ya kuzaliwa wadogo zake.....
Bible imetawataja watoto wote wa kiume wa Ibrahim
 
Waandishi wa Quran waliifanyia editing BIBLIA.

Nadhani tupo pamoja.
 
Hakuna umoja kati ya waislam na wakristo tunatofautiana hata kimaandiko sisi biblia haitufundishi kulipa kisasi wala kuua
 
Katika watoto hao wote,..yupi amewahi kuwa mtoto wa pekee wa Ibrahim?

Namaanisha Mtoto yupi aliishi kipindi ambacho Ibrahim hakua na mtoto mwingine isipokua yeye?
Upekee wa huyo mtoto ni hilo agano Mungu alilofunga na Ibrahim. Agano lilitaka Baraka ziende kwa mzao na sio wazao kana kwamba ni wengi. Mungu hakukosea kwenye kutamka. Kwani siku amemleta Adam duniani akishindwa kuleta wanadamu wengi. Sote tuliumbwa siku Moja kule mbinguni ila tumeletwa duniani Nyakati tofauti tofauti. Roho yako ilikwisha kuumbwa toka Mungu alipomuumba mwanadamu.
Alifunga agano na mtu mmoja ili baraka zipitie kwake kwenda Kwa alio wapenda.
 
Hujajibu swali nililouliza.....

Katika watoto hao wote,..yupi amewahi kuwa mtoto wa pekee wa Ibrahim?

Namaanisha Mtoto yupi aliishi kipindi ambacho Ibrahim hakua na mtoto mwingine isipokua yeye?
 
Kabla ya kujibu hilo swali tumjue kwanza. Kati ya ismail na isihaka nani mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa ibrahim
Wa Kwanza Kuzaliwa ni Ishmael, according to Muslims scholars Ishmael alitaka kutolewa Sadaka Mecca.

At the same time wanakubali kuwa Ibrahim na familia yake waliishi Kaanani Israel ya Leo na hata Ishmael alizaaliwa na kukulia Kaanani na hata alipofukuzwa yeye na mama yake walifukuzwa kutoka Kaanani kwenda Edom ambayo ni Jordan ya Leo..

Wanazuoni wa Kiislam wanakubaliana kabisa Kaburi la Ibrahim liko Hebron katika Israel ya Leo.

Ni lini Ibrahim na Ishamel walifika Mecca, huoni Quran au watafsiri wake hawakuwa na story Sahihi?
 
Kwa nini Ibrahim alimfukuza Hajiri na Ishmael huku akijua mtoto wa kwanza ndiye mrithi?
Si kweli kwamba mtoto wa kwanza ndio mrithi, rejea historia ya Yusuf alikuwa ni mtoto wa kumi na mbili kama sijakosea, ila si ndo yeye aliyefuatia katika utume baada ya baba yake wakati anao kaka 11 juu yake.

Pili, narration ya kwamba Ibrahim aliwafukuza Hajra na mwanawe hii ni narration ya biblia sio Quran. Ibrahim alienda pamoja nao akawaacha pale alipoamrishwa na mwenyezimungu akawaache (jangwani), hii ilikuwa ni trial kwake kama ile trial ya kumchinja mwanawe.

Naendelea kutafuta ecidence ya ayah ila kama yupo anayeijua atuwekee hapa
 
Hakuna umoja kati ya waislam na wakristo tunatofautiana hata kimaandiko sisi biblia haitufundishi kulipa kisasi wala kuua
Wakristo na Waislamu ni watoto wa Baba mmoja Ibrahim na Mungu wao ni mmoja, Waislamu ni watoto wa mtoto wa kwanza wa Ibrahim aitwae Ismail na Wakristo ni watoto wa mtoto wa pili Isaka, hata sheria ya Mungu ni sheria ya Musa.

P
 
Lakini pia unapozungumzia baraka,... mbona inaonyesha Ismail na Isihaka wote wamepewa baraka nyingi tu... hii imekaaje
 
Huu si ugwadu tu,Wana wa Mungu!!?..Mungu Hana watoto,Wala Aya haisemi mission ya nuhu ni kujenga safina tu,nabii wa kujenga safina tu!!?..be serious babu

Aya ipi Haisemi wito wa Núhu
Mimi nilikuwekea aya hiyo kujibu swali lako ilipouliza Núhu alikuwa mpagani.

Jibu la biblia ni kuwa hiyo Núhu mwenyewe alipata tuu neema sio kwamba alikuwa mtakatifu kihivyo

Ukisoma stori yoyote lazima ujue na kuzingatia yafuatayo;
1. Dhamira kuu ya stori.
2. Mbebaji wa dhamira hiyo ni nani? Huyu huwa mhusika Mkuu


3. Ujumbe wa stori ni upi.
4. Mtazamo na falsafa ya stori

Sasa nje ya Safina Núhu anajambo lipi linalomfanya aandikwe kwenye Biblia au Quran?

