Katika interview moja Jay Z alihojiwa na moja ya swali aliloulizwa ni kuhusu yeye huwa anajisikiaje hasa pale anapokumbuka au kuona jinsi alivyoharibu maisha ya vijana Kwa kuwauzia Madawa ya kulevya (Drugs)
Na akaulizwa je amewahi kuwatafuta waathirika wa madawa au kuwaomba msamaha Kwa kile alichowafanyia .
Alijibu hivi
Jay -Z sijamtafuta MTU yeyote kumuomba msamaha na ni kweli nakubali niliharibu maisha ya vijana Kwa kuwauzia madawa ya kulevya Ila wakati nafanya yote hayo nilikuwa na ufahamu tofauti na ambao ninao sasa hivi. ( I had different level of consciousness than I have today ).
Na mwisho akasema yeye haitaji kumuomba msamaha MTU yeyote ikiwa hilo deni la kuharibu vijana hajalilipa basi IPO siku atalilipia.
Akamaliza Kwa kutilia mkazo Kwa hii sentence.
"You can't sacrifice someone's life for your life because there's is karmax debt has to be paid"
Hivyo Jigga au Jay z anaelewa mambo mengi kuhusu universe , kwamba ikiwa utafanya ubaya lazima utaulipia haitajiki hata kutafuta public sympathy au kuomba msamaha mbele za watu.
Interview hii aliifanya na "the new York times" unaweza kuitazama YouTube