Rais anaetoka madarakani hua anaacha mipango mikakati yake kwahyo Rais anaekuja anatakiwa akamilishe kwanza aliyoyaacha mwenzie halafu na yeye aendelee na yake kwahyo anahitaj ushirikiano na mtangulizi wake hiki kitu JPM alikikataa akafuata njia yake ndio maana ktk madaraka yake alichangua kila kitu cha utawala uliopita bahati mbaya aliishia katikati kwahyo kwa sasa SSH anahitaj msaada wa JK ili kurudisha ile mikakati aliyoiacha ambayo JPM aliipuzia
Na hapo ndipo wote tunapoonekana mazwazwa. Mtu mmoja awe na mikakati yake? Raisi anaingia madarakani kutekeleza sera ya nchi(kama ipo kwenye hii nchi ya kufikirika). Hapaswi kuwa na uwezo wowote wa kutengua yale yaliyopangwa na elites wa nchi.
Ukiweka kwa utendaji, maraisi ni watatu tu waliohudumu. Waliosalia, hawakustahili hata kuwa watendaji wa kata kiupeo, labda kivyeti.
Miaka 60 bado tunajenga madarasa na kununua madawati! Miaka 60, nchi ipo kwenye kamkoa kamoja tu kadogo ambapo na kenyewe hakana muonekano wowote, hata ardhi yake tu haijapimwa yote kuashiria kuna mipango na maono.
Miaka 60 tunaendekeza ubwanyenye na umimi wa kina fulani!
Tunapata raisi mkulima, anaanda shamba, anapanda, mazao yanapoanza kuchepua, anaingia raisi mfugaji, anaingiza mifugo shambani, inakula mazao na kuharibu mazao, kisha tunapata raisi mkulima tena, then mfugaji, mkulima na circle kuendelea.
Bahati tuliyonayo sasa ni kuwa, kuna mfugaji, akiongozwa na mfugaji wakiwa na washauri wafugaji.
Kazi inaendelea