JB: Mganda huyu ni nani na anafanya nini Tanzania?

JB: Mganda huyu ni nani na anafanya nini Tanzania?

biashara zote alizonazo there's no way atakua analipa full tax TRA. lazima kuna watu wanapoozwa nae. aisee mganda yuko nchini hapa na anafanya vizuri hivi....kuna mbongo ambae yuko kenya or UG ambae ana miliki vitu kama huyu jamaa??
 
Unayoysema inawezekana yakawa ya ukweli. Lakini MMJ alipouliza huyu mtu ni nani ana habari gani zilimzomfanya amuulizie? MMJ inabidi arudi hapa atwambie. Hata hivyo, huyu mtu ananikumbusha ya "Mark Twist Kinyanjui" kwa wale waliokuwepo enzi zile!!!!

Tiba

Mkuu hata mimi nilikuwa namfikilia jamaa huyo wa Kenya lakini nikasahau jina lake, nachotaka kusema Watanzania wakati mwingine tunakosa kuwa makini sana-hakuna anaye mchukia mtu mwekezaji au tycoon; lakini vile vile siyo vibaya kuhoji mambo ambayo hayaja kaa sawa/tia shaka.

Ni vizuri Watanzania ku-emulate umakini wake katika mambo ya biashara kama kweli RITZ anayoyazungumza humu yote ni yakweli; kitu kingine kinacho nishangaza ni hiki watu kuwa na impression kwamba Watanzania tuna kasumba ya kwamba kila tajiri lazima awe ragi nyeupe-mbona Watanzania wamehoji sana kuhusu utajiri unao tia shaka wa Watanzania wenzetu wenye asili ya ASIA na ikaja kugundulika baadae kwamba Watanzania walicho kuwa na shaka nacho ni cha kweli kabisa, sasa kuna mantiki gani wanapohoji kuhusu waswahili wenzetu baadhi yetu tunakasilika!

Mbona kuna Watanzania matajiri, na wengine wamesoma LSE huko Uingereza lakini are not stinking rich! Je Watanzania walio wengi wako fast asleep?
 
Mwanakijiji habari yako haijakamilika kwa uwa inaacha maswali mengi kuliko majibu, na umeiandika katika lugha ya kijiweni kwa mimi nasikitika kuiita habari hiyo ni majungu na siko tayari kuchangia upuuzi huo zaidi ya kukuambia tumia lugha fasaha kuwasilisha usemacho kama hujui kiswahili andika hicho kiingereza chako na kama hujui kiingereza fasaha andika kiswahili fasaha.

Jamani, mbona kafanya uchonozi uliotuwezesha wengine tujue yaliyokuwa hayajulikana?

Ugomvi binafsi msiundekeze jamani.....alah!
 
Kumbe asili yake alikuwa Mjeda hapo kuna walakini!
Alafu mkuu wa nchi anapenda tumia watu ivi wakija mzika izo ela si ataja kufa kwa kihoro!
Maana kuna jamaa anasimamia miradi yake Uko Iringa!
Ivi hajui haya yote yatawekwa hadharani yeye akiondoka madarakani.
Labda aibadili ile sheria inayotaka viongozi wakuu baada ya kuitumikia nchi lazima wabaki nchini
 
Belmont...acha huyo tu, kuna waganda, makongo kibao wanaofanya kazi ya utapeli tu kwenye sekta ya madini..wanajiita generals, kanali, waasi kutoka kongo..kumbe matapeli wakubwa..mwaka jana walitutapeli fedha nyingi tu, wakakimbia zao kongo..lakini kibaya zaidi hawa jamaa huwa wakishatapeli hugawa fungu kwa polisi..ili wsikamatwe..wameharibu kabisa sekta yetu ya madini...na njia yao kubwa wanayotumia..ilikuishi hapa ni kuoa mabinti wa kitanzania na kuzaa nao ili kuhalalisha uwepo wao hapa nchini..nashangazwa na kusikitishwa sana na hali kama hii

Wenzetu wa nchi nyingine wako makini na mbinu hizi, hawakubali kabisa kukupa uraia hata kama umeoa mabinti zao! Actually niliwahi kushuhudia jamaa kagombana na mkwewe mzungu walipo kwenda POLISI - polisi na watu wa immigration wakawa wanamsihi mama huyo aseme kwamba amtaki tena mumewe hili wapate kisingizio cha kum-deport unceremoniously kurudi kwao Africa.
 
Kuna pia huyu jamaa anayeitwa JB kule Kigamboni ... ananunua viwanja na mashamba kwenye prime areas kule kwa kasi ya kutisha. Kama sijakosea kule wananchi wanamfahamu kama ni Mrundi na sio Mganda, sasa hii misconception sijui ni kama inafanywa na yeye purposely au wananchi wanashindwa kutofautisha sababu ya lafudhi yake. Anajenga sehemu nyingi pia kule gezaulole, na ni maarufu sana kwa vijana na mafundi ujenzi kule sababu ya kazi nyingi anazowapa ... pale Gezaulole ukimuuliza kijana yeyote kule kuhusu JB hatoshindwa kukupa stori zake na uwekezaji wake kule.

