Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Biblia inajikamilisha kuanzia agano la kale na jipya , ndo maana kitabu cha Isaya kimeongelea maisha ya Yesu Kristo before Yesu ajazaliwa kwa uweza wa Roho mtakatifu.
MKuu Nimewahi kuwa Myahudi na Nikasoma One Year Torati na Sheria na TANAKH kwa ujumla...
Na kwa bahati nzuri Kipindi nakuwa Myahudi..

Tayari nilikuwa nimesoma Theology..
Nikuhakikishie kuwa Agano la kale halina uhusiano na Agano jipya..

Na ndo maana ukisoma Churches History Ilichukua Muda mrefu sana Kuliweka Pamoja agano la kale na agano jipya Mpaka Mwaka karne ya 9 au 10 AD ndo liliwekwa Pamoja..

Makanisa ya awali kama Ebionite christians, Marcionite christian (Sasa hiii iliyokuwa miaka ya 100 mpaka 400) na mengine Walipinga Agano jipya Kuchanganywa na Agano la kale..

Mpaka karne ya 8 mpaka 10 ndo tulipopata bahati kuchanganya..

Na I can Tell you that Tukitumia Agano la Kale Yesu ana fail kuwa Mtarajiwa yaani kama tutatumia kipimo cha agano la kale na maisha ya yesu its really tusifike huko.. Cuz i've been There and i know it....

Isaya unayosema haihusiani na yesu hata kidogo
 
Ujuwe tu kuwa Quran ina miaka 1400 wakati Bibilia ina miaka zaidi ya 2000. Hapo utagundua ni nani kakopi kwa nani?

Halafu kuna watu wanadanganywa eti Mtume wao aliteremshiwa kitabu. Uwongo mtupu
Qur'an haijakopi kwa yeyote, kama una ushahidi wa kukopi uweke hapa, usijaze watu ujinga uliokujaa.

Andiko kuwa la zamani zaidi siyo uthibitisho kuwa ni la kweli . Qur'an ndiyo imekuja kubainisha ukweli (criterion).
 
Kitu muhimu ni tuutafute ukweli, Mungu hakuleta dini wale Yesu hakuleta dini!. Hoja hapa ni nani mkweli na nani muongo?. Mtoto aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni nani?.
P
Hakuna mtoto wala mkubwa yeyote aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinjwa, hilo nadhani nimeshalijibu, kuwa ni porojo za watu lakini mimi sijawahi kuliona kwenye Qur'an. Na nimekuhakikishia juu huko, na mwenyewe utajionea na kusikia video clipo ya sheikh aliyeambiwa atafsiri akakwepa kwa kumnukuu mtafsiri mwengine wa zamani.

Huyo Mungu anayetaka kafara ya damu ya mtu atakuwa ni mchawi, hilo sikubaliani nalo kabisa na halipo kwenye Qur'an.
 
Soma post yangu Dada Faiza Namba 310..
Inamajibu kuwa Quran imeandika Kuwa ALiota Mungu anamwambia kuwa amchinje..

Sasa nakuomba Ukishaisoma Hiyo Ukatae aya za Qurani na Uwe mmoja wa waliokufuru 🤣🤣
 
Wakristo na Waislamu ni watoto wa Baba mmoja Ibrahim na Mungu wao ni mmoja, Waislamu ni watoto wa mtoto wa kwanza wa Ibrahim aitwae Ismail na Wakristo ni watoto wa mtoto wa pili Isaka, hata sheria ya Mungu ni sheria ya Musa.

P
Sasa kama uislam ni wa mtoto wa kwanza wa ibrahimu basi uislam ndio dini ya kwanza
 
Iraq ilikuwa Mesopatamia, Misri iliitwa misri hivyo hivyo wakati huo Irani imeanza kuwa Arabuni miaka ya karne ya 18..

Sasa sjui Kama unaijua Historia vzuri kuwa..
Wana historia wanaporefer Arabuni Humaanisha Macca na medina au Saudia peke yake
Saudia ni zaidi ya Makkah na Madina, kiarabu burbur Cha kwenye QUR'AN kinazungumzwa zaidi Yemen,ambayo imepakana na saudia,na waarabu wanakwambia myemeni ndiye mwarabu haswa
 
Kukatwa Jando sio Dhabih faiza!

Hapo nitawatetea Waislam unawaonea..
Neno "khitan" au huandikwa kiarabu "ختان" ndo humanisha Jando au Kutairiwa na mtu aliyetahiriwa Huitwa "Makhtun"

Na Faiza Huwa unasoma Quran yako??
Nifatilize..

Soma Surah As-Saffat aya ya 102

فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ ٱلسَّعْىَ قَالَ يَٰبُنَىَّ إِنِّىٓ أَرَىٰ فِى ٱلْمَنَامِ أَنِّىٓ أَذْبَحُكَ فَٱنظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَٰٓأَبَتِ ٱفْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّٰبِرِينَ

Inatamkwa hivi ..

"Falamma balagha maAAahu alssaAAya qala ya bunayya innii ara fii almanami annee athbahuka faunthur matha tara qala ya abati ifAAal ma tumaru satajidunii in shaa Allahu mina alssabiriina"

Ambayo maana yake ni hii..

Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri.

nimeshangaa Kuona Neno أَذْبَحُكَ inatamkwa adhbahuka..... Unasema Tafsiri yake ni Jando ulisoma Wapi Arabic Grammar walizokufundisha hivyo??? mpaka kesho Hilo neno Humaanisha Kuchinja Au kuua Wewe umepata wapi maana tofauti na hiyo..
Unaifata tafsiri ya watu badala kuifata "tafsil" ya Qur'an, hilo neno siyo hapo tu limetumika katika Qur'an, limetumika na kwengine halimaanishi kumchinja mtu kwa kumkata shingo yake. Hiyo ni tafsida ambayo wengi imewapiga chenga.

Soma hapo hapo ulipo mbele yake kidogo aya ya 107 utalikuta hilo neno lina kisra na kutamkika "dhibh" siyo tena dhabah kama juu hapo ulipopanukuu wewe, unajuwa maana yake hiyo? Maana yake ni "incision" au mkato mdogo siyo kuchinja kama walivyopotosha watu.

Naona hapo umefata porojo za watu na hukuifata Qur'an, Qur'an inajieleza (self-explanatory) na kujibainisha (mubyin) yenyewe, haijawacha kitu kinaning'inia (hanging) ili kije kitiwe mikono ya watu. Hakuna neno la mtu linaloweza kuwa na ubora au uelewa zaidi ya Qur'an.

Ukisoma kuhusu "locution" au lexicon utanielewa nasema nini.

Hiyo uliyoitafsiri ni ndoto ambayo Ibrahim anamuekeza mwanae alichoota, ukitaka kuelewa ni mwanae yupi soma sura hiyohiyo aya ya 113.
 
Nipe Andiko akitajwa kuwa Mke wa Yakobo au Yakobo akimtaja kuwa Mke wake

Swali linakuja kwanini unaichukua Aya ya 3 mpaka uiruke na kwanini unabagua aya..

Unataka Niamini maneno ya Yesu alipowaambia Walimu na Mafarisayo..

Kuwa wanachuja Mbu na Kumeza Ngamia????
Yaani wanachukua baadhi ya Mafundisho na mengine kuyaacha (Yale yasiyoyapenda?)

Namimi Nakuuliza EWE Mtibeli KWANINI UNACHUJA MBU N KUMEZA NGAMIA???

Mathayo 23:23-25

Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.

Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.

Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi.

Hakuna aliyeruka Aya.
Ishu ni kuwa wewe unatumia aya moja kupinga aya mia moja.

Sheria za ndoa zipo wazi
Ndoa zinataratibu zake nawe unazijua.
Na talaka zinataratibu zake unazijua

Hajiri hajawahi kuwa mke wa ndoa wa Ibrahim.
Hiyo Aya úliyotoa kimantiki na kisheria haiwezi kumfanya Hdjiri kuwa Mke labda kwa mbali Concubine
 
Nipe Andiko akitajwa kuwa Mke wa Yakobo au Yakobo akimtaja kuwa Mke wake

Ushahidi uliopo ni kuwa Leah aliozeshwa kwa Yakobo yeye na Mdogo wako Raheli.

Biblia inatambua kuwa Yakobo anawake wawili na vijakazi wao
Mwanzo 32:22
[22]Akaondoka usiku ule akawatwaa wakeze wawili, na vijakazi wake wawili, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Yaboki.
And he rose up that night, and took his two wives, and his two womenservants, and his eleven sons, and passed over the ford Jabbok.
 
Hakuna aliyeruka Aya.
Ishu ni kuwa wewe unatumia aya moja kupinga aya mia moja.

Sheria za ndoa zipo wazi
Ndoa zinataratibu zake nawe unazijua.
Na talaka zinataratibu zake unazijua

Hajiri hajawahi kuwa mke wa ndoa wa Ibrahim.
Hiyo Aya úliyotoa kimantiki na kisheria haiwezi kumfanya Hdjiri kuwa Mke labda kwa mbali Concubine
Nimekuambia taratibu za Ndoa kwa mujibu wa Biblia ni zipi nakusikiliza Uniambia Ambazo Ibrahimu hakufata kwa Hajiri? 😅

Na hakuna mahali Hajiri anatakwa kuwa Suria (Concubine) sasa kwanini Umuite Suria?

Hebu nieleweshe kuhusu Ndoa maana Navyojua hata Sara ibrahimu alijitwalia tu na wala hakuna Process unazosema wewe 😅😅

Mwanzo 11:29

"Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska."

Sasa kama Mke wa kwnza Alijitwalia Inakuaje Mke wa Pili akijitwalia Useme Ndoa ya Mke wa Pili japo imeandikwa sio ya Kweli😅😅

Still On Denial mkuu, ALETHOPHOBIA
 
Unaifata tafsiri ya watu badala kuifata "tafsil" ya Qur'an, hilo neno siyo hapo tu limetumika katika Qur'an, limetumika na kwengine halimaanishi kumchinja mtu kwa kumkata shingo yake. Hiyo ni tafsida ambayo wengi imewapiga chenga.

