JB: Mganda huyu ni nani na anafanya nini Tanzania?

biashara zote alizonazo there's no way atakua analipa full tax TRA. lazima kuna watu wanapoozwa nae. aisee mganda yuko nchini hapa na anafanya vizuri hivi....kuna mbongo ambae yuko kenya or UG ambae ana miliki vitu kama huyu jamaa??
 

Mkuu hata mimi nilikuwa namfikilia jamaa huyo wa Kenya lakini nikasahau jina lake, nachotaka kusema Watanzania wakati mwingine tunakosa kuwa makini sana-hakuna anaye mchukia mtu mwekezaji au tycoon; lakini vile vile siyo vibaya kuhoji mambo ambayo hayaja kaa sawa/tia shaka.

Ni vizuri Watanzania ku-emulate umakini wake katika mambo ya biashara kama kweli RITZ anayoyazungumza humu yote ni yakweli; kitu kingine kinacho nishangaza ni hiki watu kuwa na impression kwamba Watanzania tuna kasumba ya kwamba kila tajiri lazima awe ragi nyeupe-mbona Watanzania wamehoji sana kuhusu utajiri unao tia shaka wa Watanzania wenzetu wenye asili ya ASIA na ikaja kugundulika baadae kwamba Watanzania walicho kuwa na shaka nacho ni cha kweli kabisa, sasa kuna mantiki gani wanapohoji kuhusu waswahili wenzetu baadhi yetu tunakasilika!

Mbona kuna Watanzania matajiri, na wengine wamesoma LSE huko Uingereza lakini are not stinking rich! Je Watanzania walio wengi wako fast asleep?
 

Jamani, mbona kafanya uchonozi uliotuwezesha wengine tujue yaliyokuwa hayajulikana?

Ugomvi binafsi msiundekeze jamani.....alah!
 
Kumbe asili yake alikuwa Mjeda hapo kuna walakini!
Alafu mkuu wa nchi anapenda tumia watu ivi wakija mzika izo ela si ataja kufa kwa kihoro!
Maana kuna jamaa anasimamia miradi yake Uko Iringa!
Ivi hajui haya yote yatawekwa hadharani yeye akiondoka madarakani.
Labda aibadili ile sheria inayotaka viongozi wakuu baada ya kuitumikia nchi lazima wabaki nchini
 

Wenzetu wa nchi nyingine wako makini na mbinu hizi, hawakubali kabisa kukupa uraia hata kama umeoa mabinti zao! Actually niliwahi kushuhudia jamaa kagombana na mkwewe mzungu walipo kwenda POLISI - polisi na watu wa immigration wakawa wanamsihi mama huyo aseme kwamba amtaki tena mumewe hili wapate kisingizio cha kum-deport unceremoniously kurudi kwao Africa.
 

Kwani unashangaa nini mkuu, hata Raisi Kabira Sr. alipokuwa pale msasani akifanya biashara yake ya kihini macho alikuwa anajulikana kama Mganda kwa jina la MTWALE, at least hiyo ilikuwa kama kinga kwa usalama wake - na serikali ilikuwa inalijua hilo-kama unayo zungumza humu ni ya kweli basi hii ni hatari sana! Umakini wa Kambarage kuhusu usalama na hatma ya TAIFA letu umeyeyukia wapi jamani. Haya ni mambo ya kawaida kweli!!!!!

Nisije kueleweka vibaya, mimi sina tatizo na Waganda ni majirani zangu na nina ndugu zangu huko na najua kuzungumza lugha yao, na kwa kawaida si watu wa shari na ugomvi ni wafanya biashara mahili sana, actually wana msemo wao usemao "ESENTE TEKUBA NYONYI" ni wahangaikaji kweli, awalazi damu.

Having said that, tusije tukajisahau kwamba kila mtu anaitakia mema nchi yetu - tuwe makini kujua ki-undani washirika wao ni akina nani au wenyewe ni proxy TU.
 
Ritz,

Utajuaje usipouliza maswali?

So mjadala huu ni huru props and opps leteni ushahidi/taarifa sisi tunaendelea kudadavua.
 
