Jaribio la kigaidi: Rubani kumchoma kisu rubani mwenzie na kulazimisha ndege kubadili njia

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
11,999
Reaction score
24,328
1790777740081.png
Video hii ina picha zinazoonesha majeraha yaliyotokana na ajali ambazo zinaweza kuwaogofya au kuwasumbua baadhi ya Watazamaji. Tafadhali tazama kwa tahadhari.

Ndege ya shirika la Flydubai iliyokuwa ikisafiri kutoka Dubai kuelekea Israel ililazimika kutua kwa dharura Nchini Saudi Arabia Jumatano, baada ya kutokea vurugu ndani ya chumba cha marubani, ambapo mmoja wa marubani alidaiwa kumshambulia kwa kisu rubani mwenzake na kujaribu kuichukua kwa nguvu udhibiti wa ndege hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za Vyombo vya Habari, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema tukio hilo limetokea wakati ndege ikiwa inakaribia Israel, akidai kuwa mmoja wa marubani alimchoma mwenzake na kujaribu kuiangusha ndege ikiwa na Abiria.

Netanyahu amewapongeza Abiria na Wafanyakazi wengine wa ndege kwa kuingilia kati na kusaidia kuzuia tukio hilo ambapo Maafisa wa Israel wamesema uchunguzi unaendelea kubaini iwapo tukio hilo lilikuwa jaribio la shambulio la kigaidi lililolenga kuangusha ndege, pamoja na kubaini iwapo Mshambuliaji alitenda peke yake.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, alilitaja tukio hilo kuwa jaribio la shambulio la kigaidi, akisema lilizuiwa kutokana na hatua za Abiria kadhaa wa Israel waliodhibiti Mshambuliaji na kusaidia kurejesha udhibiti wa ndege hiyo aina ya Boeing 737 MAX 8 ambayo ilielekezwa na kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Tabuk, Saudi Arabia.
 
Attachments

  • 6408031-2514bc7b3188468744f99cca93823121.mp4
    7 MB
Ndege ya Flydubai FZ1073 iliyokuwa ikisafiri kutoka Dubai kwenda Tel Aviv imelazimika kubadili njia na kutua mjini Tabuk, Saudi Arabia, baada ya mapambano kuripotiwa kati ya marubani wawili ndani ya cockpit.

Kwa mujibu wa Flightradar24, ndege hiyo ilituma kwanza namba ya dharura 7700, kisha 7500 inayotumika kuashiria kuingiliwa kinyume cha sheria au uwezekano wa utekaji wa ndege, kabla ya kurejea tena 7700. Ndege hiyo pia ilifanya mteremko mkali wa maelfu ya futi ndani ya muda mfupi.

Maafisa wa Israel wamesema kulikuwa na ugomvi wa kimwili kati ya rubani mkuu na rubani msaidizi ndani ya cockpit. Tukio hilo lilisababisha tahadhari ya kiusalama nchini Israel, ikiwemo kurushwa kwa ndege za kivita na kufanyika kwa mashauriano ya viongozi wa usalama.

Baadhi ya vyombo vya habari vya Israel vimedai kuwa mapambano hayo yalikuwa makali kiasi cha mmoja wa marubani kujeruhiwa, huku kukiwa pia na madai ya kutumika kwa kisu. Madai mengine yanasema huenda mmoja wao alijaribu kuielekeza ndege chini kwa makusudi.

Hata hivyo, madai hayo bado hayajathibitishwa rasmi na Flydubai wala mamlaka za Saudi Arabia.

Ndege hiyo ilitua salama Tabuk, huku Flydubai ikisema abiria waliokuwa ndani wako salama. Uchunguzi kuhusu kilichotokea kati ya marubani hao unaendelea.

View attachment 3681236
Unawezaje kuingia na kisu Airport 🛫 🛬?
 
Unawezaje kuingia na kisu Airport 🛫 🛬?
Meal-service cutlery, Kama ndege ilikuwa na meal service, kisu cha chakula kinaweza kuwa ndani ya cabin. Kisu kama hicho kinaweza kuchukuliwa na mtu na kupelekwa kwenye cockpit, kulingana na taratibu za crew.

Galley/aircraft equipment, Ndege hubeba vifaa mbalimbali vya kazi ambavyo vinaweza kuwa na makali au muonekano wa visu. Hii ni tofauti na silaha rasmi ya kisu ambayo abiria angejaribu kuingiza kutoka nje.

Pilot/crew equipments zilizoidhinishwa
Baadhi ya operators wanaweza kuruhusu vifaa maalum vya utility/emergency kwa crew chini ya SOP zao. Hata hivyo, hii haimaanishi rubani anaruhusiwa kubeba kisu kama silaha binafsi.

Kitu kingine kilichokuwa kwenye ndege
Inawezekana pia kilikuwa kifaa ambacho hakikuwa kisu cha chakula kabisa, uenda ni kitu kingine chenye ncha kali. Hili ni muhimu kwa sababu taarifa za awali kuhusu tukio hilo bado hazijaweka wazi chanzo na aina ya kifaa kilichotumika.
 
Sawasawa
 
Yeah..hata kalamu tu zile marubani wanazotumia wakiwa ndani ya chumba chao inaweza kugeuka kuwa silaha
 
Back
Top Bottom