Jasusi kaniambia sababu ya kuachana na Nifa

Jasusi kaniambia sababu ya kuachana na Nifa

Miaka HII WANAUME TUMEBAKI WACHACHE SANA. YAANI MTU KABISA UNAKUJA ANZISHIA UZI UHUSIANO WA MTU MWINGINE, ARE YOU NORMAL? NI AIBU HATA KUZUNGUNZIA. LENGO NINI? UONEKANE UPO KARIBU NA MTALAKA? THEN? WANAUME WAZAMANI ILIKUWA HUWEZI JADILI MAHUSIANO YA MTU MWINGINE. ULIKUWA MWIKO KABISA.
The special one laminated comment for 2024 [emoji119]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
JAMAA NIMEMSHANGAA SANA! AU NIFA ALIWAHI KUMNYIMA??

NI AIBU KWA MWANAUME KUJADILI UHUSIANO WA MTU MWINGINE, KIBAYA ZAIDI NI KAMA ANAONESHA KUFURAHISHWA KUACHANA KWAO.

WHAT IF KESHO WAKIRUDIANA, ATATUAMBIA NINI HAPA!?

#WANAUME TUMEBAKI WACHACHE SANA.
Nimeshtuka sana. Sijui kwa nini amefurahia hivi mtoto wa kiume. Na ameanzisha na uzi kabisa.... Inashangaza. Kuwa mwanaume ni kazi miaka hii.
 
Huwezi mwanaume ukwa mbea au kushadadia mahusiano ya mwanaume mwenzio. Ni mwiko. Uone aibu hata kidogo.
Watibeli wanafanya chochote isipokuwa kuvunja sheria za Mungu,
Hayo mapokezi yenu ya kijinga kama yale mwanaume haliko, haishi vyombo au hamsaidii mkewe kwetu hayana maana yoyote ile.

Wewe unajiona mwanaume kwa kufuata mapokeo yasiyo na maana yoyote.
 
Bado nipo kwenye Mkesha wa "Vuka na chako"

Habari za nifa zimenishtua mno. Sikutegemea habari hii hasa kwa siku ya leo.
Unajua nifa alikuwa anampenda sana Jasusi. Yeye ndiye aliyejivunia mahusiano hayo mara kwa mara humu JF. Wengi walimjua kupitia mahusiano hayo ya Jasusi. Ukiyaita mahusiano ya kijasusi hutokuwa unakosea.

Wale wenzangu na miye wazee wa kuchungulia pm za Wadada tulifunga breki kwenye Pm ya Nifa kwani kwa sisi wataalamu wa mapenzi tunajua kabisa mapenzi yakikolea kwa kiwango cha juu kabisa si ajabu wapenzi kubadilishana simu na password. Hiyo ikaturudisha nyuma kwa kuhofia jasusi ana-access na account ya Nifa.

Wapo waliofurahishwa na habari hizo. Wapo pia waliohuzunishwa.
Nimewasiliana na jasusi yeye kwa uchovu kabisa alinijibu kuwa imeisha! Imeisha Mtibeli.
Nikamwuliza shida nini, akaniambia kumbe walikubaliana mwaka huu warasimishe. Na kama hawatarasimisha basi binti atachukua uamuzi mgumu.

Kuna mdakaji, mdakuzi, na mdukuzi. Kwenye mambo ya ujasusi bhana.
Jasusi kazidiwa kete na mojawapo hapo.
Ilipohitimu mwezi wa nane mambo yakawa mambo. Mojawapo hapo juu akamzidi jasusi.

Hata hivyo Jasusi kwa nilivyomsikiliza, taarifa hizi hazimuumi sana. Kingine ni kuwa kama mjuavyo binti yetu ndio alipenda zaidi kuliko jasusi mbobevu.