Naomba kufahamishwa, hivi sheria zetu za umiliki wa ardhi siku hizi zinaruhusu mtu asiye raia wa Tanzania kununua na kumiliki ardhi??

Kwani unashangaa nini mkuu, hata Raisi Kabira Sr. alipokuwa pale msasani akifanya biashara yake ya kihini macho alikuwa anajulikana kama Mganda kwa jina la MTWALE, at least hiyo ilikuwa kama kinga kwa usalama wake - na serikali ilikuwa inalijua hilo-kama unayo zungumza humu ni ya kweli basi hii ni hatari sana! Umakini wa Kambarage kuhusu usalama na hatma ya TAIFA letu umeyeyukia wapi jamani. Haya ni mambo ya kawaida kweli!!!!!

Nisije kueleweka vibaya, mimi sina tatizo na Waganda ni majirani zangu na nina ndugu zangu huko na najua kuzungumza lugha yao, na kwa kawaida si watu wa shari na ugomvi ni wafanya biashara mahili sana, actually wana msemo wao usemao "ESENTE TEKUBA NYONYI" ni wahangaikaji kweli, awalazi damu.

Having said that, tusije tukajisahau kwamba kila mtu anaitakia mema nchi yetu - tuwe makini kujua ki-undani washirika wao ni akina nani au wenyewe ni proxy TU.
 
Ritz,

Utajuaje usipouliza maswali?

So mjadala huu ni huru props and opps leteni ushahidi/taarifa sisi tunaendelea kudadavua.
 
Hiyo hoteli ilikuwa ya mzee mmoja wa kisomali mmiliki wa City Garden hoteli, pale posta
Hapa sasa tunakuja kwenye issue....na nadhani hapa ndo kuna basis ya maswali ya Mwanakijiji.....Watu wamekazania kujadili lifestyle ya mganda JB na kusahau bigger picture......Kwa navojua mmiliki wa awali kabisa wa hotel zooote zinazoitwa Paradise ni huyu msomali/wasomali......Nadhani jina la JB kama mmiliki wa Paradise limejitokeza baada ya yeye kuuziwa hiyo Paradise hapo Mkapa towers na huyu Msomali/wasomali......Nachofahamu tu ni kwamba huyu msomali mmiliki wa paradise amekua tz kwa deal hizi za hotel kwa muda mrefu na kwa chini chini anahusishwa na kula deal kubwa na watawala(waliopo/walopita)......Kwa wasiojua.....huyu msomali ndie aliyekuwa mmiliki wa ile hotel kali sana ya Paradise Bagamoyo hotel....which was one of the best hotels in TZ (nimeshahudhuria semina nyingi pale)....Kama mjuavyo hotel hii iliungua na kuteketea kwa moto totally....Baada ya kuungua..watu wa karibu(haswa wahudumu)..walikuja na tetesi kuwa ile ilikuwa planed arsenal (toka kwa wamiliki)...ili wapige hela za bima...kwani hotel ilikuwa na bima....sasa sijui kama hizi ni tetesi za kweli au vipi na kama jamaa alipiga hela ya bima au la...lakini word went around about that...Sasa leo naskia kamuuzia JB Paradise ya Mkapa towers!!!....something is very fishy here.........only time will tell....keep on probing Mwanakijiji.....
 
Tuanze kwa kujua kwanini alikosana na Rais wa maisha bwn m7
 
Mzee Mwanakijiji.

Mbona Wazungu matajiri wa Tanzania utaki kufahamu habari zao wewe na weusi tu.

Mbona hujauliza yule Mzungu mmiliki wa Hoteli ya Sleep Way, ni nani na anafanya nini Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Namfahamu kama Mmiliki wa CHICKEN HUT (MLIMANI CITY) kuanzia mwaka 2008, katika mazungumzo yetu alikuwa akijifagilia kama yeye ana pesa na yupo karibu sana na familia ya kwanza Tanzania, akidai anajenga Beach Hotel Bagamoyo, Hotel/Restaurant nyingine pale Africana.

SIKUAMINI SANA KWANI NILIONA NI SOUND TU! Baada ya kufunguliwa kwa QUALITY CENTRE! YAMETIMIA! Ana Restaurant/Ukumbi wa Disco (Savannah) Maduka makubwa matatu achilia mbali JB BELMONT iliyopo BW. Mkapa Towers.

Ninachompendea yupo down to earth!

Hivi Tanzania ukiwa au ukitaka kuwa muwekezaji sharti uwe na urafiki na familia ya mkuu wa kaya? Maana kila anayewekeza hii nchi anapaswa kwanza awe rafiki wa hii familia kwa sababu zipi hasa? Nadhani kuna tatizo la msingi katika hili na hatupaswi kucheka na kufurahia hili. Shaka yangu ni kuwa kama ni hivyo watu hawa kuna kitu wanafanya ambacho si cha kawaida na kwahiyo wanahitaji ulinzi wa familia ya mkuu wa kaya.
 
Mnaulizwa
JE ANAWEZA KUWA TATIZO TANZANIA?

