Jasusi kaniambia sababu ya kuachana na Nifa

Jasusi kaniambia sababu ya kuachana na Nifa

Dude la kusi dikizia Mwaka😀🤒
Screenshot_20231231-232706_1.jpg
 
Bado nipo kwenye Mkesha wa "Vuka na chako"

Habari za nifa zimenishtua mno. Sikutegemea habari hii hasa kwa siku ya leo.
Unajua nifa alikuwa anampenda sana Jasusi. Yeye ndiye aliyejivunia mahusiano hayo mara kwa mara humu JF. Wengi walimjua kupitia mahusiano hayo ya Jasusi. Ukiyaita mahusiano ya kijasusi hutokuwa unakosea.

Wale wenzangu na miye wazee wa kuchungulia pm za Wadada tulifunga breki kwenye Pm ya Nifa kwani kwa sisi wataalamu wa mapenzi tunajua kabisa mapenzi yakikolea kwa kiwango cha juu kabisa si ajabu wapenzi kubadilishana simu na password. Hiyo ikaturudisha nyuma kwa kuhofia jasusi ana-access na account ya Nifa.

Wapo waliofurahishwa na habari hizo. Wapo pia waliohuzunishwa.
Nimewasiliana na jasusi yeye kwa uchovu kabisa alinijibu kuwa imeisha! Imeisha Mtibeli.
Nikamwuliza shida nini, akaniambia kumbe walikubaliana mwaka huu warasimishe. Na kama hawatarasimisha basi binti atachukua uamuzi mgumu.

Kuna mdakaji, mdakuzi, na mdukuzi. Kwenye mambo ya ujasusi bhana.
Jasusi kazidiwa kete na mojawapo hapo.
Ilipohitimu mwezi wa nane mambo yakawa mambo. Mojawapo hapo juu akamzidi jasusi.

Hata hivyo Jasusi kwa nilivyomsikiliza, taarifa hizi hazimuumi sana. Kingine ni kuwa kama mjuavyo binti yetu ndio alipenda zaidi kuliko jasusi mbobevu.

Ngoja tuendelee na nyimbo hapa kwenyw mkesha
Kwenye maombi 12 umejibiwa mangapi? Mimi nilipokea miracle money.
 
Miaka HII WANAUME TUMEBAKI WACHACHE SANA. YAANI MTU KABISA UNAKUJA ANZISHIA UZI UHUSIANO WA MTU MWINGINE, ARE YOU NORMAL? NI AIBU HATA KUZUNGUNZIA. LENGO NINI? UONEKANE UPO KARIBU NA MTALAKA? THEN? WANAUME WAZAMANI ILIKUWA HUWEZI JADILI MAHUSIANO YA MTU MWINGINE. ULIKUWA MWIKO KABISA.
Hivi kumbe chizi uwaga una akili saa zingine eeh?
 
Back
Top Bottom