Au unafikiri watunzi na waandishi wanaandikaga tuu?

Mungu ni Baba.
Kasome Semantic ya Lugha kisha soma Falsafa ya dini (Theolojia) utaelewa mambo haya

Lakini kwa akili ndogo ndogo huwezi kuchambua mambo ya kitaalamu na kifalsafa au Kifasihi au Isimu. Yaliyopo kwenye maandishi
 
Umeandika Mengi ila Kitu nachosikitika Umetunga Hoja zako na Umezijibu yaani Umefanya Self Implication..
Hakuna Hoja yangu hata moja Uliyojibu..
 

Tunaomba hiyo simulizi ya Quran inayoonyesha mahali aliporithishwa, achiwa huyo Ishmael
 
Habari Ammoshi!
Ibrahimu alimuoa Hajiri na alikuwa Mke wake wa Ndoa (Mwanzo 16:3)..

Ibrahimu Alimbariki na Kuomba Baraka kwa Mungu Naye Mungu akamsikia na kumbariki Ishamael soma Mwanzo 21..

Maagano kipindi Yanatoka Ibrahimu alikuwa na Miaka 99 na Ishmael alikuwa na miaka 13 Hivyo alitahiriwa na familia yake yote na hilo ndilo agano la.kwanza..

Kuhusu kutafutiwa Mke Unajisahau kabisa kwamba Isaka alikuwa Uzao wa Nadhiri Na Ishmael alikuwa uzao wa Mwili???

Wagalatia 4:28-29

"Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi.
Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa."

Wazao wa Nadhiri wote Hutafutiwa Mke ndani ya Ukoo Na ulinzi wa Baba zao..(Fuatilia Kisa Cha Esau (Edomu) na Yakobo)

Kuhusu Urithi na kuwa Pamoja Je Hukusoma Kuwa Isaka na Ishmaeli walimzika Baba Yao alipofariki akiwa na Miaka 175??
 
Soma hapo.kama una swali lingine uliza.pia baada ya hajr kijakazi wa bibi sara kumzalia Ibrahim mtoto wake wa kwanza Ishmael. Mama Sara akaanza kuona wivu akamchukia hajr na mwanae.ndipo Ibrahim akaamua kuwatorosha na kwenda kuishi makka. Na usisahau kisima cha zam zam.kilichimbwa kwa ajili ya hajr na ismail walipofika makka. Hakukuwa na mji
 

Attachments

  • Screenshot_20240621_103908_Chrome.jpg
    572.9 KB · Views: 4
Hahahaaaa Una Uhakika Mkuu Unajua Sheria Za Ndoa za kiyahudi kama Inavyosema Gimera au Halakha au Torati??

Unafahamu Mwanamke alikuwa na Mamlaka gani kwa mume??

Bhasi nikupeleke Mbele kwa Hao Wake za Yakobo..
Unajua kuwa hata Yakobo hakuwahi Kumregard Lea kama mkewe??

Na unafahamu Kuwa hakuna Mahali imeandikwa kuwa Yakobo alimuoa Lea bali alidanganyika kulala na Lea tu..

So mke wa Yakobo alikuwa Rahel na hao wengine watatu hawakuwa wake wa Yakobo..

Unaweza ukadouble check..Biblia inamtaja Rahel kama ndiye Mke wa Yakobo..ila haimtaji Lea kuwa ni mke wa Yakobo..

TItle ya Mke kwenye Biblia ni title Kubwa Sana Ambayo Kama hakuwa Mke Basi Hajiri angeitwa Suria (Ambayo Ni upgrade ya Kijakazi anapolala na Bwana..

Tatizo letu hatuelewi maandiko ila tunataka Tumeze tulivyoaminishwa bila kureason vitu... nilitoka huko zaman nilipoacha Uchungaji...

Kwanini Mke wa Kwanza alikuwa na Nguvu ya Kumrisha na hata Nguvu ya Kuomba kuolewa mwingine..(Ngoja nakuja na Halakha(Sheria za kiyahudi))
 
Hajiri hajawahi kuwa Mke wa Ibrahim
Alikuwa kijakazi wa Sarah mkewe Ibrahim.

Aliyemfukuza Hajiri ni Boss wake ambaye ni Sarah.

Hiyo simulizi unaijua vizuri?
Kwani Nyie huwa hamsomi Biblia au Mnaongozwa na Chuki..
Hebu someni Mwanzo 16:3 halafu Ichambue bila chuki Au mnataka mpaka tulete Hebrew Version of it tuichambue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…