Hiyo hoteli ilikuwa ya mzee mmoja wa kisomali mmiliki wa City Garden hoteli, pale posta
Hapa sasa tunakuja kwenye issue....na nadhani hapa ndo kuna basis ya maswali ya Mwanakijiji.....Watu wamekazania kujadili lifestyle ya mganda JB na kusahau bigger picture......Kwa navojua mmiliki wa awali kabisa wa hotel zooote zinazoitwa Paradise ni huyu msomali/wasomali......Nadhani jina la JB kama mmiliki wa Paradise limejitokeza baada ya yeye kuuziwa hiyo Paradise hapo Mkapa towers na huyu Msomali/wasomali......Nachofahamu tu ni kwamba huyu msomali mmiliki wa paradise amekua tz kwa deal hizi za hotel kwa muda mrefu na kwa chini chini anahusishwa na kula deal kubwa na watawala(waliopo/walopita)......Kwa wasiojua.....huyu msomali ndie aliyekuwa mmiliki wa ile hotel kali sana ya Paradise Bagamoyo hotel....which was one of the best hotels in TZ (nimeshahudhuria semina nyingi pale)....Kama mjuavyo hotel hii iliungua na kuteketea kwa moto totally....Baada ya kuungua..watu wa karibu(haswa wahudumu)..walikuja na tetesi kuwa ile ilikuwa planed arsenal (toka kwa wamiliki)...ili wapige hela za bima...kwani hotel ilikuwa na bima....sasa sijui kama hizi ni tetesi za kweli au vipi na kama jamaa alipiga hela ya bima au la...lakini word went around about that...Sasa leo naskia kamuuzia JB Paradise ya Mkapa towers!!!....something is very fishy here.........only time will tell....keep on probing Mwanakijiji.....
 
Tuanze kwa kujua kwanini alikosana na Rais wa maisha bwn m7
 
Mzee Mwanakijiji.

Mbona Wazungu matajiri wa Tanzania utaki kufahamu habari zao wewe na weusi tu.

Mbona hujauliza yule Mzungu mmiliki wa Hoteli ya Sleep Way, ni nani na anafanya nini Tanzania.
 
Last edited by a moderator:

Hivi Tanzania ukiwa au ukitaka kuwa muwekezaji sharti uwe na urafiki na familia ya mkuu wa kaya? Maana kila anayewekeza hii nchi anapaswa kwanza awe rafiki wa hii familia kwa sababu zipi hasa? Nadhani kuna tatizo la msingi katika hili na hatupaswi kucheka na kufurahia hili. Shaka yangu ni kuwa kama ni hivyo watu hawa kuna kitu wanafanya ambacho si cha kawaida na kwahiyo wanahitaji ulinzi wa familia ya mkuu wa kaya.
 
Mnaulizwa
JE ANAWEZA KUWA TATIZO TANZANIA?

Na ni swali la kawaida kabisa...mara nyingi watu wengi tunafanya mambo kwa mazoea na hatutaki kuangalia zaidi ya pale macho yetu yanapoishia. Ndio maana tumepotea sababu sifa kubwa leo ya watanzania ni mtu kuwa na hela nyingi bila hata kujiuliza hizo hela zinapatikana vipi. Mwisho wa yote ndio hili Taifa tunaloliona...limejaa wezi mpaka kwenye levels usizoweza kufikiria.
 

Tutawezaje kujua kama anaifanyia kazi za siri serikali ya Uganda? Ex soldier aachiwe analanda landa hivi hivi? Hii dunia yote could be in a total mess!
 
Unajuwa ni kitu gani kilichosababisha mpaka huyu JB akakosana na M7?

Tutajuaje kama kweli alikosana na Museveni? Maana hata Marehemu Shekhe Yahya alikaa sana Kenya sababu eti "aligombana Nyerere".
 

Umemaliza yote niliyotaka kusema! Hivi nani katuloga watanganyika? Pokea LIKE!
 
Naomba nitofautiane na wewe, huyu ni MWEKEZAJI!

Ametoa ajira lukuki kwa wa~Tanzania tofauti na hao Wafanyakazi wa kigeni WACHINA/WAHINDI/WAPAKISTAN etc. zaidi ya 10,000
wanaokaa na kufanya kazi zinazoweza kufanywa na Wa-Tanzania!
Tusker Bariiiidi Neno MWEKEZAJI linaweza kuwa kichaka kibaya sana cha wahalifu!
 
Last edited by a moderator:

Hivi hizi ransom wanazolipwa watekaji nyara meli zanikwenda kuwa-invested WAPI!!! Kenya, Tanzania, Uganda au wapi? Sijawahi kusikia zinakuwa invested SOMALIA - kwa nini? Hivi huu urafiki wa ghafla wa wasomali kumwamini mswahili umetoka WAPI!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…