Ngoja tuendelee na nyimbo hapa kwenyw mkesha
Huenda nifah hana msinyungu
 
Safi za Malawi si mbaya pia. Nitumie nitashukuru. Muwe mnawasaidia hawa watu wanaanzisha nyuzi kama hizi muwashauri kuwa ni kupoteza uanaume. Yaani mwanaume kabisa unajisifu kuwa umeongea na mwanaume kuhusu mwanamke wake na unaanza tangaza mtaani? Nimeshtuka sana. Siku hizi hata wanawake wameacha umbea na uchawa wa namna hiyo.
🤣🤣🤣🤣Mi najua wewe ni mzee kifimbocheza hebu mshughulikie huyu Kijana aisee
 
Najua una nature ya ubishi Huwa hukubalo kushindwa Wala kuambiwa ukweli ila Kwa hili chukua au acha umechemsha...
1.mwanaume unatakiwa kuwa na kaba,haiwezekani umesikia jambo ukanunua vocha ukaanza kumuuliza the bold personal life yake,sawa maybe ni mshkaji wako kama unavyojinasibu,mwenzio akakusimulia kilichotokea baina yao,wewe badala uyatunze unakuja kuyamwaga kwenye public "eti nimeongea na muhusika"

2.Unamkandamiza dada wa watu anaforce ndoa,hata kama alikuwa anaforce ndoa ni hitaji la Kila mwanamke anapokuwa kwenye mahusiano ya muda mrefu Sasa kisa lake lipi?

3.Huko Kwa Mwamposa umevuka na na Nini?maana akili yako ilikuwa juuu juuu kuwaza ubuyu.

Eti watibeli 🤣🤣🤣🤣🤣
Mtumishi,nn Tena
Naona kumekucha

Afu mbona pm Iko closed 😅😅
 
.....
Achaneni na huu uzushi basi, sijawahi kulazimisha ndoa, katu!

Kwamba nilitaka ndoa ndipo tukaachana? Nonsense.
Sababu zilizotufanya tuachane ni nyingi na hii sio moja wapo.
Asanteni.
.........nikushauri kitu bibie, kwa kuwa ulishaweka uzi wa kutoa taarifa rasmi, basi achana na maswala ya kufuatilia uzi wowote utakaoanzishwa kukuhusu, hii ni kwa ajili ya afya yako hasa kiakili(cyber bullying zipo za aina nyingi)
........kwa nionavyo mimi wapo wengi humu wasiokupenda, na wamefurahishwa na hili, hivyo basi kadiri unapoendelea kujibu, unadraw attention zao na kuendelea kukubeza kukujadili negatively kadili unavyojibu
........mwanzoni koments zimeanza kwa kukutakia kila lakheri na pole, lakini utaona muda unavyokwenda meseji zenye mrengo wa kiudhalilishaji na maneno yenye muelekeo wa matusi yameshaanza kuonekana coz wanajua unafuatilia(mbaya zaidi maneno mengine yanatoka kwa wanawake wenzio) so wewe acha kujibu na ishia hapa, napengine usirudi hata kuchungulia nini kinaendelea coz utalazimika kujibu........
........mwisho nakuona nakuona ni mwanamke mwenye akili(self determined), mwenye nguvu ujasiri na uwezo wa kusimama nakusonga mbele, pia ulikuwa unakuja vema ktk stori zako za udaku wa mastaa hebu rudi tuandikie kazi iendelee(ukifoocus vizuri eneo hili nakuona ukifikammbali coz upo vizuri sana kiuandishi, unaweza kufunguankiblogu chako ukaanza kupiga shekeri mdogomdogo then you grow up)......
.......ila kama utalazimisha kujadili hili swala lako utajikuta unaanza kutaja mambo ambayo ulipanga iwe siri yako au yenu, we si unaona jamaa yupo kimya, na wewe nikuombe uwe kimya, hii mada mtuachie wananzengo wenyewe tujadili, tujiulize na pia tujijibu wenyewe, umefunga mwaka vizuri fungua mwaka vizuri kwa mambo mapya, hilo litapita, jf ni pazuri ila sio pazuri sana, Heri ya mwaka mpya.
 
Back
Top Bottom