Soma hapo hapo ulipo mbele yake kidogo aya ya 107 utalikuta hilo neno lina kisra na kutamkika "dhibh" siyo tena dhabah kama juu hapo ulipopanukuu wewe, unajuwa maana yake hiyo? Maana yake ni "incision" au mkato mdogo siyo kuchinja kama walivyopotosha watu.

Naona hapo umefata porojo za watu na hukuifata Qur'an, Qur'an inajieleza (self-explanatory) na kujibainisha (mubyin) yenyewe, haijawacha kitu kinaning'inia (hanging) ili kije kitiwe mikono ya watu. Hakuna neno la mtu linaloweza kuwa na ubora au uelewa zaidi ya Qur'an.

Ukisoma kuhusu "locution" au lexicon utanielewa nasema nini.

Hiyo uliyoitafsiri ni ndoto ambayo Ibrahim anamuekeza mwanae alichoota, ukitaka kuelewa ni mwanae yupi soma sura hiyohiyo aya ya 113.
Bi mkubwa wewe tetea hoja sio hizi porojo, weka haya hizo ili uleweke Kama jamaa alivyo kujibu.
 
Suratul Maryam aya 54

وَٱذْكُرْ فِى ٱلْكِتَٰبِ إِسْمَٰعِيلَ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ صَادِقَ ٱلْوَعْدِ وَكَانَ رَسُولًۭا نَّبِيًّۭا

TAFSIRI:

Na mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii.
Aya ya pili
surat Ibrahim Aya ya 39

ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى وَهَبَ لِى عَلَى ٱلْكِبَرِ إِسْمَٰعِيلَ وَإِسْحَٰقَ ۚ إِنَّ رَبِّى لَسَمِيعُ ٱلدُّعَآءِ

TAfsiri..

"Alhamdulillahi! Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu aliye nipa juu ya uzee wangu Ismail na Is-haq. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia maombi."

Aya ya Tatu

Suratul Baqarah aya ya 127

وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَٰهِۦمُ ٱلْقَوَاعِدَ مِنَ ٱلْبَيْتِ وَإِسْمَٰعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّآ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ

Tafsiri:

"Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi."

Aya Ya nne:

Suratul Baqarah aya ya 136

قُولُوٓا۟ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَآ أُنزِلَ إِلَىٰٓ إِبْرَٰهِۦمَ وَإِسْمَٰعِيلَ وَإِسْحَٰقَ وَيَعْقُوبَ وَٱلْأَسْبَاطِ وَمَآ أُوتِىَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَآ أُوتِىَ ٱلنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍۢ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُۥ مُسْلِمُونَ

TAFSIRI:-

"Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake."

Ziko nyingi ila kwa leo Chukua Hizo.labda nyongeza ni 2:133
Hapo umechanganya madawa, sijakuelewa hizo ayat zote umeziweka ili uthibitishe nini?

Nakushauri werka aya moja, useme unachotaka kukisema au kukithibitisha, tukisha kufundisha hiyo aya uhamie nyingine.
Unaonesha ulichokifanya ni ku search "Ismail" na kukopi na kubandika hapa kila ulipokuta Ismail. Usomi na uelewa hauendi hivyo, hizo ayaat ulizobandika mitume mingi imetajwa hapo na unaweza kuzinukuu quote bila uelewa wa muktadha (context).
 
MKuu Nimewahi kuwa Myahudi na Nikasoma One Year Torati na Sheria na TANAKH kwa ujumla...
Na kwa bahati nzuri Kipindi nakuwa Myahudi..

Tayari nilikuwa nimesoma Theology..
Nikuhakikishie kuwa Agano la kale halina uhusiano na Agano jipya..

Na ndo maana ukisoma Churches History Ilichukua Muda mrefu sana Kuliweka Pamoja agano la kale na agano jipya Mpaka Mwaka karne ya 9 au 10 AD ndo liliwekwa Pamoja..

Makanisa ya awali kama Ebionite christians, Marcionite christian (Sasa hiii iliyokuwa miaka ya 100 mpaka 400) na mengine Walipinga Agano jipya Kuchanganywa na Agano la kale..

Mpaka karne ya 8 mpaka 10 ndo tulipopata bahati kuchanganya..

Na I can Tell you that Tukitumia Agano la Kale Yesu ana fail kuwa Mtarajiwa yaani kama tutatumia kipimo cha agano la kale na maisha ya yesu its really tusifike huko.. Cuz i've been There and i know it....

Isaya unayosema haihusiani na yesu hata kidogo

Sahihi
 
Bi mkubwa wewe tetea hoja sio hizi porojo, weka haya hizo ili uleweke Kama jamaa alivyo kujibu.
Aya kishaweka yeye, lakini kaishia juu, nimemweleza hivyo ili akasome muktadha, na wewe pia unaweza kufanya hivyo ili uupate muktadha. Yeye kaweka aya ya 103, nimemfahamishe aende hapo hapo mpaka aya ya 107 atayakuta yanajieleza vizuri:

1718966096978.png
 
Back
Top Bottom