Na ni swali la kawaida kabisa...mara nyingi watu wengi tunafanya mambo kwa mazoea na hatutaki kuangalia zaidi ya pale macho yetu yanapoishia. Ndio maana tumepotea sababu sifa kubwa leo ya watanzania ni mtu kuwa na hela nyingi bila hata kujiuliza hizo hela zinapatikana vipi. Mwisho wa yote ndio hili Taifa tunaloliona...limejaa wezi mpaka kwenye levels usizoweza kufikiria.
 
Kumbe asili yake alikuwa Mjeda hapo kuna walakini!
Alafu mkuu wa nchi anapenda tumia watu ivi wakija mzika izo ela si ataja kufa kwa kihoro!
Maana kuna jamaa anasimamia miradi yake Uko Iringa!
Ivi hajui haya yote yatawekwa hadharani yeye akiondoka madarakani.
Labda aibadili ile sheria inayotaka viongozi wakuu baada ya kuitumikia nchi lazima wabaki nchini

Tutawezaje kujua kama anaifanyia kazi za siri serikali ya Uganda? Ex soldier aachiwe analanda landa hivi hivi? Hii dunia yote could be in a total mess!
 
Unajuwa ni kitu gani kilichosababisha mpaka huyu JB akakosana na M7?

Tutajuaje kama kweli alikosana na Museveni? Maana hata Marehemu Shekhe Yahya alikaa sana Kenya sababu eti "aligombana Nyerere".
 
Ujinga kama huu wako ndio janga halisi la kitaifa-watu kupenda uzushi au ku-conclude mambo bila hoja au ushahidi wowote!JB(ingawa simjui) ni janga la taifa kivipi?Halipi kodi?Yeye ndie anayefanya sisi tusifanye kazi na kuishia kuimba nyimbo za ufisadi na freemason?Kuna mtanzania amezuiliwa kufanya biashara Uganda?Tatizo letu ni elimu ya kukariri na kujibu mitihani ya darasani tu.Huu ndio utandawazi uliokariri darasani,watu wanazunguka dunia nzima kutafuta business opportunities.Acha JB afanye kazi huku sisi tukiendeleza porojo zetu za kuogopa kujiunga na EAC kwa sababu ya uvivu wetu.Unamwita JB malaya na kusahau kuwa kama ni umalaya si anaufanya na Watanzania wenzetu,kwa nini tusiwalaume hao watanzania wenzetu,let's deal with our own failures first.

Umemaliza yote niliyotaka kusema! Hivi nani katuloga watanganyika? Pokea LIKE!
 
Naomba nitofautiane na wewe, huyu ni MWEKEZAJI!

Ametoa ajira lukuki kwa wa~Tanzania tofauti na hao Wafanyakazi wa kigeni WACHINA/WAHINDI/WAPAKISTAN etc. zaidi ya 10,000
wanaokaa na kufanya kazi zinazoweza kufanywa na Wa-Tanzania!
Tusker Bariiiidi Neno MWEKEZAJI linaweza kuwa kichaka kibaya sana cha wahalifu!
 
Last edited by a moderator:
Hapa sasa tunakuja kwenye issue....na nadhani hapa ndo kuna basis ya maswali ya Mwanakijiji.....Watu wamekazania kujadili lifestyle ya mganda JB na kusahau bigger picture......Kwa navojua mmiliki wa awali kabisa wa hotel zooote zinazoitwa Paradise ni huyu msomali/wasomali......Nadhani jina la JB kama mmiliki wa Paradise limejitokeza baada ya yeye kuuziwa hiyo Paradise hapo Mkapa towers na huyu Msomali/wasomali......Nachofahamu tu ni kwamba huyu msomali mmiliki wa paradise amekua tz kwa deal hizi za hotel kwa muda mrefu na kwa chini chini anahusishwa na kula deal kubwa na watawala(waliopo/walopita)......Kwa wasiojua.....huyu msomali ndie aliyekuwa mmiliki wa ile hotel kali sana ya Paradise Bagamoyo hotel....which was one of the best hotels in TZ (nimeshahudhuria semina nyingi pale)....Kama mjuavyo hotel hii iliungua na kuteketea kwa moto totally....Baada ya kuungua..watu wa karibu(haswa wahudumu)..walikuja na tetesi kuwa ile ilikuwa planed arsenal (toka kwa wamiliki)...ili wapige hela za bima...kwani hotel ilikuwa na bima....sasa sijui kama hizi ni tetesi za kweli au vipi na kama jamaa alipiga hela ya bima au la...lakini word went around about that...Sasa leo naskia kamuuzia JB Paradise ya Mkapa towers!!!....something is very fishy here.........only time will tell....keep on probing Mwanakijiji.....

Hivi hizi ransom wanazolipwa watekaji nyara meli zanikwenda kuwa-invested WAPI!!! Kenya, Tanzania, Uganda au wapi? Sijawahi kusikia zinakuwa invested SOMALIA - kwa nini? Hivi huu urafiki wa ghafla wa wasomali kumwamini mswahili umetoka WAPI!
 
Back
Top Bottom